SoC04 Silikoni Bongo Mkombozi wa Bunifu Tanzania, ili kuchochewa ongezeko la ajira katika nchi yetu

SoC04 Silikoni Bongo Mkombozi wa Bunifu Tanzania, ili kuchochewa ongezeko la ajira katika nchi yetu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Mabula marko

Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
44
Reaction score
38
SILIKONI BONGO MKOMBOZI WA BUNIFU TANZANIA, ILI KUCHOCHEA ONGEZEKO LA AJIRA KATIKA NCHI YETU
th.jpg



Utangulizi

Ukitazama picha hapo juu wazo la uumbaji wa ulimwengu kama ambavyo maandiko matakatifu hutueleza linakuijia kichwani, lakini vile vile ukiendelea kuangalia vizuri utaona nembo za bunifu kadhaa ambazo zimeleta mapinduzi makubwa katika Nyanja mbalimbali hasa mawasiliano , biashara , kilimo na zinginezo hapa duniani.

Ukifuatilia vizuri utaona kwamba bunifu hizi na zingine zinazoendelea kuibadilisha na kuishangaza dunia zimezaliwa katika maeneo ambayo kwa lugha ya picha ni mithiri ya mbingu ambazo zimeweka mazingira wezeshi ya kuzaa bunifu hizi katika ukubwa wake na kutengeza ajira za watu milioni nyingi sana katika mataifa yao na duniani kote

Lugha ya picha ya mbingu katika andiko hili ni vituo vya kitaifa na kimkakati vya kuibua na kulea bunifu kwa kuwakusanya wabunifu katika mataifa yao bila kujali ngazi yao ya elimu, ukitazama mataifa yaliyo endelea kama marekani ,Israel na mengine huko ulaya , kenya , Nigeria na mengine hapa Africa yaweka mbingu hizi kwa ajiri ya kuzalisha bunifu na kuzilea ikiwa ni mkakati wa punguza wimbi la vijana na watu wasio kuwa na ajira kwa kuwawezesha kujiajiri kupitia bunifu zao na kuajiri wengine pia.

Silkoni Valley nchi marekani ni moja ya maeneo ya kimkakati katika nchi hiyo ambayo ni mbingu ya uumbaji wa bunifu kubwa Zaidi dunia zilizotengezwa mabilionea na matrionea wakubwa na makampuni makubwa kama Meta, Tesla,Netflix,Amazon ,Google,Twitter ,Microsoft , Apple na nyinginezo nyingi na ukitazama vizuri utagundua kwa asilimia kubwa ya matajiri walio katika kumi bora ya matajiri duniani ni sehemu ya wamiliki wa kampuni hizi, nchini Israeli wana eneo lao pia liitwalo silkoni world na nchi zingine zinamaeneo yao kadhalika

Katika nchi yetu eneo la ubunifu bado linapewa kisogo licha ya wadau mbali mbali wa maendeleo kujaribu kuwasaidia wabunifu hawa kwa kuwakutanisha na wawekezaji lakini asilimia kubwa watu wameshindwa kuzifikia ndoto zao kwa kukosa sehemu sahihi ya kuendeleza bunifu zao kwa kupatiwa mahitaji yote wayatakayo katika kufanikisha mchakato, kuna wengine wamezulumiwa au kukatishwa tamaa na kushindwa kuziendeleza na kubaki wakiwa tegemezi wa ajira badala ya kujiajri kupitia bunifu zao na kutengeneza ajira kwa wengine.

Silikoni bongo ni jina la kibunifu ambalo linalenge kuwepo kwa kituo maalumu cha kitaifa cha kimkakati cha kulea na kukuza bunifu za vijana wabunifu ili kuwafanya wajiajiri kupitia bunifu zao na kutengeneza ajira katika bunifu hizo kwa wengine uwepo wa kituo hicho hautaangalia ngazi ya elimu , tuachane na mizania ya SIDO , COSTECH na taasisi binafsi zinazo wezesha wabunifu badala yake kuwe na kituo maalum cha bunifu ambacho kitatangazwa na kuvutia wawekezaji kufika na kuwekaeza katika mawazo haya bunifu ili yaendelezwe na kutengeza ajira kwa vijana wa kitanzania. Eneo hili linatakiwa lijengwe katika kwenye mawazo ya uvumbuzi, ujasiriamali, na uwekezaji wa kiufundi na sera wezeshi ili kuibua bunifu na kuziendeleza na kusaidia kukuza sekta binafisi ili kuongeza ajira

Mfano mzuri wa eneo la kuigwa ni hili la silikon valley kama unavyoona kampuni nyingi kubwa zimeuniwa hapa picha na mtandao.
R (2).jpg

