Simba, Azam ndoa ya kijakazi

Simba, Azam ndoa ya kijakazi

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
5,986
Ni sawa tukisema kwamba ndoa ya kijakazi hatihati.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ametoa kali baada ya kusema amesusia kununua vitu vinavyotengenezwa na kampuni ya Azam FC.

Hans Poppe amesema hatakuwa akinywa maji ya Azam wala kula keki za Azam kwa madai wamewafanyia ‘uhuni".

Hans Poppe ameyasema hayo leo wakati akihojiwa la E FM Radio kwa madai Azam FC wamefanya hila kuhakikisha wanampata kiungo Ramadhani Singano ‘Messi' kwa hila.

"Wamemsajili Messi kwa ujanja, wameshinikiza hili suala ili wampate kijanja. Nasema mimi sasa sitakula keki zao wala kunywa maji yao.
"Ndiyo, nafanya hivyo ili kupunguza nguvu. Maana kama tunanunua vitu vyao tunawapa nguvu halafu wanatudhulumu," alisema.

Messi ametua Azam FC baada ya kamati ya maadili na hadhi za wachezaji ya TFF kuvunja mkataba wake.


Simba wamekuwa wakilaumu uvunjwaji huo wa mkataba unaonyesha kuwa wa mipango.
 
Anhaa kumbe keki, nilidhani 'kesi zao'.
Apotezee tu kama vp!!
 
Mikia povu linawatoka!washasahau km okwi walimpata kwa njia km hii azam waliyompata singano!
 
Hawa simba kweli ni kigenge cha wahuni! Yani kila siku wao tu hawajifunzi!
 
Walivyowapata Abdi Banda na Emmanuel Okwi ndivyo Azam ilivyompata Ramadhan Singano. Ama kweli mkuki ni kwa nguruwe tu, kwa binadamu mchungu!
 
so walitaka singano awe kijiweni, asisajiliwe na timu yeyote??
 
viongozi wa Simba hawajui ukubwa wa timu yao wako pale kufanya biashara zao kama wako makini timu kama Azam au Tff hawawezi kuwasumbua badala wamekuwa wakilalamika tu wanashindwa hata na viongozi wa kimondo ambao walisimama kidete kudai haki zao kama wangekuwa makini wangekataa mkataba wa kuonyesha tv ambao ni wa kinyonyaji matokeo yake azam wanapata pesa nyingi kupitia mgongo wao pesa ambazo wanatumia kuwahujumu
 
Maskini Simba Timu Yangu Kwa Aina Hii Ya Viongozi, Sasa Najua Kwa Nini Timu Yetu Haifanyi Vizuri.
 
Timu ina Rais katuni tu. Maamuzi yanafanywa na Hans Pope.
Tatizo liko hapo. Mtamkumbuka Wambura pamoja na utapeli wake.
Issue za wachezaji siku zote lazima wapigwe bao.
 
Back
Top Bottom