Sikuwa mjinga, niliamini niko sahihi, leo Ndugai amejibu

Sikuwa mjinga, niliamini niko sahihi, leo Ndugai amejibu

Kwanini mkataba huo unapingwa na pande mbili? Upande mmoja wanasema mkataba una mapangufu na upande mwingine una ukubali mkataba huo? Kwa kunzana hivi, ni dalili tosha kuwa mkataba huo una walakini.

Muhimu mkataba huo uwekwe hadharani, ili anayetaka kusoma asome. Mwenye mkataba huo aweke hapa. Hata kama na wewe Yericko Nyerere unao huo mkataba tuweke hapa na sisi tuupitie.
 
Tafuta michango yangu humu kuhusu mradi wa Bagamoyo...... Niliandika humu kuhusu multiplier effect ya mradi kwamba ina outscore hasara za mradi.

Shida watu waliangalia kodi tu na kupanua Bandari zingine ila hawaangalii ukubwa wa mradi kwamba una faida lukuki za long term. Mfano kwa ukwasi mabenki yetu, Ajira (Indirect), Enterprise growth, spillover ya teknolojia, suppliers, feeding SGR, ATCL etc, aaah name it

Hayo ndio ya kufocus sio kelele za miaka 99 sijui nchi kuuzwa kana kwamba negotiatiors wetu hawana

Wewe tunakujua ni magna njaa anataka kutumia economics yako uchwara kutaka kupata /umepeta cut yako toka kwa Vasco Dagama na Wachina!!

Let me ask you , the so called multiplier effects from the project will they only happen when the country commits to a $10 billion loan with those harsh conditions? Can't the multiplier effects from the project could as well happen if the country takes its stock and at the appropriate time invest in the project from its own internal sources!!!

YUO DO NOT LIKE THE SECOND OPTION BECAUSE YOU HAVE ALREADY TAKEN YOUR 10% FROM THE CHINESE AND NOW YOU ARE CONFUSED AS TO HOW YOU ARE GOING TO PAY THEM BACK!
 
Wewe tunakujua ni magna njaa anataka kutumia economics yako uchwara kutaka kupata /umepeta cut yako toka kwa Vasco Dagama na Wachina!!

Let me ask you , the so called multiplier effects from the project will they only happen when the country commits to a $10 billion loan with those harsh conditions? Can't the multiplier effects from the project could as well happen if the country takes its stock and at the appropriate time invest in the project from its own internal sources!!!

YUO DO NOT LIKE THE SECOND OPTION BECAUSE YOU HAVE ALREADY TAKEN YOUR 10% FROM THE CHINESE AND NOW YOU ARE CONFUSED AS TO HOW YOU ARE GOING TO PAY THEM BACK!
Tofautisha mkopo na guarantee!! Wao wanawekeza.... Serikali inakua guarantor tu.

HATA KAMA bahati mbaya ungekua mkopo na bandari wanaendesha wenyewe unachoogopa ni nini? Kwanini mnawaza itafeli tu hamuangalii potential for growth?

SGR tumekopa trillion ngapi? Mbona hamuogopi tukishindwa kulipa waturuki watatupora reli, ila mkisikia tu bagamoyo basi mnawaza kuporwa bandari? Mbona waliwajengea kambi ya jeshi na hamkutoa povu?

Embu tuwe logical tuache conspiracy theory
 
Hapa we umewakilisha maoni tu hujawekwa indicators za mkataba.

Kupitia maoni yako tu kuna mapungufu tayari, kama sheria zetu zinaruhusu uwekezaji wa 33yrs na 99yrs kwanini sisi tukasaini miaka 99 tukaacha miaka 33?
Uwekezaji wa trillion 20+ una break even ndani ya miaka 33??
 
Tofautisha mkopo na guarantee!! Wao wanawekeza.... Serikali inakua guarantor tu.

HATA KAMA bahati mbaya ungekua mkopo na bandari wanaendesha wenyewe unachoogopa ni nini? Kwanini mnawaza itafeli tu hamuangalii potential for growth?

SGR tumekopa trillion ngapi? Mbona hamuogopi tukishindwa kulipa waturuki watatupora reli, ila mkisikia tu bagamoyo basi mnawaza kuporwa bandari? Mbona waliwajengea kambi ya jeshi na hamkutoa povu?

Embu tuwe logical tuache conspiracy theory
Mradi hautatekelezwa na kizazi hiki
 
Mradi hautatekelezwa na kizazi hiki
Kwani wewe ni nani? Kamati ya bajeti imeshapeleka pendekezo na spika amelipa endorsement. U r nothing zaidi ya mpiga kelele tu wa mitandaoni.

