Simba hii vilio basi, Wababe wa Ulaya kutoka Moscow nusura walale na viatu

Simba hii vilio basi, Wababe wa Ulaya kutoka Moscow nusura walale na viatu

Klabu kubwa hapa afrika Simba mnyama mkali leo imetoshana nguvu na vigogo wa soka barani ulaya CSKA Moscow kwa kufungana magoli 2-2 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliopigwa huko Dubai.

Magoli yote mawili ya Mnyama mkali Simba yametiwa kimiani na Mshambuliaji mkali Habib kyombo (Halland wa bongo)

Baada ya kumaliza mechi zake za kimataifa za kirafiki, timu ya Simba itaanza safari ya kurudi nchini iyo kesho jumatatu kujiandaa na mchezo wa ligi ya Nbc dhidi ya mbeya city unaotarajia kupigwa jumatano ya tarehe 18/Jan
Hamjamalizaaaaaaaaaaa
 
Tumeukubali Mzee[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]... Simba ni tishio ukanda huu wa maziwa makuu,Afrika na Dunia Kwa ujumla
Akili imekukaa sawa sasa acha kwenda kule kigamboni
 
Hana unyama wowote,timu imefungiwa dunia,haijacheza mwaka mzima,mnatoa sare🏃
Ligi ya kwao si inaendelea ? Wamefungiwa kucheza mashindano makubwa ulaya
 
Asante kwa taarifa.

Ila Moscow haipo Ulaya!

Yupo sahihi, Moscow ipo Ulaya(Europe)

N.B. Hii ni changamoto kwa wengi sana. Ila kiuhalisia Russia ni bara linalopatikana katika mabara haya mawili (Europe na Asia).
Japo, eneo kubwa la Russia lipo ASIA

-Food for thought.
 
Back
Top Bottom