Simba 1-0 Prisons | Ligi kuu bara | Benjamin Mkapa

Simba 1-0 Prisons | Ligi kuu bara | Benjamin Mkapa

Kwa mtazamo wangu naona shida ya Simba inaanzia kwa namba 6, hatuna namba 6 wa kukaba anyan'ganye mipira na kuitoa kwa wakati, yule 6 wa kuwalinda mabeki wa kati na mwenye spidi ya kuanzisha mashambulizi, hapa ndipo tunapoharibu.

Kama angepatikana huyo angemuweka Chama active zaidi, Chama angepata mipira mingi kwa wakati hivyo angetengeneza nafasi nyingi za kufunga kwa washambuliaji wetu.
 
Hapa benchi la ufundi la Simba lijitafakari upya, yaani dakika ya 33 hakuna shoot on target wala off target huku unacheza na timu ya mwisho kwenye msimamo wa ligi. Hapa kazi tunayo
Muda bado sana usikate tamaa
 
Kumbe wale madogo wa Dar city tuliwaonea kwa sababu ndio ilikuwa mara yao ya kwanza kucheza mechi usiku, paka daki ya 21 tulikuwa tunaongoza goli 4-0.
Leo tumekutana na timu level yetu ndio maana tunambwelambwela tu.
 
Jamani jamani niliswma hizi counter attacks ndo weakness ya simba

98% ya mechi tulizofungwa zote tumepigwa kwa style hii, simba ina dominate mpira lakini mashambulizi ya hatari yanakuwa yanatuandama sisi
Huu ndio ukweli na kama tukifungwa basi tutafungwa goli la aina hiyo hiyo Muangalie huyu Mbangula na Muhilu ni hatari sana hawa watu
 
tumekoswa tena, jamani hii mipira tunayocheza ni ya wapi?
 
Onaa hii daah Heko Kwa Inonga Baka
 
Huu mfumo wa kucheza pasi fupifupi tu zisizo na maana hakika ni mwendawazimu tu atakayesifia uhuni huu wa kocha na benchi la ufundi, yaani dakika karibu ya 40 hakuna on target wala off target hata moja kwa Simba. Hii timu itatuua mwaka huu. Mashambulizi yote ya hatari tunashambuliwa sisi tu
 
Huu ndio ukweli na kama tukifungwa basi tutafungwa goli la aina hiyo hiyo Muangalie huyu Mbangula na Muhilu ni hatari sana hawa watu
Na sio kulinda tu, madogo hata kwenye kunyang'anya mipira wamekuwa imara maradufu kuliko simba, angalia shambulizi walilofanya muda huu bila dogo kupaisha ingekuwaje?
 
Simba inapata kona dakika ya 40
 
Back
Top Bottom