Simba haitochukua taji lolote msimu huu wa 2018/2019

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Kutokana na mwenendo wa timu ulivyo kwasasa, Simba haitobeba taji lolote kwa msimu huu.

Wachezaji wanaonekana wameridhika na viwango vyao walivyoonesha katika mechi za Nkana, Mbabane na Js Soura. Baada ya hapo hawana tena consistency wanacheza ili mradi kukamilisha ratiba. Wana mechi ngumu dhidi ya Al Ahly ambapo nadhani ikipungua sana dozi inaweza kuwa 5-0 tena.

Ukija kwenye ligi, licha ya kuwa na viporo sidhani kama watavitumia vyema, kwani ikumbukwe wachezaji hao hao watakuwa wamechoka kutokana na mechi za ligi ya mabingwa ya Afrika.

Pia kama mabadiliko ya benchi la ufundi yasipofanyika mapema, Simba hata 4 bora anaweza asiwepo kwani inaonekana wazi kocha wa sasa ameshindwa kukontroo nidhamu za wachezaji wake hadi wengine kufikia kutoroka kambini.

Nimalizie kwa kusema, japo ni ngumu kunielewa lakini ukweli mchungu ni kwamba, ifikapo mei mwaka huu Simba itakuwa inamaliza msimu wa 2018/2019 bila ya taji lolote lile na hapo ndipo hali ya sintofahamu itakapoanza klabuni.

Tukutane mei.
 
Mi tokea juzi yanga alipotolewa mapinduz na. Sport pesa na. Simba kutolewa ktk hatua ya nusu fainal pia mbao. Na timu za tz kushindwa kubakisha kikombe cha. Mapinduz nyumbani nmeona nijiuzuru kushabikia timu hapa bongo nahamia Ulaya mazima. Hapa nitakuwa nazhangilia. Atakaeshinda. Kwa siku husika tu ama kuchukua ubingwa na yy akibolonga. Kesho nazhangilia timu nyingine itakayofanya vizur tu staki tena kuwa na timu maalum ya kushambikia staki pesha wala kufa mapema mpira bongo bado saaaana yaaani.

Pia kingine kilichoniuzi ni ushambiki wetu sisi watz yaani kama timu inawakilisha nchi bado kuna watu watashabikia timu pinzani za nje hali timu kama yanga au simba au timu yoyote inapowakilisha nchi inatakiwa tuwe wazarendo kushabikia hiyo lakini hapa bongo mambo ni tofauti kabisa yaani mpaka watu na nchi zingine wanatushangaa kwa ujinga huuu.. Mimi. Juzi kati simba ilicheza na timu ya kutoka mkoa wangu mashujaa ktk kombe la shifikisho simba alifungwa na. Mashujaa. Lakin kutokana na uzalendo wangu mi siku hiyo nilikuwa mshabiki wa mashujaa bila kujali simba ndo chama langh ila nyumbani ni nyumbani buana na huu unatakiwa watz wote tuwe.. Yaaani hizo tabia ndo zimekera na kuamua kutoshabikia timu yoyote bongo. KAMA. HIYO TABIA. IMEKUKUKERA NA WEWE LINK HII POST TUONE NI. WATZ WANGAPI HATUIPENDI

{Hutajuta ukitembelea
& kusubscribe chanel yangu ya youtube jina Misifa Skills,Link hii hapa
 
Tatizo kubwa la simba ni incomptent players, wachezaji dzain km wameridhika vile yaani kuendesha gx 100 anaona km alishamaliza kwenye maisha ...km uliangalia mechi dhidi ya as vita wachezaji walikuwa wanacheza km wamelazimishwa yaani hawana uchungu kusema mpira ni kazi yangu inatakiwa nipigane kila dk kuhakikisha timu yangu inashinda

Ushauri wangu simba wafanye maamuzi magumu ya kuwafukuza wachezaji wote wasiojielewa wakianzia na kichuya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ya kutoroka kambini sikuisikia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeandika maneno mengiiiii kumbe unataka subscribers acha mambo yako wewe.
.
Hakuna mpenda soka popote duniani asieshabikia soka la ligi yao ashabikie la taifa jingine hata kama ni zuzu
 
Sheikh Yahya at work. Ofisi ipo wapi?
Ujinga ni maradhi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…