kibaravumba, Tuna mizigo ya kutosha sana pale watu kama chama, kagere, Wabrazili wote, Ndemla, Gadiel, Shamte yaani wapo wengi tu hawastahili kuwa pale.
Sent using
Jamii Forums mobile app
Mchezaji ninayemsikitikia ni Ndemla.
Habadiliki anacheza vilevile Mwaka hadi Mwaka. Hajifunzi hata kwa Mzamiru.
Ndemla kama angefanya bidii asingekuwa hapa nchini, lakini inaonekana anasubiri mazoezi ya kocha wake, na hana mazoezi binafsi.
Kijana mdogo hana kasi ya mbio, anasubiri mpira wa kuletewa, hawezi kupiga chenga. Asilimia 90 ya mashuti yake hayalengi goli. sijaona akipiga faulo au penati, ingawa ndiye mwenye mashuti mazito zaidi hapa nchini.
Ndemla angefanya mazoezi kwa bidii namba ambayo ingemfaa ni namba 9, yaani mtu wa kuuchukua mpira na kuuweka wavuni.
Ndemla anakipaji kikubwa sana lakini hajakigundua yeye mwenyewe.
Hajiamini uwanjani ni kama anauogopa mpira.
Mimi ningeambiwa unataka uwe kama nani ningechagua niwe kama Ndemla na mda huu ningekuwa nakipiga katika timu ya Ligi Kuu England.
Golikipa gani wa kudaka shuti la Ndemla. HAKUNA.
Wachezaji wengine ambao walikuwa na vipaji vikubwa Ila hawakujielewa ni Shiboli na Mwaikimba.
Vipaji vyao vimepotea kwa kuto jiamini tu na bidii ndogo ya mazoezi.
Msuva na Samata ni bidii na kujiamini kwao ndiko kunakowasaidia.
Hakina ninasikitika.
Sent using
Jamii Forums mobile app