Simba Haina ubora anaotuamisha Haji Manara

Simba Haina ubora anaotuamisha Haji Manara

Hziyech22

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
15,351
Reaction score
21,362
Simba ya msimu uliyopita ndo ilikuwa yenye ubora na sio hii ya sasa.Kuna mambo yaliyochangia Simba hii isiwe na ubora

USAJILI
Baada ya Simba kufanikiwa kuingia robo fainal kwenye CAF champions league wakajiona wapo level moja na team kama As vita baada kutolewa wakajipanga kwenye usajili na wakawaacha watu muhimu waliyochangia Simba kufika hatua Hiyo mtu Kama okwi, kotei wakawaona hawana maana wakawaona wabrazil wenye maana.

Simba wakasema okwi anataka dau kubwa Cha ajabu wakapoteza hela nyingi kwa yule striker mbrazili ambaye tokea atue Simba amecheza mechi tatu tu na zote ameanzia benchi Hiyo ni hasara moja, hasara ya pili wametoa accommodation facilities kwa mchezaji huyo hewa Kama kulala hotel nzuri, kuishi nyumba nzuri ya kupanga, hasara ya tatu gharama ya kuvunja naye mkataba.

Simba walitakiwa wasajili beki mmoja, kiungo na mshambuliaji mmoja basi ili wafike malengo yao ya kufanya vizuri Tena CAF champions league Cha ajabu wamesajili viungo wengi washambuliaji na ambao hawakabi na kuacha sehemu nyeti ambapo tuliona tatizo lao ni beki na kiungo mkabaji ili kuziba pengo la kotei pamoja na kuziba udhaifu wao wangemsajili yule beki number 5 wa nkana wangelamba dume.

KUMFUKUZA UCHEBE
Wamemfukuza kocha mzuri uchebe wamemleta kocha kituko.ukiangalia Simba hii ya sasa ni rahisi sana kufungika kwanza wanaacha space kubwa kwa opponent kumshambulia ndomaana inakuwa rahisi Simba kufikiwa kwenye lango lake ingekuwa hizi team ndogo Zina wachezaji angalau wana quality japo ya 50% Kama team ya Mtibwa hadi sasa simba angepoteza game nyingi Sana wachezaji binafsi wanambeba huyo kocha.

Tatizo lingine wapo slow kwenye kutengeneza mashambulizi tofauti na kipindi yupo uchebe walikuwa wanaocheza with high intensity.Tatizo lingine Simba wakiwa Hawana mpira wanakuwa ovyo Sana hawakabi unaweza kuwafanya chochote unachotaka wewe.

NB: Mo asipokuwa makini hela zake zitapotea kiholela holela makosa waliyofanya Simba msimu Huu yanaweza kujirudia miaka ijayo Kama wazee wa 10% wataendelea kuwepo hapo Simba na malengo ya kufika mbali kwenye michuano ya CAF champions league yatafifia.
 
Simba ni mbumbumbu
Mo.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom