Simba hii inakufa kama zilivyokufa African Lyon

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Ni kama mzaha mzaha lakini ninaiona timu hii ikiwa chini sana na ikibaki premier ni kwa sababu za kisiasa tu ili utani wa yanga na simba usife.

Sote tuliona jinsi African Lyon ilivyokufa na mmiliki ni huyu huyu mbwia unga.
Kibaya zaidi tuna wanachama wajinga sana pale Dar ambao ndio wapiga kura.
Hapo ndipo ubaya wa demokrasia tunauona.Wapiga kura wasipokuwa bora,tutapata viongozi wasio bora,wengi wakiwa wahuni tutapata viongozi wahuni.

Kwa sasa ni kama hakuna dawa ya hili.
Tutaendelea na huyu mo na genge lake la viongozi wakituchezea akili huku wakiwa na nia ya kujimilikisha timu 100%
Hapa asipoingilia mtu mkubwa kama rais, simba ndio imekwisha hii


Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Mmezaliwa lini ndugu zetu hapo juu?

Si mara ya kwanza kwa Simba kuwa dhoofu kama ilivyo sasa...

Timu za Kariakoo huwa zinapishana kuwa juu, ni mara chache sana zote kuwa juu kimafanikio...
 
Pole sana Ndugu kama hujui vitu njoo hata Inbox uulize tutakusaidia.

Viongozi wa selikali ndio wanazing'ang'ania hizo timu zenu. Hawataki wawekezaji hawataki wadhamini.

Selikali imezuia usajili wa wanachama wapya ndani ya Club mwaka wa tano huu.

Hawataki wanachama wapya, hawataki fikra mbadala hawataki Mawanzo mbadala wala viongozi wapya makusudi kabisa.

MWENYE MASIKIO NA ASIKIE.
 
Mmezaliwa lini ndugu zetu hapo juu?

Si mara ya kwanza kwa Simba kuwa dhoofu kama ilivyo sasa...

Timu za Kariakoo huwa zinapishana kuwa juu, ni mara chache sana zote kuwa juu kimafanikio...
Umemaliza Kila kitu

Inaonekana mtoa mada hajui historia ya hizi timu mbili za Kariakoo

Alafu ajue kwamba Africa Lyon kamwe haiwezi kuwa Simba
 
kwani timu zilizopo kwenye ligi ni simba na yanga tu? Kwaini hao wawekezaji wasiwekeze kwenye timu zingine? Mbona MO alitelekeza timu yake ya sport lyon akakimbiria simba unajua sababu? unawaona serikali ni wajinga?
 
Pamoja na kwamba Simba kuna changamoto kubwa sana na nimezipigia kelele toka enzi ambapo haikuwa "popular" kufanya hivyo ila tusisahau tofauti ya point kati ya Simba na anayeongoza ligi ya NBC kwa sasa ni sare mbili tu. Yaani anayeongoza akipata sare mbili tu, wanalingana point. Kwa hiyo ukiniambia Simba ni mbovu nitakuuliza kulinganisha na nani?

Suluhisho la kwanza kuinusuru Simba ni kuongeza ukubwa wa team ya management. Inahitaji watu wa kutosha katika kila idara, kuwe na wafuatiliaji wa mambo na wasimamizi imara wa shughuli za klabu na timu. Kosa kubwa limefanyika kuipa Bodi ya Wakurugenzi kazi ambazo siyo zake.
 
Serikali itafanya vyovyote ili isife, ikiwezekana hata kupewa kombe kama kwny ngao ya jamii[emoji23]
Simba imeshajinyea huo upendeleo hawatakaa waupate tena wasiporekebisha makosa yao.
Kile kitendo cha semaji lao kuishutumu Serikali kuhusu ile safari ya South Africa ya Wana YANGA na viongozi wa timu kutokujiweka kando na kauli ile hata kinafiki tu, na pia kufurahia waziwazi kuondolewa kimizengwe timu ya YANGA kumeonekana kama ni kwenda kinyume na msimamo wa Serikali, na kujishushia hadhi kwa Serikali.
Wasubiri 2024/2025 wakacheze ligi moja na WanaTP Lindanda au Pan Africa na mwaka unaofuata Ndanda.
Wajitahidi watengeneze timu ya ushindani na viongozi wanaojielewa ndio dawa pekee itakayo waokoa.
Sometimes uchawa unalipa.
Funika kombe mwanaharamu apite.
 
kauli ile hata kinafiki tu, na pia kufurahia waziwazi kuondolewa kimizengwe timu ya YANGA kumeonekana kama ni kwenda kinyume na msimamo wa Serikali
Kwani baada ya zile mechi za kwanza za Dar ambapo Simba alifungwa 1-0, msemaji wa Yanga alibaki na kauli za ki-solidarity?
 
Na huko FA kuna sare au tofauti ya point ngapi?
 
kwani timu zilizopo kwenye ligi ni simba na yanga tu? Kwaini hao wawekezaji wasiwekeze kwenye timu zingine? Mbona MO alitelekeza timu yake ya sport lyon akakimbiria simba unajua sababu? unawaona serikali ni wajinga?
Hujiulizi kwa nini GSM asiende kuwekez a Lipuli au Majimaji?
 
Subiri siku utapigwa goli 9 ndio utajua huo uhuni mnaousapoti ninyi mashabiki wa Dar

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…