Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
Uzoefu unanifundisha kuwa maumivu mengi tunayokutana nayo hapa Duniani yanatokana na sisi wenyewe kushindwa kuwajibika katika maisha yetu " living active life". Leo tumefikia hatua ya kushindwa kabisa kujitofautisha na matatizo na kufikiri sisi wenyewe ndiyo matatizo jambo ambalo siyo sahihi.
Katika tatizo lolote unalokutana nalo au tunalokutana nalo tunapaswa kuwajibika kikamilifu lakini hatupaswi kuwa tatizo hilo. Katika maisha yako tambua wewe siyo tatizo ila ni kiumbe mwenye wajibu wa kuishi kwa kuwajibika kikamilifu"
Maumivu mengi tunayokutana nayo na kuyaona kama tatizo kwenye maisha yetu yanatokana na mambo makubwa mawili:
(i)kumbukumbu zetu(memory)
(ii)mawazo yeti (imagination.
Siyo jambo la kushangaza kumkuta mtu anaumia sana kiasi cha kujiona hana thamani yoyote leo lakini ni kutokana na kumbukumbu za miaka mingi iliyopita halikadhalika tupo tunaoumia sana leo ila kwa mawazo yetu juu ya siku za usoni.
Mambo hayo mawili yanaumiza maisha ya wengi kiasi cha watu kuvurugikiwa kabisa na kuona kila kitu wakiwemo wenyewe kama tatizo.
Ninafikiri binadamu tunapaswa kuishi maisha hai yanayotufanya kuwajibika kikamilifu "conscious life" na hii ndiyo sifa pekee inayotutofautisha na viumbe wengine kwa kutumia akili tulizojaliwa.
Usiitumie akili yako kinyume chako, hakikisha akili uliyonayo inatumika kwa ajili yako na siyo kwa ajili ya kukuangamiza "brain is a very complex machine". Kumbuka kuwa na akili ni jambo jingine na kuitumia kwa ajili yako ni jambo jingine.
Msaada wako Mkuu haupo nje yako. Wa kukusaidia wewe ni wewe tu msaada wowote unaotoka nje yako hauna nafasi kubwa zaidi ya kuikumbusha akili yako kufanya jukumu lake la msingi la kuwa upande wako na siyo kinyume chako.
Ipo methali isemayo " sikio la kufa halisikii dawa" nikiishadidia kwenye andiko hili ni kwamba akili ya mtu inapokuwa kinyume na mhusika na mhusika asipoamua kuifanya iwe upande wake hata kama akisaidiwa vipi hatopata suluhisho.
Oooh!....kumbe sisi wenyewe ndiyo tunaweza kuwa suluhu bora kabisa katika hali tunazopitia kwa kuhakikisha akili zetu zinakuwa upande wetu kwa sababu zinapokuwa kinyume nasi tunaona kila kitu kikiwa adui kwetu.
Haujawahi kukutana ma mtu anayeamini kuwa kila mtu mfano majirani zake,wafanyakazi wenzake, waajiri wake na ndugu zake ni maadui wake na wanamchukia?...tatizo kubwa hapo siyo hao majirani ila akili ya mhusika inavyomuonesha kuhusu hao majirani.
Natamani nisimalize kuandika kwa maana mawazo yanazidi kuja kwa wingi ila ili nisiwachoshe sana katika kusoma natamani sana kutambua kuwa sisi wanadamu tumepewa funguo moja muhimu sana " akili" tunaweza kuitumia kujifungia katika gereza lolote na pia tunaweza kuitumia kufungua popote tukijua namna ya kuitumia.