Unachopaswa kukubali JPM ameshaondoka and he's never coming back no matter wat u do or say.
 
Tofautisha mkopo na guarantee!! Wao wanawekeza.... Serikali inakua guarantor tu.

HATA KAMA bahati mbaya ungekua mkopo na bandari wanaendesha wenyewe unachoogopa ni nini? Kwanini mnawaza itafeli tu hamuangalii potential for growth?

SGR tumekopa trillion ngapi? Mbona hamuogopi tukishindwa kulipa waturuki watatupora reli, ila mkisikia tu bagamoyo basi mnawaza kuporwa bandari? Mbona waliwajengea kambi ya jeshi na hamkutoa povu?

Embu tuwe logical tuache conspiracy theory

Kwanini mnang'ang'ania huo mkopo wa $10 bill. hamtaki kujenga kutumia internal resources? Kama sio Ufisadi wenu ni nini?
 
Huu mkataba wa bandari ya Bagamoyo usipowekwa wazi kwa wananchi hakuna upande wa kuuamini. Kujadili hili jambo ni kulenga shabaha gizani tu.
Ni kweli ni kulenga shabaha gizani
 
Kwanini mnang'ang'ania huo mkopo wa $10 bill. hamtaki kujenga kutumia internal resources? Kama sio Ufisadi wenu ni nini?
SGR mmetumia pesa za ndani? Au mnadhani kuna 20 Trillion za kumwaga tu?
 
Kama ambavyo awamu ya tano ilificha ficha taarifa na ninyi ndivyo mnavyokazana kuficha ficha mikataba ya huo mradi, mkataba upelekwe sehemu husika, upitiwe upya na wananchi tuambiwe ABC, ili siku yakianza kwenda ndivyo sivyo tujue wakumshika shati.

Msitumie hizi kelele za kukosolewa kwa awamu ya tano kupitisha mambo yenu binafsi. Hii nchi ni yetu sote.
we kweli kiziwi hivi kuna mkataba gani uliowekwa wazi? kwa kawaida utaelezwa vipengele vyenye changamoto na kwanini umekataliwa, kwa msaada zaidi tazama au sikiliza hotuba ya aliyekuwa Mkurugenzi wa TPA Mr Kakoko na vyombo vya habari alielezea ni kwanini wameukataa, pia sikiliza hotuba ya Mh Rais. hata ukigoogle utazipata hizo video
 
Mnahangaika kuujibu huu mjadala lakini mimi nauona umekaa kibiashara zaidi,mtoa mada hajarudi kujibu hoja yoyote zaidi ya ile aliyoulizwa kitabu kinapatikanaje😃
 
acha ujinga yericko, mradi wowote ambao unazungumzia kutokulipa kodi huo ni mradi wa kipumbavu.
 
Mkataba kamau huo umetekelezea huko Sri Lanka na wanalia nao sana.
Leo Tz Mnataka tucheze karata hiyohiyo ya wachina.?
Nasema HAPANA.

Tuwe makini sana katika hili.
 
we kweli kiziwi hivi kuna mkataba gani uliowekwa wazi? kwa kawaida utaelezwa vipengele vyenye changamoto na kwanini umekataliwa, kwa msaada zaidi tazama au sikiliza hotuba ya aliyekuwa Mkurugenzi wa TPA Mr Kakoko na vyombo vya habari alielezea ni kwanini wameukataa, pia sikiliza hotuba ya Mh Rais. hata ukigoogle utazipata hizo video
Tabia ya watu wawili watatu kukaa kujifungia na kujisomea mkataba pekeyao na kuusaini au kukataa kuusaini ni vitu ambavyo kama taifa tunapaswa kuvipinga kwa nguvu zote. Wakijakutusimulia tutajuaje kuwa hawavutii upande wao?

Hiyo mikataba ipitishwe hata katika kamati husika za bunge, ipitiwe na jopo la watu, sio vimtu vitatu vipitie pekeyao halafu waanze kutusimulia umbeya.

Who is kakonko? mimi mwananchi wa kawaida nitajuaje kuwa Kakonko anasema ukweli? na wewe mwananchi wa kawaida ambaye hujauona mkataba unajuaje kuwa kakonko anasema ukweli mpaka tumtumie kama rejea?
 
Tabia ya watu wawili watatu kukaa kujifungia na kujisomea mkataba pekeyao na kuusaini au kukataa kuusaini ni vitu ambavyo kama taifa tunapaswa kuvipinga kwa nguvu zote. Walijakutusimulia tutajuaje kuwa hawavutii upande wao?

