Simba haitochukua taji lolote msimu huu wa 2018/2019

Simba haitochukua taji lolote msimu huu wa 2018/2019

RUDI USOME UZI WAKO. Uliyoyasema YAMETIMIA
Kutokana na mwenendo wa timu ulivyo kwasasa, Simba haitobeba taji lolote kwa msimu huu.

Wachezaji wanaonekana wameridhika na viwango vyao walivyoonesha katika mechi za Nkana, Mbabane na Js Soura. Baada ya hapo hawana tena consistency wanacheza ili mradi kukamilisha ratiba. Wana mechi ngumu dhidi ya Al Ahly ambapo nadhani ikipungua sana dozi inaweza kuwa 5-0 tena.

Ukija kwenye ligi, licha ya kuwa na viporo sidhani kama watavitumia vyema, kwani ikumbukwe wachezaji hao hao watakuwa wamechoka kutokana na mechi za ligi ya mabingwa ya Afrika.

Pia kama mabadiliko ya benchi la ufundi yasipofanyika mapema, Simba hata 4 bora anaweza asiwepo kwani inaonekana wazi kocha wa sasa ameshindwa kukontroo nidhamu za wachezaji wake hadi wengine kufikia kutoroka kambini.

Nimalizie kwa kusema, japo ni ngumu kunielewa lakini ukweli mchungu ni kwamba, ifikapo mei mwaka huu Simba itakuwa inamaliza msimu wa 2018/2019 bila ya taji lolote lile na hapo ndipo hali ya sintofahamu itakapoanza klabuni.

Tukutane mei.
 
Back
Top Bottom