Pole sana,pamoja na upungufu wako wa kibinadamu unastahili ushauri,kabla ya kuondoka na mwanao nakusihi kaa chini na mume wako na uzungumze naye kuhusu hilo,naye pia ana mapungufu kama ulivyokuwa nayo wewe,tangu ulipoweka ile thread ya kumtaka mume wa mtu nilishahisi una tatizo na mume wako,kaeni chini mzungumze kwa uwazi,kama nyote mko tayari kuimarisha ndoa kwa kubadilika na kujifunza kuvumiliana na kukataa tamaa mbaya kadri ya uwezo wenu poa,kama mtaamua kuachana,then sawa,nitakutakia kila la kheri,ila tulia kwanza na fanya uamuzi hasira ikiwa imepungua kidogo........sikuzote kumbuka si vizuri kuyakimbia matatizo ni vizuri kuyakabili manake huko uendako yaweza kuwa makubwa zaidi.