Muonekano wa silikon valley kwa nje picha na mtandao
download.jpg

Umuhimu wa kujenga Silikon bongo hapa Tanzania

  • Kuongezeka kwa Ukuaji wa Uchumi: Sekta ya ubunifu na biashara changa inaweza kuwa injini ya ukuaji wa uchumi. Kuanzisha kituo cha uvumbuzi kunaweza kusaidia kukuza sekta ya TEHAMA na teknolojia nyinginezo, hivyo kuongeza uzalishaji na kutoa fursa za ajira.
  • Kuchochea Ubunifu na Uvumbuzi: Mazingira ya uwepo wa eneo zuri la ubunifu yanaongeza ubunifu na uvumbuzi. Kwa kuvutia akili na talanta, na kutoa rasilimali za kutosha kwa wajasiriamali na wabunifu, kunaweza kusababisha maendeleo ya suluhisho mpya na ubunifu wa kiteknolojia.
  • Kuongezeka kwa Ajira na Talanta: Sekta ya teknolojia inahitaji talanta yenye ujuzi. Kuanzisha "Silikoni bongo" kunaweza kusaidia kutoa fursa za ajira kwa vijana wenye ujuzi wa TEHAMA, sayansi ya kompyuta na zinginezo huku pia ikazalisha wataalamu na watafiti wenye ujuzi.
  • Kuvutia Uwekezaji wa Ndani na Nje: Mafanikio ya kituo cha uvumbuzi yanaweza kuvutia uwekezaji wa ndani na nje. Hii inaweza kuongeza mtiririko wa mitaji na kusaidia kukua kwa makampuni ya ndani.
  • Kuboresha Miundombinu ya Teknolojia: Uwekezaji katika miundombinu ya TEHAMA unaweza kuboresha upatikanaji wa intaneti na teknolojia kwa ujumla, ambayo inaweza kuleta manufaa kwa makundi mbalimbali ya watu na sekta nyingine za kiuchumi.
  • Kukuza Uwezo wa Kitaifa: Kuanzisha kituo cha uvumbuzi kunaweza kukuza uwezo wa kiteknolojia wa taifa na kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya watu kupitia teknolojia, kama vile afya, elimu, na huduma za umma.
  • Kuongeza Mchango wa Teknolojia katika Maendeleo ya Jamii: Teknolojia inaweza kusaidia kuboresha huduma za umma na kuwezesha maendeleo ya kijamii. Kwa mfano, teknolojia inaweza kutumiwa kuboresha huduma za afya, elimu, na kilimo.
Hitimisho

Ikiwa bunifu zimekuwa sehemu ya suluhisho la ukosefu wa ajira katika sehemu nyingi duniania,jitihada za kuanzisha kituo cha uvumbuzi na teknolojia zinaweza kuwa na manufaa makubwa kwa maendeleo ya taifa na kuboresha maisha ya wananchi wote. Ni muhimu kwa viongozi wa serikali, wawekezaji, na jamii kwa ujumla kuweka nguvu pamoja kuleta mabadiliko haya chanya
 
Upvote 4
Silkoni Valley nchi marekani ni moja ya maeneo ya kimkakati katika nchi hiyo ambayo ni mbingu ya uumbaji wa bunifu kubwa Zaidi dunia zilizotengezwa mabilionea na matrionea wakubwa na makampuni makubwa kama Meta, Tesla,Netflix,Amazon ,Google,Twitter ,Microsoft , Apple na nyinginezo nyingi na ukitazama vizuri utagundua kwa asilimia kubwa ya matajiri walio katika kumi bora ya matajiri duniani ni sehemu ya wamiliki wa kampuni hizi, nchini Israeli wana eneo lao pia liitwalo silkoni world na nchi zingine zinamaeneo yao kadhalika
Kizuri, wengi wanakiiga.

Ikiwa bunifu zimekuwa sehemu ya suluhisho la ukosefu wa ajira katika sehemu nyingi duniania,jitihada za kuanzisha kituo cha uvumbuzi na teknolojia zinaweza kuwa na manufaa makubwa kwa maendeleo ya taifa na kuboresha maisha ya wananchi wote. Ni muhimu kwa viongozi wa serikali, wawekezaji, na jamii kwa ujumla kuweka nguvu pamoja kuleta mabadiliko haya chanya
Tunakubali, ubunifu ni muhimu kwa maendeleo ya kweli. Tujitahidi kupunguza ku'export' ajira zetu nje.

Kwa kiwa na wabunifu wetu badala ya wachuuzi tu
 
Back
Top Bottom