Simba iliahirishiwa mechi, kwanini Kitayosce ilazimishwe kucheza pungufu?

Simba iliahirishiwa mechi, kwanini Kitayosce ilazimishwe kucheza pungufu?

Desemba 28, mwaka 2021, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania(TPLB) iliamua kuahirishwa kwa mchezo namba 69 wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Kagera Sugar FC na Simba SC uliokuwa uchezwe siku hiyo Saa 10:00 Alasiri katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, kutokana na taarifa za kitabibu kuwa wachezaji 16 kati ya 22 wa Simba SC waliosafiri kwenda Bukoba kuonekana kuwa na dalili ya mafua na kukohoa hali inayochangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa (Seasonal Influenza).

Simba ingeweza kulazimishwa kuchezesha wachezaji nane, iagize wachezaji wa Under 20, au la ipoteze pointi kwa mujibu wa Kanuni maana kuugua kwa wachezaji wao haikuwa kosa la Kagera kabisa ila Bodi ikatumia 'Busara' mechi ikaahirishwa.

Lakini jana Bodi hiyo ikashindwa kutumia 'Busara' hiyo hiyo kuahirisha mechi ya Azam na Kitayosce kutokana na baadhi ya wachezaji wa Kitayosce kutokidhi vigezo huku wengine, akiwemo golikipa wakiwa ni wagonjwa lakini wakalazimishwa wacheze hivyo hivyo wakiwa nane.

Je, hapa Bodi haikuona haja ya kutumia 'Busara' au inaonea timu ndogo?

Tujadili.
Hii yote kisa mnyama kuchukua ngao?Au Fei kufunga hat trick?
 
Timu za Ligi Kuu zinaruhusiwa kuongeza na kuwatumia wachezaji wa timu za vijana hadi watano, hivyo kama kulikuwa wagonjwa wangeenguliwa wakawekwa vijana.

Rejea andiko la TFF, haukutajwa ni ugonjwa gani sasa wewe unalazimisha iwe ni Covid 19!
ba walilalamika tu wachezaji wetu wagonjwa mida ya saa 8, masaa mawili kabla ya mchezo, ingawa katika pre match walihudhuria vizuri. Kitayose walisema wamekuja na wachezaji wao wote, walipoambiwa wengine hawatocheza, wale wengine pia wakawa hawako vizuri kiafya (wagonjwa kama Simba), mechi haikuahirishwa na wakalazimishwa kucheza hivyo hivyo tena pungufu. Yanga waliwahi kuugua kule Mbeya, mechi haikuahirishwa, kulikoni kwa Simba tu?
Kwani hao wachezaji vijana wangekaa kambi tofauti na wenzao, kiasi kwamba ugonjwa huo usingewahusu!

Lengo la kuahirisha ilikuwa kuepuka kusambaa kwa ugonjwa huo, sio tu kwa wachezaji wa simba, hata Kagera pia.

Kumbuka, wakati huo, tahadhari kubwa ilikuwa kwenye ugonjwa wa Covid19, ambao mpaka sasa tunauita changamoto za upumuaji.

Narudia tena mechi hizi zina maudhui tofauti katika kuahirishwa kwake. Unakuwa mbishi hadi kwenye maswala ya Afya?? aisee ushabiki usikutioe ufahamu

Usiwe mbishi.
 
Kitayose mechi imechezwa sababu walienda uwanjani wakiwa 8

Simba walibaki 6 wazima
 
Ile nafasi ya Kitayose ilikuwa ya PAMBA waache wavune walichopanda

Hujuma dhidi ya PAMBA zilikuwa za wazi na Karia akaziba masikio Sasa aibebe na huku tuone
Hivi mpango wa kubadili jina kuwa Tabora Utd uliishia wapi?
 
Desemba 28, mwaka 2021, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania(TPLB) iliamua kuahirishwa kwa mchezo namba 69 wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Kagera Sugar FC na Simba SC uliokuwa uchezwe siku hiyo Saa 10:00 Alasiri katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, kutokana na taarifa za kitabibu kuwa wachezaji 16 kati ya 22 wa Simba SC waliosafiri kwenda Bukoba kuonekana kuwa na dalili ya mafua na kukohoa hali inayochangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa (Seasonal Influenza).

Simba ingeweza kulazimishwa kuchezesha wachezaji nane, iagize wachezaji wa Under 20, au la ipoteze pointi kwa mujibu wa Kanuni maana kuugua kwa wachezaji wao haikuwa kosa la Kagera kabisa ila Bodi ikatumia 'Busara' mechi ikaahirishwa.

Lakini jana Bodi hiyo ikashindwa kutumia 'Busara' hiyo hiyo kuahirisha mechi ya Azam na Kitayosce kutokana na baadhi ya wachezaji wa Kitayosce kutokidhi vigezo huku wengine, akiwemo golikipa wakiwa ni wagonjwa lakini wakalazimishwa wacheze hivyo hivyo wakiwa nane.

Je, hapa Bodi haikuona haja ya kutumia 'Busara' au inaonea timu ndogo?

Tujadili.
Wananchi twendeni tukakate rufaa CAS. Mbaya zaidi Feitoto amepewa hat-trick, atashirikiana na Simba kutuzodoa
 
Simba ingeweza kulazimishwa kuchezesha wachezaji nane, iagize wachezaji wa Under 20, au la ipoteze pointi kwa mujibu wa Kanuni

1692268359513.png
 
Mnaoleta hoja ya izembe wote hoja yenu haina mashiko, msimu uliyoisha baada ya mapinduzi cup Simba ilienda Dubai na kocha Robertinho, tena katikati ya msimu

Tff ikabidi wabadili ratiba waisogeze mbele maana Simba walikuwa na mchezo wakasema wamekosa usafiri wa kurudi mapema ikabidi wapelekewe mbele mchezo wao Kwa sababu ya upuuzi kabisa,

Kwa upande wangu game ya kitayosce Kwa namna yoyote Ile ilibidi ihairishwe ipangiwe tarehe nyingine

Taarifa Yao tff waliitoa asubuh ya kufungiwa, na baadae wakatoa kuwa wamefunguliwa maana malipo wamefanya?? Kwann wasiwaruhusu wacheze?? View attachment 2720159View attachment 2720160
 
Back
Top Bottom