Simama upande wa Lulu

Simama upande wa Lulu

Kama nimekusoma sawasawa, umedai umeona udaku kwamba alikutwa na hirizi na mpenzi wake!!! Kama ndivyo, huyo hawezi kuwa mpenzi wa kiume hata kama ana viungo vya kiume! Sifa kuu ya mwanaume ni kifua hususani linapokuja jambo la aibu kwa mwenza wake!! Sasa yeye kaona hirizi tu inapumua; dunia mzima inafahamu!!! Mwanaume angepiga chini kimya kimya na hiyo ikabaki siri yake....
 
Mshana jr umeingia lini huku, kuwajengea hoja wasanii au wanamuziki kwenye mitandao kuna maana na matokeo tofauti tofauti. Ata hivi jinsi watu wanavyojibu hoja inathibitisha unavyoheshimika.
 
Kutoweka vitu wazi'mitandao ya kijamii inaweza ikamsaidia asisemwesemwe.ni wazo tu.
Mbona vitu anavyoweka mitandao ni vya kawaida sana!! Au ku-post picha akiwa na bwana ake... jambo ambalo kwa dunia ya leo hata asipofanya yeye; watu wata-post tu unless asiwe anakuwa nae pamoja kabisa!!!
 
Mkuu weka hata kapicha kake, hata zikiwa mbili tatu hatutojutia mbs... post nzuri kama hio isindikizwe na picha
 
Mshana jr umeingia lini huku, kuwajengea hoja wasanii au wanamuziki kwenye mitandao kuna maana na matokeo tofauti tofauti. Ata hivi jinsi watu wanavyojibu hoja inathibitisha unavyoheshimika.
[emoji120] [emoji120] [emoji817] [emoji817] [emoji115]

Sent from my INFINIX-X551 using JamiiForums mobile app
 
Kama nimekusoma sawasawa, umedai umeona udaku kwamba alikutwa na hirizi na mpenzi wake!!! Kama ndivyo, huyo hawezi kuwa mpenzi wa kiume hata kama ana viungo vya kiume! Sifa kuu ya mwanaume ni kifua hususani linapokuja jambo la aibu kwa mwenza wake!! Sasa yeye kaona hirizi tu inapumua; dunia mzima inafahamu!!! Mwanaume angepiga chini kimya kimya na hiyo ikabaki siri yake....
Yeah sure thanks nimekupata vizuri sana

Sent from my INFINIX-X551 using JamiiForums mobile app
 
Kama binadamu na Kama mzazi ukiacha mapungufu yote ya Lulu. Elizabeth Michael naye ni binadamu mwenye hisia kama wengine! Anastahili kupata kila unachostahili wewe, upendo ulinzi kujaliwa utu wake kusifiwa privacy nk nk
Kuna watu wana kipawa cha kuwa maarufu kiasili Lulu ni mmojawapo na tatizo limeanzia hapo

Ni binti ambaye nyota yake iliwaka akiwa mdogo kabisa, umaarufu wake kuna watu wameusotea miaka bila kuupata..hili ni tatizo la pili

Nyota yake hiyo ikaenda sambamba na matatizo, katika Umri mdogo kabisa akapata mpenzi ambaye mamilioni ya wanawake wangetamani kumpata na ikibidi kummiliki milele..hili ni tatizo la tatu na msingi wa mada

Hulka yake binadamu ni kufurahia ama kuona mwingine anashindwa hasa yule anayedhani kamzidi hiki ama kile...ishu za haters huanzia hapa

Tangu wakati huo Lulu hajawahi kupumua ikawa ni bandika bandua ya matatizo, sehemu kubwa ya jamii ikajitenga naye bila kutafakari kwamba nje ya ustaa na umaarufu wake Lulu ni binti kama binti mwingine yoyote anayepitia hatua za kawaida kabisa za makuzi na anakumbana na mengi....

Mabinti wengi huchukua maamuzi mabaya ya kujiua kwenye changamoto ndogo tu za ukuaji. Jamii ikamtenga fulani hivi wachache wakampa moyo wa kusonga mbele anaweza kusimama na kuendelea mbele NAMSIFU

matatizo yamemkomaza yuko imara kuliko maelfu ya watu, lakini ni nani anayependa kuambiwa kuwa ana nuksi? Ama kimavi? Ni nani anayependa kuitwa kuwa yeye ni malaika wa kifo? Hakuna!!!!

Lulu katika binadamu wake anapenda maisha yake amani furaha na upendo... Lakini kagundua kuna tatizo mahali... Kaenda kusaka tiba mbadala, limekuwa ni tatizo kubwa!

Ni nani ambaye hapendi kujaribu njia nyingine kama akiona mambo hayaendi? Tuacheni unafique kiwango cha PhD
jamani "HIMEKUWAJE" TENA?
 
Tukiacha yooote yasemwayo kuhusiana na yeye ila Lulu ni mdada anayejua thamani yake ukiachilia mimama mizima iliyojazana Bongo movie.Kapitia katika matatizo ambayo kiukweli ni ngumu sana kuendana nayo ila mtoto wa watu kasimama imara anaendeleza maisha yake.Anastahili pongezi pia inaonesha mama yake pia ni msaada mkubwa kwake na anaweza kumrudisha kwenye mstari.Maana wasanii wengine wanashindana tu na mama zao na wao kutupia picha instagram na kutoa matamko.
 
Back
Top Bottom