Simba: Hatuchezi tena na Yanga

Simba: Hatuchezi tena na Yanga

MaxShimba

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2008
Posts
35,771
Reaction score
4,065


Simba: Hatuchezi tena na Yanga
Na Suleiman Mbuguni

UONGOZI wa klabu ya Simba umetishia kutocheza mechi na watani wao wa jadi, Yanga, endapo mechi zao zitaendelea kuchezeshwa na waamuzi wa hapa nchini.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Hassan Dalali alisema ni bora mechi zao na Yanga zikachezeshwa na waamuzi kutoka nje ya nchi, ambao hawatakuwa na mapenzi na timu hizo.

Dalali alisema hii ni mechi ya nne kati ya tano mfululizo, ambazo wamecheza na Yanga na mara zote ni lazima mchezaji wao apewe kadi nyekundu na hivyokucheza pungufu.

"Victor Costa alitolewa Mwanza, Henry Joseph alitolewa Morogoro, Moses Odhiambo alitolewa hapa Dar es Salaam na mechi ya juzi, wachezaji wetu wawili walitolewa kwa kadi nyekundu na Yanga mmoja lakini, mara zote ni kuhakikisha, Simba inakuwa pungufu," alidai Dalali.

Hata hivyo Dalali alisema, uongozi wa Simba una imani kubwa na wachezaji, lakini kuna baadhi yao wameamua kutumikia ufisadi, ambapo dawa yao ipo jikoni kwa uchunguzi ambao unaendelea.

Mwenyekiti huo aliwaomba wana-Simba kuendelea kuwasaidia wachezaji wao hasa wale wenye moyo imara na kuamua kutumika klabu hiyo kwa moyo mkunjufu na kwamba katika dirisha dogo la usajili kikosi kitaimarishwa zaidi.

"Jambo la pili ni vizuri tukaanza kuchangia klabu yetu kwa hali na mali, klabu yetu ni timu ya watu na si ya mtu, hivyo tutazindua kampeni maalumu itakayosimamiwa na kamati mahsusi kwa ajili ya kuchangia klabu yetu, kampeni hii itakuwa ya nchi nzima," alisema Dalali.

Dalali alisema timu yao ipo imara na itapambana kwa nguvu zote na kuwataka kutembea kifua mbele bila wasiwasi kwa kuwa kikosi chao ni bora. Simba Jumapili ilifungwa bao 1-0, kipigo kilichomaliza miaka sita ya Yanga kutoifunga Simba.

Tuma kwa Rafiki Nakala inayochapika

Nakala kutoka Gazeti la Majira

 
Politiki hizo hakuna kitu hapo....Mechi watacheza kama kawaida
 
Mbona walivyokuwa wanashinda hawakusema hayo
 
Pamoja na kufungwa kwa simba lakini Dalali ametoa point moja ya msingi, hivi kweli Simba na Yanga lazima achezeshe Mwandike? na Kamisaa awe Lwiza? kuna siri gani hapo inafichwa?kwanini wanasimba wasidhani kuwa TFF inaendekeza unazi?
 
Pamoja na kufungwa kwa simba lakini Dalali ametoa point moja ya msingi, hivi kweli Simba na Yanga lazima achezeshe Mwandike? na Kamisaa awe Lwiza? kuna siri gani hapo inafichwa?kwanini wanasimba wasidhani kuwa TFF inaendekeza unazi?

Unazi kwa nani? haohao ndo walokua wakichezesha na simba wakawa wanashinda. Yanga kila mara walikua wakimlalamikia mwandike. Hizo ni siasa za soka tu. Hivi nikiuliza katika hizo mechi 4 walizofungwa alichezesha mwandike? wacha kuunga mkono mambo yasiyoungika.
 
Simba watalalamika mpaka watachoka. Hamna kitu. Maana mbali na mechi ya Yanga wamefungwa mechi nyingi tu na wanashikilia nafasi ya 7 kutoka juu wakati ndio inaanza raundi ya pili. Sasa kote huko wanaonewa?
Hali yao iko mahututi na kwa kuwa Dalali hataki kujiuzuru kama alivyoahidi anafuta bangusilo.😀
 
Simba wana point 13 na Yanga hadi sasa wana pointi 27. Je hapo tulinganishe wapi kwa wapi!
 
Refa mgeni..... ha ha haaaa, watani mkubali tu kwamba jembe likiwa butu hata ubadili mpini kazi ni ile ile!!! zibeni viraka msimbazi na sio waamuzi manake duh, mwaka si wenu huu yakhe!!!
 
wanakaribia kukata roho hao ndo maana wanatapatapa, je juzi wangeshinda si wangemfananisha mwandike na corina?
ni maneno ya soka ya kuwapoza washabiki wao.
na mechi ijayo hata refa akiwa dalali wanakalishwa tena kwenye kifuu na maisha yanaendelea....pumbaaaavu
 
Back
Top Bottom