Hiyo mikataba ipitishwe hata katika kamati husika za bunge, ipitiwe na jopo la watu, sio vimtu vitatu vipitie pekeyao halafu waanze kutusimulia umbeya.

Who is kakonko? mimi mwananchi wa kawaida nitajuaje kuwa Kakonko anasema ukweli? na wewe mwananchi wa kawaida ambaye hujauona mkataba unajuaje kuwa kakonko anasema ukweli mpaka tumtumia kama rejea?

Exactly

Maoni: Misingi ya Usalama wa Taifa. Sizungumzii TISS
 
Hebu acha kumuita huyo jambazi I mzalendo.

Mnajikuta mnaujua mkataba kuliko Mzalendo namba moja, JPM. Wote mnaoshabikia kuliuza taifa letu pendwa hakika laana hii itakuwa juu yenu na vizazi vyenu.
 
SIKUWA MJINGA, NILIAMINI NIKO SAHIHI, LEO NDUGAI AMEJIBU.

Na Yericko Nyerere

Job Ndugai mfuasi kindakindaki wa hayati John Magufuli aliyeapa kumuongeza muda wa kutawala Tanzania, ananirejesha nyuma miaka miwili iliyopita 22 December 2019 nilipoandika Makala nikipinga hotuba ya Rais Magufuli akikataa kuendelea na ujenzi wa Mradi ya Bandari ya Bagamoyo, nilipinga hoja alizozijenga Rais ili kuualalisha katazo lake juu ya mradi husika.

Nilieleza wazi kwamba, Kuna mambo katika nchi yanahitaji uchunguzi kubaini pengine kuna hujuma katika taifa, hii inatokana na michakato mingi muhimu ya kichumi na kijamii imekuwa ikiishia njiani na kuliacha taifa katika hasara kubwa. Hii ni hujuma inahitaji mwarobaini kulitibu.

Mifano ya michakato ambayo kwamiaka mingi imeikuwa ikiishia njiani ni kama vile sekta ya nishati ambapo uzalishaji wa umeme limekuwa jambo linalotumiwa kama mchakato wakuzuka na kufa kwa miaka mingi sana tangu mwaka 1994 ilipokuja kitu kinaitwa umeme wa dharula kuokoa taifa (IPTL), ikafata michakato mingi yenye kuumiza taifa na haikufanikiwa hadi tukafika kuchimba Gesi mtwara tukapoteza mabilioni, gesi hadi Kinyerezi, kufumba na kufumbua mradi umetelekezwa sasa tunaimba mradi wa Bonde la Rufiji. Twende tuendelee..

Serikali ya awamu ya nne ilianzisha mradi wa kimkakati kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara duniani, mradi huu ilikuwa ni kujenga bandari ya Bagamoyo kwa ubia kati ya China na Omani wenye thamani ya dola bilioni 10, Serikali ya Tanzania katika mradi huu ilikuwa haiweki pesa yoyote isipokuwa ardhi na raslimali zingine, huku Uchina na Omani wakiweka mtaji na utaalamu.

Kwamjibu wa mapendekezo ya mkataba wa awali wa mradi huo, ni kwamba kungeundwa chombo maalumu cha nchi zote tatu ambacho kingekusanya mapato ya mradi huu na kusimamia gawio la pande zote, hii inamaana kwamba TRA ya Tanzania isingekuwa na haki ya kukusanya mapato moja kwa moja kutoka katika mradi badala yake ingekusanya gawio toka kwa chombo cha wabia kinachokusanya mapato ya mradi wa nchi zote tatu.

Huu ni moja ya mradi ambo kimsingi ulikuwa umeitangazia dunia vita vya kiuchumi toka kwa washindani wetu ambao ni nchi jirani na zinazotuzunguka. Kwakuwa Afrika yote ingepokelea bidhaa zake toka ulimwenguni hadi Bagamoyo, sawa na ilivyo Dubai ambayo ndio mlango wa Afrika kupokelea bidhaa zake.

Afrika inaingiza bidhaa toka Uchina kwa 88.8% na kiwango cha 98% ya bidhaa hizo zinapita Dubai. Hivyo kujengwa kwa Bandari ya Bagamoyo kungefunga nyia ya Dubai na bidhaa zote za Afrika kutoka China kupita Bagamoyo. Hii inamaana kwamba uchumi wa Dubai na Marekani ambayo ndio mdau mkuu ungemegwa. Mradi huu ulikuwa ndio msingi halisi wa kuanzisha mradi wa reli ya kisasa ya SGR, bila Bandari itakayozalisha mizigo kwa wingi SGR itakuwa ni kwakubeba abiria tu badala ya mizigo.

