Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,896
- 4,058
Inaelekea viongozi wa Yanga hawaelewi wafanye nn kwa sasa ili Yanga irudie makali yake kwani wanatapatapa. Nmeshangaa kuona wanaajiri wasemaji 2 wa klabu ili wapambane na Haji Manara mmoja. Inatia aibu sn. Kwa mtazamo wangu kupoteza mvuto kwa Yanga kumesababishwa na timu kupoteza mvuto ndani ya uwanja. Nilitegemea viongozi uje na mkakati wa kuboresha timu ndani ya uwanja badala hz sarakasi za nje ya uwanja ambazo hazisadii timu kwa chochote zaidi ya kufunika ubovu wa timu uliokithiri karibu kila idara ambao hata mtu asiejua mpira anaweza kuubaini. Viongozi wa Yanga wanapaswa kutambua kuwa Simba bora ndio inayomfanya Haji Manara kuwa msemaji bora. Mkitaka kushindana na Haji Manara tengenezeni timu bora sio hii inayobutua butua mpira. La hivyo mtaendelea kunyanyashwa na kuteseka sn na Manara. Mpaka sasa sielewi kwanini mliwaacha wachezaji km Matheo Antoni,Maka Edward na Haji Mwinyi.