Kwanza poleni lunyasi. Pamoja na kupokea kichapo toka kwa J.S. Saoura bado mna nafasi kubwa ya kufuzu na kuingia robo fainali. Katika kundi lenu mnapishana kidogo sana. Mfano timu ya kwanza ina pointi nane, zinazofuata mbili zina pointi saba kila moja na Simba ina pointi sita. Mkijipanga vizuri dhidi ya AS Vita mtatoboa. Kazeni buti.