Serikali ya awamu ya tano katika hali ya kustaajabisha imeutupilia mbali mradi huo kwakutoa sababu ambazo hazina nguvu na zingine za kushangaza sana, mimi naitafsiri kama ni hujuma kwa taifa, izingatiwe kuwa tayari taifa lilishaingia gharama kubwa kuanzia kwenye upembuzi yakinifu, na kusaini mikataba ya awali. Kitendo cha kusitisha katika hatua hii ni kulitia hasara taifa. Moja ya hoja zilizotolewa na rais kama sababu ni kwamba masharti ya wabia nikuwa TRA hairuhusiwi kukusanya mapato, hoja hii ya Rais alikuwa sahihi lakini bahati mbaya alishindwa kufafanua wazi sababu za TRA kutokuwa miusanya mapato ya ubia. Pengine hili Rais alidanganywa.

Pili rais alisema kuwa masharti ya wabia nikuwa Tanzania hairuhusiwi kuendeleza bandari zake zingine. Hoja hii nayo inautata mwingi sana, Bandari zingine zote ziko kwaajili ya ndani, na mradi huu ulikuwa kwa shughuli za kimataifa. Sasa hoja ya kuwa tusikarabati bandari zetu zilizopo ni hoja isiyo na mashiko, Hili inawezekana kabisa Rais hakuambiwa ukweli.

Hoja ya Tatu aliyoitumia Rais Magufuli kukataa mradi ule, ilikuwa kwamba, wabia wanataka wapewe umiliki wa ardhi kwa miaka 99. Hili si la mwekezaji bali la sheria zetu ambazo zinatoa uwekezaji katika ardhi kwa miaka 33 hadi 99. Sasa hoja hii haiwezi kuwa kwa wabia wawili tu kati ya watatu ikiwemo Tanzania yenyewe. Hili nalo kuna uwezekano watu waliamua kumpotosha rais wetu.

Chakusikitisha kwa nchi yangu, Katikati ya mvutano wetu na wabia hadi Rais Magufuli kusitisha mradi, Rais wa Msumbiji Philip Nyusi kwakutumia majasusi wake waliotanda kila pembe ya Afrika na kwingineko, amefanya mageuzi makubwa, amechukua wazo lilelile ambalo limekataliwa Dar es Salaam na wajuvi, amekwenda kulisimika katika Bandari ya Nacala kwakuingia ubia na Wachina kwa Dola bilioni 5 za Kimarekani, hii ni Bandari inayotarajiwa kuwa lango kuu la kiuchumi Afrika.

Wakati hili halijapoa, Mwaka 2017 tu juzi Tanzania tulipowazuia wazungu wasisafirishe madini ghafi na makinikia yao, tuliimba nyimbo kwamba Tanzania itajenga vinu vya kuchenjulia madini hapahapa, na nyimbo ziliimbwa kisiasa zikaitikiwa kishabiki kwa beti za kinafiki kwelikweli. Leo nyimbo haziimbwi, hakuna anayejua kama viwanda vimeshajengwa au laa na hakuna anayehoji hilo kwakuwa ukihojihoji tu basi ukinusurika sana utaenda mochwari au Ubelgiji, tulishazoe vimbunga kwamba vitavuma na kutulia.

Lakini huku sisi tukiwa tumebadili nyimbo sasa tunaimba nyimbo za Standard Gauge nk, Rwanda kwakutumia majasusi wao waliotanda kila pembe ya Dunia, imelichukua wazo lilelile la Tanzania imejenga vinu vya kuchenjulia madini na inatarajiwa kwamba hadi 2024 Rwanda iwe ndio nchi ya kwanza barani Afrika inayosafirisha madini kwa wingi nje ya Afrika. Kumbuka na elewa Rwanda sio mzalishaji wa Dhabu, Almasi wala chochote kiitwacho madini isipokuwa kwenye kilimo cha chai na kahawa huko. Hivyo anategemea viwanda vyake vipokee madini ghafi toka Tanzania, Kongo, Zambia akusanye kodi yake na kugonga muhuri wa madini unaotambulisha kuwa ni madini toka Rwanda nk. Sisi tumelala. Siasa inanguvu bana.

Kwa maoni yangu ninafiki kuna tatizo kubwa kwenye eneo la Ujasusi katika nchi yetu, hasa ujasusi wa Kiuchumi, na hili ndilo lilikuwa msingi wa mimi kuandika Kitabu changu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi. Michakato mingi ya kiuchumi katika nchi hii imekuwa haina mafaa ama inaliacha taifa katika makovu makubwa yasiyozibika. Hii inazaa uhalali wa kuhitaji mageuzi makubwa katika Idara ya Ujasusi nchini kuanzia kwenye ideology, sheria, misingi, kanuni, na mambo anuai ndani ya idara ya ujasusi nchini.

