Simba hii inakufa kama zilivyokufa African Lyon

Simba hii inakufa kama zilivyokufa African Lyon

Pole sana Ndugu kama hujui vitu njoo hata Inbox uulize tutakusaidia.

Viongozi wa selikali ndio wanazing'ang'ania hizo timu zenu. Hawataki wawekezaji hawataki wadhamini.

Selikali imezuia usajili wa wanachama wapya ndani ya Club mwaka wa tano huu.

Hawataki wanachama wapya, hawataki fikra mbadala hawataki Mawanzo mbadala wala viongozi wapya makusudi kabisa.

MWENYE MASIKIO NA ASIKIE.
Kama hii ni kweli, mbona wanachama wameshindwa kumtoa Mangungu? Kiongozi anafikia kuleta mchezaji wa timu ya Far East kumpigia kampeni na wanachama wanaona ni hoja ya kumpasisha? Mjinga kiongozi au wanachama?
 
Tatizo linapokuja Simba inataka ijifananishe na Yanga, badala kufocus na vitu vya msingi Kwa upande wao, wao humchungulia jirani kwanza then unakwenda na biti ya jirani...jirani akifeli Simba inashangilia kuwa hapo Sasa tupo sawa, Yanga hawajilinganishi na Simba siku hizi hivyo huangalia ya kwao namna ya kutoboa, njoo huku kwetu Simba Sasa tunataka kuwa kama Yanga kitu ambacho kinaharibu utaratibu, ni ngumu sana kufanya maamuzi Sasa ukiwa na hofu ya kushindwa.
 
Unaumwa. Utakufa na kuiacha Simba ikiwa Simba kama ulivyozaliwa ukaikuta. Acha kutusumbua na vitu vya kuokoteza
 
Mmezaliwa lini ndugu zetu hapo juu?

Si mara ya kwanza kwa Simba kuwa dhoofu kama ilivyo sasa...

Timu za Kariakoo huwa zinapishana kuwa juu, ni mara chache sana zote kuwa juu kimafanikio...
Ilishindwa kufa Yanga Bakuli, ije ife Simba hii???
 
Hahahaah mnachekesha sana...nyie mlikufa ile miaka 4 ya msoto?? Hebu mtupishe na vi theory vyenu..
 
Pole sana Ndugu kama hujui vitu njoo hata Inbox uulize tutakusaidia.

Viongozi wa selikali ndio wanazing'ang'ania hizo timu zenu. Hawataki wawekezaji hawataki wadhamini.

Selikali imezuia usajili wa wanachama wapya ndani ya Club mwaka wa tano huu.

Hawataki wanachama wapya, hawataki fikra mbadala hawataki Mawanzo mbadala wala viongozi wapya makusudi kabisa.

MWENYE MASIKIO NA ASIKIE.
Kisiasa, hizi timu haziwezi kuwa na wawekezaji kamili... Yaani haziwezi milikiwa na mtu yeyote... Imagine timu ina wanachama 20m+... Hizo ni kura kabisa za kuweza muweka mtu madarakani
 
Unajua try again anasimamoa biashara za nani?
Mangungu kawekwa na nani?
Vunja Bei aliwekwa na nani?
Kwanini mo katika wajumbe wa bodi lazima aweke wanasiasa.
Uliuliza watu ndani ya Simba watakwambia na hao wanasiasa ndio waliilazimisha tume ya ushindani kupitisha mchakato pamoja na kujua una walakini.
Mangungu ni mwanasiasa ana sauti gani pale Simba?

Try again ni mwanasiasa ?

Unaweza kuzitofautisha Simba na Yanga na Siasa za nchi hii ?
 
Kipindi cha nyuma huko Simba inapokua na migogoro hua haiathiri sana performance uwanjani kwa sababu wachezaji walikua hawajiingizi kwenye hiyo migogoro tofauti na Yanga.
Lakini kipindi hiki unahisi hasa wachezaji nao wanachagua upande. Ni hatari kubwa hii.
Muombeni KARIA aisogeze mbele mechi ya tarehe 20/4 vinginevyo mazao ya hiyo mechi ni kukosa hata nafasi ya 4.
NI MTAZAMO TU.
Simba kuna mgogoro ?
 
Simba kuna mgogoro ?
Mgogoro upo viongozi wanaficha.
Maelewano hayapo baina ya upande wa wanachama na mwekezaji.
Mwekezaji ameisusa timu kiana, Mpunga aliokua anautoa hapo mwanzo ameupunguza kwa kiasi kubwa mpaka kupelekea Klabu kubana matumizi yasiyo ya lazima mfano bonasi za wachezaji na kupelekea kupunguza morali wao
Mwekezaji aliposema timu ameinunua miaka 5 nyuma hakusema kwa bahati mbaya yule.
Wishes zake ni kuimiliki timu na sio kua mfadhili, na ndio maana katiba yenu ya mchongo inampa nguvu yeye kuliko majority shareholders ambao ni wanachama.
Upande wa wanachama wanataka mabadiliko ya katiba yatakayo wapa nguvu wao, mwekezaji hataki.
NDIO MISUSO YOTE HIYO.

Hao kina "JARIBU TENA na WEEDS" ndio watetezi wenu lakini ndio wanaoonekana hawafai.
 
Huko kuyumba kwa simba ni kwa sababu ya siasa ,husuda....mmeinunua Ihefu kisa ilikuwa inawaharibia siasa zenu.
 
Back
Top Bottom