Simba hii ni sawa na Nigeria ya Kombe la Dunia 1998. Inashinda ila siuoni ufundi kabisa

Simba hii ni sawa na Nigeria ya Kombe la Dunia 1998. Inashinda ila siuoni ufundi kabisa

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Posts
1,761
Reaction score
2,391
Niseme tu labda siwafahamu De Agosto vizuri. Lakini mpira wa Jumapili wa Simba sikuelewa, butu butu nyingi.

Ubora wa timu niliouona kwa Mgunda ni ifuatayo;

Uchaguzi mzuri wa wachezaji.
1. Niliona mapungufu ya Quatara yakifanyiwa kazi. Na Kanute anakuwa mzuiaji wa chini kabisa. Anazuia mipira ya juu na kwa ushirikiano mzuri na Onyango. Pia Chama na okra kuwa huru kucheza mpira, sivyo kocha alivyoondoka anavyotaka.

2. Timu imekuwa hatari sana mwishoni. Unaona Chama anaprogramu mazoezini. Goli la Phiri ni Chama mtupu. Unaona wachezaji wana uhuru wa kufanya na kuongeza programu zao mazoezini kabisa.

Madhaifu ya kufanyia kazi
Lazima Simba irudishe utulivu. Simba siyo ya kubutua butua hivyo. Simba siyo ya kupanda yote na kurudi kidogo kidogo. Simba unakoswa magoli.

Hata kama tunafanya mashambulizi ya kushitukiza yapite kwenye njia, kwa uhakika na mipango, tusiangalie matokeo. Wakicheza hivyo makundi, robo hatutoboi.

Makosa ya Nigeria mwaka 1998. June 13 anashinda 3-2 dhidi ya Spain kwa pira la hivi hivi. Denmark inawasoma. 16 Bora watu wanaweka hesabu vizuri wanalala 4-0 watu wanasema wamehongwa. Piga mashuti ya mbali nje.

Tulimchukia sana okocha. Pamoja na ushindi Simba inatakiwa kuwa watulivu sana. Enonga na Onyango wacheze Tena Mpira waache pasi ndeefu Kama minazi zisizo na macho.
 
Fumba jicho moja ndo utaanza kuuona ufundi

Sjasema jicho gani mkuu
 
Team ikifunguka kama kule Jo burg ikapigwa 4-0 na kaizer chiefs inalaumiwa kwamba haikuonyesha heshima ugenini..ile mechi ya South Afica simba alipiga mpira mzuri akala 4

Ulitaka wachezaje ugenini ndugu yangu? agh aiseee au unadhani al hilal ilivyocheza juzi dar es salaam ndiyo itakavyocheza nyumbani?
 
Simba hamna kitu maneno mengi
FB_IMG_16640567488881733.jpg
 
team ikifunguka kama kule Jo burg ikapigwa 4-0 na kaizer chiefs inalaumiwa kwamba haikuonyesha heshima ugenini..ile mechi ya south afica simba alipiga mpira mzuri akala 4

Ulitaka wachezaje ugenini ndugu yangu? agh aiseee au unadhani al hilal ilivyocheza juzi dar es salaam ndiyo itakavyocheza nyumbani?
Kama nakuelewa kwa mbaaali hivi. Ngoja niangalie marudiano ntakoment kitu
 
Hyo timu ilifungwa 6 na Namungo , hyo Tu inatosha kukujuza kuwa hyo timu ni mbovu
 
Hyo timu ilifungwa 6 na Namungo , hyo Tu inatosha kukujuza kuwa hyo timu ni mbovu
Ina points 10 za caf ni ya 28 ,namungo ana points 2 ni wa 56, al hilal ana points 19.5 ni wa 19 simba ana points 28 ni wa 14 ....team kubwa ya hersi ina points 0.5 ni ya 75...0.5 utopolo fm
 
Back
Top Bottom