Simba FC futa benchi lote

bulabo

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2015
Posts
628
Reaction score
780
Kwa hali ilivyo simba inabd wafute benchi lote wasimuonee huruma hata matola mwenyewe kisa ni simba.

WE UNACHEZA NA PRISON UNAJUA KABISA NI WATU WA KUPARK BUS NA KUVIA
1. Unamuweka benchi mchezaj mwenye kasi kama Sakho.

2. Unajaza viungo wanaishia kucheza katikati tu.

3. Chama ameisha alikuwa anapoteza mipira na hakabi. Lakini pia yupo slow kwa mpira wa sasa ni haraka haraka mkicheza taratibu ni ngumu kufanya counter.

4. Vijana pia wapewe nafasi Jimmyson mhilu n.k.

5. Januari tulipuuza hatukununua wachezaj tukagamble na hawa wamechoka 4yrs wanatumika.

6. Ondoa bocco na mugalu mlete phiri kutoka zanaco.

7. Mbinu zetu zimepitwa na wakati mambo ya pira biriani mwisho wa siku wachezaj wa simba wanacheza na majukwaa.

8. Tunajua siku zote mechi ya prison ni ngumu benchi laufundi hawakufanyia kazi namna ya kufungua beki line yao ambayo ilikuwa na watu kama 10 wakiwa hawana mpira.

9. Mazoezi ya Simba why yapo kwenye open space kila mtu anaona.

10. Je mazoezi ya Simba wanajifunza kweli kupiga faulooo.

11. Kocha asipobadilishwa hata nafasi ya pili hatuipati ngo
 
Wafute benchi muhim pia Januari tulipuuza hatukununua wachezaj tukagamble na hawa wamechoka 4yrs wanatumika
 
WAJUAJI kama WAJUAJI KWENYE UBORA WAO.....Eti wachezaji 4 yrs wanatumika ivi kina Lukaku,Salah,Cr7,Zlatan na washambuliaji wengne uko dunia wanamiaka 10+ kwenye game na wanapeta unasema nini wewe??

Sakho:;Tuliwahi kum(OVERRATE) ILA mechi mbili 3 za mwisho kacheza nini uwanjani zaidi ya kukosa magoli..Leo akikaa benchi unalalamika....

Mhilu,Mzamiru::Wakikaa benchi lawama wakipewa nafasi wanacheza upuuz tu bado unalalamika

Punguza Lawama mkuu
 
WAJUAJI kama WAJUAJI KWENYE UBORA WAO.....Eti wachezaji 4 yrs wanatumika ivi kina Lukaku,Salah,Cr7,Zlatan na washambuliaji wengne uko dunia wanamiaka 10+ kwenye game na wanapeta unasema nini wewe?....
Hao akina Salah umri unawabeba, sasa boko na Kagere walianza kucheza mpira pamoja na Zidane miaka ya 2008 huko. Angalia Samir Nasri, kastafu, jack wilsheya,kazora wote hawawezi kucheza kama vile zamani.

Kila kitabu na zama zake , boko sio wa kutumainiwa tena na Mugalu kama Mugalu yeye kila siku uwanjani anajifunza namna ya kufunga ila hadi leo ajui, jana mlimuona analivyopeleka mpira kwa mashabiki
 
Jana niliandika uzi kama huu nikaamua kuahirisha kuupost.

Ila nimechukizwa sana na kuona makocha wasivyofikiri vizuri.

Simba ilihitaji wachezaji wasumbufu kule mbele mithili ya Sakho na Morrison.
Unawezaje kumuanzisha bench mchezaji kama Sakho?

Kusema kweli Matola na Pablo sioni kama wanaipeleka timu yetu popote.
 
Tukatae tukubali ukweli mchungu ni kuwa benchi la ufundi la Simba nalo lina matatizo yake. Haiwezekani timu inacheza dakika ya kwanza mpaka ya 30 timu haijapiga shuti hata moja halafu benchi la ufundi halishtuki kubadilisha wachezaji au mfumo/mpango kazi. Yaani timu inacheza vile vile halafu ilikuwa inategemea ipate goli? Hii Prison iliisumbua Simba msimu uliopita tena ikiwa na Luis ndani kwa mfumo wao wa kupaki basi sasa kwa mwaka mzima benchi la ufundi halijafanyia kazi tatizo hilo sijui huwa wanafundisha nini kwenye viwanja vya mazoezi. Na huyo "analyst " wao anafanya kazi gani iwapo kwenye mechi ya jana hata upangaji wa timu haukuendana na aina ya timu pinzani wanayopambana nayo?

