Sikuwa mjinga, niliamini niko sahihi, leo Ndugai amejibu


Details za mkataba ziwekwe hadharani ili tuuchambue kwa kina. Jiwe akiwa Mbunge na Waziri wa Ujenzi halikutia neno bungeni kuhusu mkataba huo.
Huo mradi wa Bagamoyo as long as yupo Mchina, sisi wabongo tunapaswa kuutazama mkataba kwa upya neno nadi neno...wale wapumbavu macho madogo wana hila kuliko mwanadamu yoyote juu ya uso wa nchi...
 
Njama kuu zinatokea South Africa kwani Bandari ya Darban ndiyo Bandari kuu kwa upande huu na ndiyo tegemezi kwa zimbabwe Botswana Zambia na hata msumbiji yenyewe hivyo uwepo wa Bandari kubwa mpya ni pigo kwa Bandari za Angora, Tanzania, kenya congo Brazzaville nk
 
Mnajikuta mnaujua mkataba kuliko Mzalendo namba moja, JPM. Wote mnaoshabikia kuliuza taifa letu pendwa hakika laana hii itakuwa juu yenu na vizazi vyenu.
Marehemu alitikisa kiberiti avute mpunga tokea kwa Wachina lakini kwa kuwa ile kampuni ni ya Serikali wakagoma kwa kudai kuwa tayari walitumia pesa nyingi kulipa wakazi wa Bagamoyo fidia na kufanya upembuzi yakinifu kwa gharama kubwa ndipo marehemu akaamua kuwasingizia kuwa watakusanya mapato wenyewe pasipo gawio na mengineyo kwa lengo la kuwakomoa, Cha muhimu ni Mkataba kuanikwa wazi hata kwenye mitandao au hata magazeti ili watanzania wote wauchambue vizuri wapate kubaini mapungufu yote kisha waje na jawabu sahihi la kufanikisha ujenzi wa Bandari pasipo Athari kwa pande zote mbili
 
Bandari za Dsm Tanga mtwara haziwezi kufa kwani ni mapito ya meli nyingi zikiwa njia kuelekea sehemu nyingi Duniani na pia zinaweza kutumika kama Bandari ya Capetown, Pot Elizabeth, East London za kule South Africa zinavyotumika kuleta bidhaa za ndani ya Nchi na pia kupokea meli za kitalii, Bandari ya Bagamoyo itakuwa Bandari ya kimataifa tu ili kuileta Tanzania iwe Dubai ya Africa kwani Reli na uwanja mwingine wa Ndege za mizigo vitajengwa Bagamoyo na kuipelekea Bagamoyo kuwa jiji kubwa Barani Africa, mikataba irejewe upya itengenezwe mikataba isiyo na shaka kwa watanzania
 
Details za mkataba ziwekwe hadharani ili tuuchambue kwa kina. Jiwe akiwa Mbunge na Waziri wa Ujenzi halikutia neno bungeni kuhusu mkataba huo.
Mikataba ya awali Magufuli alikubali pasipo kuweka pingamizi alipoingia ikulu akawageuka Wachina akijua wataleta mpunga mwingi kumbe Wachina nao wana hesabu zao zingine kwenda Nchi zingine ambazo hakuna magumashi kama Tanzania
 
Yale yale tulipinga Chato sasa ni Bagamoyo. Haya ni mapambano ya wakubwa wawili. Samia asiingizwe kwenye vita hii should remain neutral na atekeleze miradi ya urithi. Ushauri.
 
Huo mkataba umeuona? Ndugai anadai Rais alikua misled? Rais anadai mkataba ni mbaya.

Suluhu draft ya mkataba upelekwe bungeni kuliko mnachukua speculation tu za wanasiasa.

Yani hujauona hata ila umeanza kuukosoa?
 
Huo mkataba umeuona? Ndugai anadai Rais alikua misled? Rais anadai mkataba ni mbaya.

Suluhu draft ya mkataba upelekwe bungeni kuliko mnachukua speculation tu za wanasiasa.

Yani hujauona hata ila umeanza kuukosoa?
Rais alituambia kwanini mkataba haukuwa to our national interests; sababu alizozitoa ni genuine unless uwe umenunuliwa na wachina!!!

Ndugai hajasema kwanini anadhani Rais was misled [ maneno ambayo aliogopa kusema mwendazake alipo kuwa hai] kitu kinachoonesha jinsi alivyokuwa mnafiki!!
 
Kwanini unaamini Rais yupo sahihi na Ndugai ni muongo? Ilihali mkataba hujawahi kuuona?

Si JPM hyu hyu alidanganya kuwa ATCL inatoa gawio/Dividend kumbe hta hawaja break even wala kucover operating expenses toka 2016!!

Nadhani ingefaa tupige kelele mikataba iwe reviewed na kamati za bunge kuliko kurely kwenye maneno ya populists!!
 
Kuhusu Bandari ya bagamoyo,haujadadavua vzr,kipengere Cha miaka 99,umekuwa shallow sana,
 
Huu mradi wa bagamoyo ujadiliwe kwa kina kabla ya kuamuliwa Cha kufanya, ndugai haaminiki.Kwa Nini asubiri mpaka jpm afe ndo aseme? Je hoja za Jpm zimejibiwa ipasavyo?
 

Attachments

  • 2736317-18d679f7a5f0d520b2b3467822105fdc.mp4
    5.5 MB
Mnajikuta mnaujua mkataba kuliko Mzalendo namba moja, JPM. Wote mnaoshabikia kuliuza taifa letu pendwa hakika laana hii itakuwa juu yenu na vizazi vyenu.
Ndugai kabadilika ghafla, sielewi Kuna nn.Tatizo kuu la viongozi wetu ni unafiki, yaani spika wa bunge anamuogopa rais kutoa ushauri kwa maslahi ya taifa?
 
Moja, Mkataba umeuona au unajitia jasusi lakiuchumi huku huna data!!
Pili, kuzuia madini lilikuwa jambo lisilofaa? Na je, unajua nini kinachelewesha ujenzi wa mitambo ya uchenjuaji?

Tatu,je unajua uharamia wa Rwanda kwenye madini ya Congo? Unadhani mitambo ya kuchenjua wanajenga wakitegemea madini ya tz?

Tusiwe wepesi kurukua hoja nyeti bila deep study! Utajiita jasusi kumbe nibange tuu zinakusumbua lkn huna welewa wa kutosha kwenye mada unazosimamia!
Jifunze kwanza kabla ya kufunza la utaponza wengine!!
 
SWALI KWA WASUKUMA:

UWANJA WA NDEGE CHATO ILIKUWA SAWA ILA BANDARI YA BAGAMOYO SIO SAWA?

MKATABA UWEKWE WAZI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…