MaxShimba
JF-Expert Member
- Apr 11, 2008
- 35,771
- 4,065
Simba: Hatuchezi tena na Yanga
Na Suleiman Mbuguni
UONGOZI wa klabu ya Simba umetishia kutocheza mechi na watani wao wa jadi, Yanga, endapo mechi zao zitaendelea kuchezeshwa na waamuzi wa hapa nchini.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Hassan Dalali alisema ni bora mechi zao na Yanga zikachezeshwa na waamuzi kutoka nje ya nchi, ambao hawatakuwa na mapenzi na timu hizo.
Dalali alisema hii ni mechi ya nne kati ya tano mfululizo, ambazo wamecheza na Yanga na mara zote ni lazima mchezaji wao apewe kadi nyekundu na hivyokucheza pungufu.
"Victor Costa alitolewa Mwanza, Henry Joseph alitolewa Morogoro, Moses Odhiambo alitolewa hapa Dar es Salaam na mechi ya juzi, wachezaji wetu wawili walitolewa kwa kadi nyekundu na Yanga mmoja lakini, mara zote ni kuhakikisha, Simba inakuwa pungufu," alidai Dalali.
Hata hivyo Dalali alisema, uongozi wa Simba una imani kubwa na wachezaji, lakini kuna baadhi yao wameamua kutumikia ufisadi, ambapo dawa yao ipo jikoni kwa uchunguzi ambao unaendelea.
Mwenyekiti huo aliwaomba wana-Simba kuendelea kuwasaidia wachezaji wao hasa wale wenye moyo imara na kuamua kutumika klabu hiyo kwa moyo mkunjufu na kwamba katika dirisha dogo la usajili kikosi kitaimarishwa zaidi.
"Jambo la pili ni vizuri tukaanza kuchangia klabu yetu kwa hali na mali, klabu yetu ni timu ya watu na si ya mtu, hivyo tutazindua kampeni maalumu itakayosimamiwa na kamati mahsusi kwa ajili ya kuchangia klabu yetu, kampeni hii itakuwa ya nchi nzima," alisema Dalali.
Dalali alisema timu yao ipo imara na itapambana kwa nguvu zote na kuwataka kutembea kifua mbele bila wasiwasi kwa kuwa kikosi chao ni bora. Simba Jumapili ilifungwa bao 1-0, kipigo kilichomaliza miaka sita ya Yanga kutoifunga Simba.
Tuma kwa Rafiki Nakala inayochapika
Nakala kutoka Gazeti la Majira