Muda mwingi wa kipindi cha kwanza Simba walikuwa wanamiliki mpira kwenye nusu yao wakipigiana pasi fupi fupi na benchi la ufundi limekaa tu limeridhika au kwa kuwa mshahara wao unaingia washinde wasishine? Hivi walikuwa hawaoni tatizo timu imeaanza na viungo wakabaji wawili halafu tena Dilunga, Bwallya na Chama wote wanashuka tena kwenye nusu yao na kumuacha Kagere yupo "isolated" na mabeki watatu wa Prison. Kwa Chama kushuka naweza nikaelewa kidogo kwa sababu alikuwa "playmaker" sasa Dilunga na hasa Bwallya alikuwa anashuka muda wote wa mchezo kwenye nusu yao halafu anaishia kucheza pasi fupi alikuwa anategemea nani ampe mpira Kagere au nani acheze "second balls" pale Kagere anapopambana na mabeki wa Prison? Si ilikuwa inatosha tu kwa Chama kuwa anashuka halafu Dilunga na Bwallya wabaki juu kwenye robo ya tatu ya uwanja hasa ukizingatia uwezo binafsi wa Bwallya kua "unlock" ukuta wa timu pinzani. Sasa hata hili benchi la ufundi lilikuwa halioni na kulifanyia kazi. Vipi kama "plan B" ingekuwa kumtoa Bwallya baada ya dakiaka ya 25 na kumuingiza Sakho ambaye huwa siku zote hawaogopi mabeki anawafuata kwani mwelekeo wa Prison ilikuwa ni kupaki basi mwanzo mwisho.

Lakini kiukweli benchi la ufundi la Simba linahitajika lifanye kazi ya ziada kwenye maeneo yafuatayo:-
1. Upigaji wa mipira ya kona na krosi. kama Mwenda jana anaenda kupiga krosi miguuni kwa adui zaidi ya mara tatu anategemea mpira upite vipi kwenda kwa mshambuliaji wake?
2. Tabia ya kurudisha mpira nyuma kila mara. Hapa Gadiel Michael (japo jana hakucheza), Muzamiru, Bwallya na Mwenda ndio michezo yao badala ya kupeleka timu mbele wao kila saa kugeukia golini kwao. Na hapa unakuta mpaka mchezaji wa kiungo naye anageukia golini kwake anarudhisha mpira nyuma zaidi hata ya mara kumi. Hivi ku "turn " na mpira kuelekea mbele pia benchi la ufundi limeshindwa kufundisha.
3. Timu kupeleka mpira mbele kwa haraka. Kanuni rahisi sana ya mpira inayojulikana duniani kote ni kuwa ili kumfunga adui wako mlazimishe afanye makosa na wewe yatumie makosa yake vizuri upate goli. Sasa Simba ilikuwa inacheza taratibu sana "square pass " kwenye nusu yake hilo goli wangelipata wapi hata kama ile mechi ingechezwa mpaka saa sita siku? Ashukuruwe sana refarii ambaye ndiye alikuwa nyota wa mchezo. Na hili mashabiki wa Simba wasilifurahie sana kwani kwenye Shirikisho itawagharimu sana.
4. Sio kila mara lazima mpira uanzie nyuma kwa dakika zote 90. Kwa mfano jana kuna wakati Prison walikuwa wanakuja kushambulia kwa hiyo kidogo walikuwa wanaacha nafasi kule nyuma lakini kipa anadaka badala ya kumpigia moja kwa moja Kagere ambaye kwa wakati huo yupo na mabeki wawili tu kipa anakaa anasubiri Prison warudi wajipange halafu anaanza na mabeki wake.
 
Simba yangu ipo hoi bin taaban,kwakweli ushindi wa jana haujanipa matumaini mimi kama shabiki wa Simba.

nakubaliana na mleta mada benchi la ufundi lote lipigwe chini tena ikiwezekana na viboko viwahusu wote pamoja na huyo kocha wa Madrid ya Kimara bonyokwa.
 
namba 9 tumeshasema ila wanajifanya vichwa maji, ni rahisi timu pinzani kujua simba watakuja na mfumo gani ili wawazuie
 
Tatizo la simba liko kwenye bench la ufundi na managment ya timu.kwasababu inaonekana hawa watu wana kiburi ndo maana hatuoni marekebisho ya mapungufu ya wazi yanayojitokeza uwanjani kila siku.Ukiangalia utaona kabisa nikama vile bench la ufundi hawajui kutumia kikosi walichonacho na uongozi umeizira timu.Maana mambo yako vile vile toka anaondoka uchebe hadi leo.kwahiyo utaona kuna watu wako kwenye timu ambao labda ni wabishi au ni wajuaji kiasi chakufanya timu icheze mpira wa kubahatisha au mbinu zile zile na mapungufu yale yale na makosa yale yale. Wachezaji bado wako vizuri ni mbinu tu za namna yakuwachezesha ndo bench la ufundi limeshindwa.Lakini pia timu haina morali kabisa kwahiyo napata mashaka labda kuna shida ambayo sisi mashabiki hatuijui.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Ifike mahali wachezaji wasifuate mbinu za makocha vilaza km Pablo na matola ,wao wakiingia uwanjan wabadir game plan kuipambania Simba maana Ni Waz hao makocha hawana jipya.

Pokea maelekezo ya kocha yatumie dakika ishirin wakiona hakuna kitu basi waamue wao ndani ya uwanja kwa kuswitch kwenda plan B ambayo Ni yao wao km wachezaji maana wao ndio wanajua wafanye nn ili wapenye ngome ya mpinzan
 
Exactly kabisa

Jana nilikuwa natafakari kwanini chama asingeshuka katikati huku akibaki Bwalya upande wa chama?

Chama siyo Mzuri akitokea pembeni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…