Simba fanyeni maboresho ya kikosi vinginevyo tarehe 08 Machi 2025 tunakwenda kumpa ubingwa Tena Yanga

Simba fanyeni maboresho ya kikosi vinginevyo tarehe 08 Machi 2025 tunakwenda kumpa ubingwa Tena Yanga

Joined
Nov 27, 2024
Posts
43
Reaction score
127
Jana kwa namna nilivyouangalia mpira, timu yetu katikati ilikuwa inakatika sana, kama wangekuwepo wale sungura huku Pacome, kule Max, kule Aziz, cjui Mzize au Dube Leo wengine tusingeamka majumbani kwetu na tungebakia mavyumbani kusikiliza nyimbo za Amapiano TU, kiukweli Azam walitukosa sana Jana, beki zilikuwa zinakatika mno, Ngoma alikuwa ameshuka chini akisaidiana na Kagoma huku viungo wa Azam akina Akaminko, Yahya Zaid, Sylla, Feitoto wakisukuma sana mashambulizi kwetu hasa kipindi cha pili, Mimi nilitegemea sana kipindi cha pili kinaanza kocha angemtoa Ngoma na Ahoua na kumuingiza Mavambo na Awesu Awesu.Hata hivyo haikuwa hivyo, badala yake yeye anawafuata mashabiki na kuwaaambia waongeze sauti gemu imeshaisha hiyo wakati sio kweli.

Pia Zimbwe amekuwa anajisahau sana, hii sio mara ya kwanza kwa Zimbwe kutuchomesha, mnakumbuka mechi ya Yanga ile ya 2 2 ambayo Yanga walisawazisha kwa BAO la pili la mzanzibar Banka mechi ambayo Deo Kanda aliwasumbua sana Yanga lakini Yanga wakarudisha mabao yote mawili kipindi cha 2, Zimbwe alijisasahau Banka akasawazisha akimuacha Manula hana cha kufanya.

Leo tunamweka sana benchi Kijiji kwa kosa la mechi vs ya Yanga lakini Zimbwe naye anatakiwa kula adhabu kama Kijiji, tuache ubaguzi na upendeleo.
 
Sasa ndugu marekebisho gani ya wiki,,,yule kocha ule muda aliokua anashangilia na mashabik ni muda ambao alitakiwa afanye sub ikiwemo ya zimbwe
 
Mmechanganyikiwa, wala haikuwepo haja ya kuandika, kijiji ndo mchezaji wa timu gani?
 
Hatuwezi wafunga yanga bhana , tutapata sare inatosha
Halafu baadae muje muanze kusema GSM anaharibu ligi huku uhalisia mmeshaanza kuuona wenyewe!, hapo mmecheza na azam tu tayari mmeshaanza kulia kabla ya tarehe 8... kweli kazi ni kipimo cha utu..🤣
 
Halafu baadae muje muanze kusema GSM anaharibu ligi huku uhalisia mmeshaanza kuuona wenyewe!, hapo mmecheza na azam tu tayari mmeshaanza kulia kabla ya tarehe 8... kweli kazi ni kipimo cha utu..
 
Narudia tena, Simba haijacheza vibaya. Simba imejipata mapema kuliko tulivyofikiria. Yanga anaweza kufa tena nyingi tu.
Mashabiki msiwatoe wachezaji kwenye reli. Draw ni matokeo ya kawaida dhidi ya tumu kama Azam! Yanga walifungwa!
 
Mnawapa bichwa hao utopwox wanaotepeta wakikutana na timu ambazo sio za gsm..
Azam ina timu nzuri kuliko makundi fc
Azam ni timu nzuri sana na inapata ushindani kamili nje ndani na still wako top 3 sio hao wadhamini wa timu 8
 
SIKU NINAANDIKA HAPA, SIMBA INAPASWA KUFANYA SAJILI ZA MABORESHO ZISIZOPUNGUA TANO.

TIMU BADO SANA KUFIKA WALAU NUSU WA ILE YA 2019.

WAACHANE NA.
1. Joshua Mutale.
2. Karabue Chamoe.
3 .Agustine Okejepha.
4. Dese Mukwala.
5. (Ngoma).
6 Manula.

MABORESHO YA SAJILI.
Beki wa kati NO 5.
Kiungo mkabaji No 6.
Kiungo mshambuliaji 10.
Mshambuliaji No 9.

Hadi leo sijapata majibu kwanini Fadru alisajili mchezaji mmoja tu Dirisha Dogo, ilinishangaza sana!!!!!!!!

Au ndio kuvizia ma Free Agent.

NIMEMALIZA
 
Back
Top Bottom