Silent Inn Mwenge: Starehe za Dar miaka ya 1990-kwa Freddy Rwegasira!

Silent Inn Mwenge: Starehe za Dar miaka ya 1990-kwa Freddy Rwegasira!

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
17,434
Reaction score
27,177
Nakumbuka enzi zile kila Ijumaa,Faculty Day bonanza,wanavyuo wote wa Dar wanasombwa na mabasi bure wanaletwa New Silent Inn Mwenge.Kiingilio buku,anaanza DJ Fast Eddy kisha kwenye mida ya tano hivi wanapanda Diamond Sound Band "Ikibinda Nkoi".Wakishuka jukwaani Fast Eddy anamalizia show.Nawakumbuka baadhi yao wana Ikibinda Nkoi:

Ellyston Angai - solo guitar - band leader
Elly Chinyama - solo guitar/rythym guitar
Adolph Mbinga - solo guitar
Saido - rythym guitar
Gabby Katanga - Drums
Kessy Kitindi - Drums
Jaji Jumanne "Jojo" - bass guitar
MCD - Tumba
Motoo - Tumba
Andrew Sekidia - Keyboards
Zola Ndonga - Vocals
Balusi Canta - Vocals
Rogers Muzungu - Vocals
Germa Kissa - Vocals
Mackay Fanta - Vocals
Richard Mangustino - Vocals
Alain Mulumba Kashama - rapper
Livason Hassan Sultan - rapper
Anicet Petelo - rapper
Halima Abeid "Mama Lao" - stage show
Diana Aston Villa - stage show
Lilian Internet - stage show
Elly Longomba - stage show
Kamuke Sukari - stage show
Janet Jackson Isinike - stage show
Salum Pongwe - Sound engineer

Huyu Rwegasira alikuwa na Silent in na diamond sound then Feliacian Muta yeye alikuwa na FM recording studio akianzia MWANZA then kinondoni Studio. FM studio 55. ndiye boss wa Saida Kaloli

Nakumbuka watoto wa kike wengi walipata mimba
 
Ehe hapo mzee rwegasira kilikuja kukumkuta nini badaye

Ova
Aliokoka, akawa anaswali kwa mChungaji Rwakatare pale mikocheni B na baadae akarudi nyuma baadae akaacha wokovu na shetani akapita naye na sasa amerudi wak Yesu.

Ukumbi ulivunjwa na jeshi baada ya migogoro usisuluhishika kwa vile huyo muhaya jengo lilikuwa lake,ardhi ya mchaga Mmoja anaitwa shirima,naomba niishike hapo kwa sababu rwegasira amekimbilia kwa yesu
 
enzi hizo nauli ya daladala ni sh 150,
band za mnanda kama vile jaguar au wanyamwezi family, wakipiga show hapo. wateja wao wengi kama co wote ni wale masela nunda, mtoto wa mama hizo show hauziwezi

bange, gongo na unga ndo mahala pake, asubuhi kunapopambazuka, wanapofanya usafi, ni mwendo wa vipisi vya bange, sigara, chupa za gongo na vinaylon vya unga.

halafu nenda kaulize kaunta, jana mmeuza kreti ngapi? hapo ndipo utakapochoka
 
😂😂😂
 
Aliokoka, akawa anaswali kwa mChungaji Rwakatare pale mikocheni B na baadae akarudi nyuma baadae akaacha wokovu na shetani akapita naye na sasa amerudi wak Yesu.

Ukumbi ulivunjwa na jeshi baada ya migogoro usisuluhishika kwa vile huyo muhaya jengo lilikuwa lake,ardhi ya mchaga Mmoja anaitwa shirima,naomba niishike hapo kwa sababu rwegasira amekimbilia kwa yesu
Ardhi Ilikuwa nafikiri sio ya Shirima Bali Mzee Mmoja anaitwa Makoi kama kumbukumbu zangu ziko sawa.Hapo Kwa sasa Tunaendelea Kubamba na Dance Club Hapo Mwenge Sam Nujoma..
 
Hapo wengine tulikuwa tunasoma kwenye magazeti kuhusu hiyo Silent Inn. Kiukweli bila kuja chuo, ingechukua miaka mingi sana kufika Dar. Mwisho wangu ilikuwa Chalinze wakati naenda shule Mkwawa Iringa.. nilikuwa naishia kuona kibao cha DAR ES SALAAM wakati basi la Hood from Arusha likikata kona.
 
Ardhi Ilikuwa nafikiri sio ya Shirima Bali Mzee Mmoja anaitwa Makoi kama kumbukumbu zangu ziko sawa.Hapo Kwa sasa Tunaendelea Kubamba na Dance Club Hapo Mwenge Sam Nujoma..
Makoi huyu wa Mwika Hotel ya Sinza na kumbi za best choice? Huyu Makoi mchaga tajiri hashughuliki na vitu vidogo na hanaga kashfa, katulia kariakoo anapandisha tu maghorofa.
 
Dah.! Umenikunbusha mbali. Silent in ilikuwepo pale ilipo dance club kwa sasa. Ndio mitaa iliyonilea hiyo. Enzi darasa la kwanza. Giza likiingia madogo janja tu ndio tulikua tunafika maeneo hayo.

Palibomolewa pale. Mitaa ile baadae ikaja kuibuka meeda pale ambapo sasa hivi ipo kitambaa cheupe
 
Nakumbuka enzi zile kila Ijumaa,Faculty Day bonanza,wanavyuo wote wa Dar wanasombwa na mabasi bure wanaletwa New Silent Inn Mwenge.Kiingilio buku,anaanza DJ Fast Eddy kisha kwenye mida ya tano hivi wanapanda Diamond Sound Band "Ikibinda Nkoi".Wakishuka jukwaani Fast Eddy anamalizia show.Nawakumbuka baadhi yao wana Ikibinda Nkoi:

Ellyston Angai - solo guitar - band leader
Elly Chinyama - solo guitar/rythym guitar
Adolph Mbinga - solo guitar
Saido - rythym guitar
Gabby Katanga - Drums
Kessy Kitindi - Drums
Jaji Jumanne "Jojo" - bass guitar
MCD - Tumba
Motoo - Tumba
Andrew Sekidia - Keyboards
Zola Ndonga - Vocals
Balusi Canta - Vocals
Rogers Muzungu - Vocals
Germa Kissa - Vocals
Mackay Fanta - Vocals
Richard Mangustino - Vocals
Alain Mulumba Kashama - rapper
Livason Hassan Sultan - rapper
Anicet Petelo - rapper
Halima Abeid "Mama Lao" - stage show
Diana Aston Villa - stage show
Lilian Internet - stage show
Elly Longomba - stage show
Kamuke Sukari - stage show
Janet Jackson Isinike - stage show
Salum Pongwe - Sound engineer

Huyu Rwegasira alikuwa na Silent in na diamond sound then Feliacian Muta yeye alikuwa na FM recording studio akianzia MWANZA then kinondoni Studio. FM studio 55. ndiye boss wa Saida Kaloli

Nakumbuka watoto wa kike wengi walipata mimba

Keyboard Andrew Sekidea...Huyu Mwamba alihamiaga Twanga Pepeta ....sijui bado yupo au ameshakufa???

Hao wanenguaji wote wameshafukiwa chini ya mchanga
 
Back
Top Bottom