Ujasusi kwa nchi zilizoendelea kama China, Israel, Urusi na Marekani, unafanywa na watu ambao ni smart na wanajengwa kuwa smart ili kuweza kumudu ugumu wa kazi hiyo na kuifanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa. Majasusi katika nchi hizo hawapewi kazi kwasababu ya ujomba ujomba na kujuana.

Ni kweli asilimia kubwa ya information's zenye thamani katika kazi ya ujasusi huwa zinaletwa na "human intelligence" badala ya magazeti, TV na source nyingine za habari.

Kwa maana hiyo basi ni lazima kuwe na watu competent ambao wana uwezo wa kukusanya habari za kijasusi ili tuweze kupata information's za maana na kujenga uwezo wa kuzifanyia kazi informations hizo. Imagine wakati ule wa vita baridi jinsi Directorate 16 ya KGB ilivyoweza kufanya kazi ya kununua sensitive navy information za USA na kuweza kutengeneza balance ya navy fleet bila USA kugundua kwa miaka 17 kupitia kwa Johny Walker junior!

Tanzania kwenye balozi zetu kuna majasusi. Lakini ni majasusi wa aina gani? Wale wa kujua kuongea kifaransa na kireno na lugha nyingine za mataifa ya nje bila upeo wowote wa Technologia? Kama kuna sehemu tunakosea basi ndio hapo. Majasusi wengi wa Tanzania au tunaoambiwa kuwa ni watu wa system wengi katika tafsiri ya kijasusi ni "informers". Ujasusu kama ujasusi hapa Tanzania ni kama hakuna. Usalama wa Taifa au TISS/UWT msingi wao uliounda chombo hiki ni "power defensive", yaani wajibu mkubwa unaelekezwa kwenye kumonitor mwelekeo wa kisiasa Tanzania hasa kuwadhibiti oppositions na elements zote za upinzani na assasinations za elements zozote zinazoonekana kuwa against na himaya ya CCM.

Idara ya Usalama wa Taifa hii tuliyonayo leo ilianzishwa na CCM 1997 kutoka katika muundo wa kijamaa wa chama kimoja, hii ni baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, kwa hiyo bado unaiserve CCM kwanza kisha Taifa linatafsiriwa salama kupitia matokeo ya uimara wa ccm, kama yakifanyika mageuzi ya kimuundo, kisheria, kikanuni na kisera, uimara wa Taifa hautatafsiriwa kupitia uimara wa ccm madarakani, na mambo mengi tunayolalamikia sasa juu ya taifa hayatakuwepo tena. In simple words, taswira kubwa inayoonekana yauhakika ni kazi yao ya kulinda viongozi, kusafiri na viongozi na kuilinda CCM.

Nje ya mambo ya Ujasusi wa Kiuchumi ambao mimi ndio ninaoupigania siku zote uongoze nchi, Naweza kusema Tanzania tuko vizuri katika Ujasusi wa kidola kuliko nchi yoyote pengine Afrika nzima, Hili limefanya kuimeza idara na kuonekana siasa ambazo ndio zinabeba taswira kubwa ya ubora ama udhaifu wa ujasusi Tanzania, Eneo la Ujasusi wa Kidola Tanzania kuna vitengo vya wachapakazi hasa kiko jeshini.., kitengo cha ujasusi ambacho kilikuwa kiko free from politics party ni CMI (central military intelligence). Lakini bahati mbaya muundo na aina ya uongozi wa Magufuli ulikiingiza katika siasa pale kilipofanywa kuwa decision maker wa nchi, lakini upande wa foreign assets ndio wazuri sana wako bize kukusanya taarifa hatarishi dhidi ya nchi...

Kwa undani zaidi Soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.
View attachment 1747076
1. Physibility study za miradi hii zilifanywa lini na ziko wapi?
2. Kwanini wabia wa Bagamoyo Port & SGR wawe TZ na China tu badala ya nchi jirani kama project hizi zina faida kwao?
3. Bila facts and figures khs mambo hayo hizi zitakuwa 'white elephants' kama tazara.
4. Mfano ni bomba la mafuta kati ya TZ na Uganda kuna wabia kadhaa pamoja na wafadhili.
 
Wapiga debe na makafa watiifu wa CCM wakigeuzwa kuwa usalama wa taifa unategemea Nini kitokee
 
Back
Top Bottom