Simba anzeni kupiga jalamba

Simba anzeni kupiga jalamba

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Penye moshi kuna moto, muda sio mwingi Mh. MO atakaa pembeni maana inaonekana anatoa pesa yake kishingo upande. Kuna siku alisemega kuwa 20 bil zake zinaweza kununua bank, na sasa anasema 4bil zake zinatumika kulipa mishahara ya Simba bila sababu.

Mh. MO anataka Simba ishinde mechi zoooooote (100%) inapocheza na timu zote kwenye mashindano yote. Na hilo ndio lililomfanya Aussems afukuzwe pia.

Simba tujiandae kutafuta namna bora ya uwekezaji.
 
vyura fc walikuwa na Manji - sasa hivi chali!

mbumbumbu fc wana Mo - nao chali punde!
 
Mimi sijatoa hata sumuni 5 kwa Simba lakini naumia sana Simba inapofungwa, kiasi Kwamba ningekuwa karibu na wachezaji wa Simba ningeshaua walau mmoja, hali hiyo inakuwaje kwa MO?
 
Penye moshi kuna moto, muda sio mwingi Mh. MO atakaa pembeni maana inaonekana anatoa pesa yake kishingo upande. Kuna siku alisemega kuwa 20 bil zake zinaweza kununua bank, na sasa anasema 4bil zake zinatumika kulipa mishahara ya Simba bila sababu.

Mh. MO anataka Simba ishinde mechi zoooooote (100%) inapocheza na timu zote kwenye mashindano yote. Na hilo ndio lililomfanya Aussems afukuzwe pia.

Simba tujiandae kutafuta namna bora ya uwekezaji.
mikia FC.
 
Mimi sijatoa hata sumuni 5 kwa Simba lakini naumia sana Simba inapofungwa, kiasi Kwamba ningekuwa karibu na wachezaji wa Simba ningeshaua walau mmoja, hali hiyo inakuwaje kwa MO?
Sisemi namuunga mkono Mzee Kilomoni, lakini nataka-sitaki hii ya Mo inaonesha kasoro kubwa ya mfumo uliopo wa uendeshaji Klabu ya Simba. Hivi baina ya Simba na Manchester United, ipi imedumu zaidi na matokeo mabovu? Ipi imetumia fedha nyingi zaidi ndani ya misimu mitatu iliyopita?

Lakini Kwa nini hatumsikii ‘tajiri’ wa Manchester United akisikitikia pesa yake?. Kwa sababu yeye amenunua biashara inayojiendesha. Akiona mambo hayajipi, anauza hisa zake na kusepa.

‘Tajiri’ wa SImba hajanunua biashara, amewekeza kwenye inayoweza kuwa biashara. Na kwa hivyo lazima aumizwe pale uwezekano wa alichokiwekeza kuwa ni biashara unaposuasua ilhali hana wa kumuuzia his naye akasepa zake.

Mfumo sahihi wa kuendesha biashara ya namna hiyo ni ama kuwa na wanahisa halisi (sio wanaobadilishwa kutoka kuwa wanachama) au kuiwacha timu ikawa ya wanachama moja kwa moja. Hili la kwanza ndilo ambalo Mo angependa liwe na huenda uwekezaji wake wa sasa ni mkakati wa kulifanya hilo litokee. Hili la pili ndilo analopigania Mzee Kilomoni.

Nina wasiwasi Mo anaweza kuiwacha timu mwaka wowote atapobaini mikakati yake haikufanikiwa. Na hapo itakuwa ni njia panda kwa klabu, kwa sababu hata huo mfumo anaoupigania Mzee Kilomoni utakuwa mgumu kuurejea tena.
 
Mo amekumbushwa kuwa kama anataka ajiweke pembeni ni vyema aandike barua rasmi na sio kwenye twitter kama alivyofanya na kuleta taharuki.

Msimamo wa Mo bado ni kukaa pembeni ila kwasasa anaanda taratibu rasmi ila ndo basi tena.

Simba andaeni bakuli sisi tumeshalizoeya hatuoni soni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinachomuuma Mo sio hela za mishahara tuu bali hela anazowapa wakina Manara ili timu ikaloge na kuhonga marefa hazileti ushindi 100%,hilo ndio tatizo kuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simba tatizo Kwanza ni makocha, hawajuia mchezaji yupi anafaa kucheza wakati gani.
Pili wachezaji wenyewe hawajui nini wamekifuata uwanjani, muda mwingi wanatumia kuzulula na mpira uwanjani.
Wanacheza kwa tabasamu na hawana hasira ya kufunga magoli.
Hata kupiga faulo kunawashinda, utafikiri hawafanyii mazoezi.
Kiufupi wachezaji ni wazuri Ila wanacheza na jukwaa badala ya kuusaka ushindi kwa hasira dakika za mwanzo.
Ili ucheze mpira vizuri ni lazima ukasirike na kupigana kwa nguvu zako zote. Ukichoka jiangushe utolewa nje.
Wachezaji wanapumzika uwanjani na kutembea kwa madaha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo lipo kwa makocha na wachezaji. Hata mimi ningekuwa MO ningelala zangu mbele niachane na hii timu ambayo wachezaji hawajielewi na sasa makocha pia hawajielewi.

Hivi Matola na huyo mzungu kwenye mechi ya fainali walishindwa vipi kupanga kikosi "konk" cha watu 11 ndani ya kundi la wachezaji mahiri zaidi ya 25? Badala yake wanataka kumridhisha kila mchezaji acheze tu bila kuangalia ugumu wa mechi. Hata kwenye chandimu huwa wanapanga mchezaji kulingana na ugumu wa mechi. Na huo mfumo wao wa kuendelea kumtumia mshambuliaji mmoja asili mbele badala ya wawili watendelea kupata tabu sana.

Wachezaji wa Simba tangu wamefika robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika msimu uliopita wamekuwa na vichwa vikubwa. Wanajiona wao ndio wao na hapa Tanzania wanaona kabisa hakuna timu inayoweza kuwafunga. Wanajiona kabisa hawastahili kucheza na timu za hapa bongo na yule msemaji wao anazidi kuwaharibu kwa kuwapa sifa kuwa wao ni "level" za Mazembe, Al haly n.k.

Wachezaji wa Simba wakishaifunga timu kibonde goli moja au mbili utaona wanaanza madoido wanashindana kupiga visigino, kanzu, tobo ili washangiliwe na jukwaa badala ya kuendela kutafuta magoli yafike hata 10 kwa bila. Matokeo yake dharau zao zimekuwa kama tabia ndio maana wakikutana na chuma kama Mtibwa wanachanganyikiwa kwa sababu wenzao wapo serious wanatafuta magoli wao wanabaki wanashangaa mbona jamaa wanakaza hivi. Mara utasikia kila timu inatupania na nyie si muwapanie tuone nani anaweza?.

Mwambieni MO amebadilisha uamuzi wake mapema sana. Angekaa pembeni walau kwa miezi miwili halafu ndio arudi ili wachezaji na makocha wajue ubaya wa njaa na hapo wangepata la kujifunza.
 
Mimi sijatoa hata sumuni 5 kwa Simba lakini naumia sana Simba inapofungwa, kiasi Kwamba ningekuwa karibu na wachezaji wa Simba ningeshaua walau mmoja, hali hiyo inakuwaje kwa MO?
Kama hamtaki kufungwa jitengenezeeni kombe lenu msishiriki kwenye mashindano. Mawazo kama hayo ni chanzo cha kununua mechi.
 
Back
Top Bottom