Simba Day v/s Wananchi Day, Compare and Contrast

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,775
Reaction score
29,746
Wakuu Kwema?

Hapo Kabla kwa mara ya kwanza, timu ya Yanga ilifanya tamasha lake la kutambulisha wachezaji wake wapya iliyowasajili msimu huu, pamoja na wanaoendelea. Tamasha hili lilikwenda kwa jina la Wananchi Day.

Kwa upande wa watani wao wa jadi, Wekundu wa Msimbazi, Simba S. C nao walifanya tamasha lao kama kawaida yao hapo jana ili kutambulisha kikosi chao nao, wapya na wanaoendelea.

Sasa basi ningependa tujadili juu ya matamasha haya mawili, utani wa jadi hauko kwenye pitch tu, hata matukio kama haya tunashindana pia kujua nani kafanikiwa zaidi ya mwengine. Nitaanza kulinganisha kama ifuatavyo,

KUJAZA UWANJA
Ni Wazi kwa matamasha yote mawili uwanja ulijaa. So kila timu imefanikiwa kwa hilo. Ila Simba inafanikiwa zaidi sababu imeweza kujaza Uwanja siku Kazi (Jumanne) wakati Yanga ilijaza Uwanja siku ya Mapumziko.

Inawezekana kabisa Simba wangefanya tamasha lao siku ya Mapumziko basi Uwanja "Ungetapika" zaidi ya Jana. Au Yanga wakafanya tamasha lao siku ya kazi basi wangeshuhudiwa na Mashabiki Wachache + Viti Vitupu!!

VIKOSI
Simba inaonekana kua na kikosi bora kuliko Yanga, sababu kwa hesabu za kawaida tu Simba imeshinda kwa tofauti ya Magoli mawili wakati Yanga imesuluhu.

Pia ikumbukwe kua Zambia wako juu kisoka kuliko Kenya, hivyo inawezekana kabisa Simba imecheza na timu bora zaidi kuliko Yanga.

Kwa muono wangu huu, juu ya haya machache basi Simba imefanikiwa zaidi kuliko Yanga. Karibuni kwenye mjadala...!!!
 
Maendeleo hayana timu[emoji3][emoji3]
Your browser is not able to display this video.
 
Mikia inabidi mkafanye mtihani wa IQ ...unasema Zambia iko juu kisoka kuliko Kenya ?mbona Zambia hawakuwepo AFCON 2019....Zambia kizazi Cha dhahabu kimeshapotea..Kariobang sharks waliwavimbia Everton hao Power Daynamos wangeweza kwa jinsi wanavyocheza?kujaza uwanja kwani huko nyuma hamkuwahi kufanya tamasha weekend?Sifia Yanga wamefanya kazi nzuri..mara ya kwanza hamasa ilikuwa juu..itakuwaje mwakani?mwisho Manara ana kesi mahakamani amefanya Nini???
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
HUJUI UNACHOANDIKA
 
KMC ni zaidi ya Everton
 
Unazi unakusumbua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…