Simba iliyoibiwa inatafuta mawakili wa kuwatetea Aveva!?

Simba iliyoibiwa inatafuta mawakili wa kuwatetea Aveva!?

Umewahi kumuwekea wakili unayemtuhumu kukuibia? Common let's be logical. Kesi iliyoko mahakamani ni Aveva na Kaburu kuiibia Simba. Kwa mtazamo wangu, Simba walitakiwa waje juu dhidi ya wezi Hawa. Hii ni ajabu nyingine katika soka la TZ
Hauna logic, kwani hao wametuhumiwa na Simba?
 
simba bhana............hahahahaha nacheka kwa dharauuuuuu
Mkuu hizo timu zina siri nyingi, hukumbuki aveva alishaifadhiri simba miaka ya nyuma. Pengine walikua wanaikopesha timu kienyeji na wanajilipa kianyeji.
 
Mkuu hizo timu zina siri nyingi, hukumbuki aveva alishaifadhiri simba miaka ya nyuma. Pengine walikua wanaikopesha timu kienyeji na wanajilipa kianyeji.
Aveva alishaifadhili SSC mwaka gani Mapupu?
 
Aveva alishaifadhili SSC mwaka gani Mapupu?
Usikasirike ndugu.
Kuongoza timu za mpira huku ukiwa masikini ni tabu sana sana sana.
Mara nyingi kunatokeaga ghalama za dharula kama kulipia kambi, au safari za timu au vifaa, madawa na matibabu nk.
Viongozi wanalazimika kukopa pesa hata kwa mtu.
Ona mfano Manji anavyosema anaidai Yanga fc.
Sasa tatizo ni ulipaji wake, kama hiyo pesa ilitolewa kienyeji ni vigumu kuiingiza kwenye vitabu vya ukaguzi.
Hapo ndipo mdai anapolipwa kienyeji, na inaonekana kama pesa imeibiwa.
Simba na Yanga zinahitaji kuingozwa na watu wenye pesa kama
Manji Yanga.
MO Simba.
 
Wezi wafungwe walidhani awamu ya NNE hii...pesa zitawatokea puani umbwa hao
 
Jamani mi nauliza tu
Ivi timu zote za TZ, ni Simba sc pekee yenye hati chafu ?

Nini hasa kimetokea ?
 
Umewahi kumuwekea wakili unayemtuhumu kukuibia? Common let's be logical. Kesi iliyoko mahakamani ni Aveva na Kaburu kuiibia Simba. Kwa mtazamo wangu, Simba walitakiwa waje juu dhidi ya wezi Hawa. Hii ni ajabu nyingine katika soka la TZ
Usishangae mkuu, waweka wakili na wawekewa wakili wote wezi hakuna jipya hapo maana wasipowekewa wakili watatajana mwisho Simba itajikuta haina viongozi wote watakuwa wameungana na akina Aveva
 
Umewahi kumuwekea wakili unayemtuhumu kukuibia? Common let's be logical. Kesi iliyoko mahakamani ni Aveva na Kaburu kuiibia Simba. Kwa mtazamo wangu, Simba walitakiwa waje juu dhidi ya wezi Hawa. Hii ni ajabu nyingine katika soka la TZ
Kwani mlalamikaji ni simba???
 
Usishangae mkuu, waweka wakili na wawekewa wakili wote wezi hakuna jipya hapo maana wasipowekewa wakili watatajana mwisho Simba itajikuta haina viongozi wote watakuwa wameungana na akina Aveva
Hapa nawashangaa wanachama. Walipaswa mpaka Sasa wawawajibishe viongozi waliopo kwa sababu lazima walilifahamu vema hili dili.
 
Nyenyere
Nimekuuliza waliomshtaki ni Simba? Unaleta story za sungusungu, kwani sungu sungu wakimkamata huyo mwizi wanamshtaki wao? , kama mpaka sasa haujui maana ya mtuhumiwa basi tuna tatizo. WanaSimba wanajua why kaburu? Why malinzi? Why now? Na kuna upepo ukipita, utaleta mrejesho.
 
Nimekuuliza waliomshtaki ni Simba? Unaleta story za sungusungu, kwani sungu sungu wakimkamata huyo mwizi wanamshtaki wao? , kama mpaka sasa haujui maana ya mtuhumiwa basi tuna tatizo. WanaSimba wanajua why kaburu? Why malinzi? Why now? Na kuna upepo ukipita, utaleta mrejesho.
Samahani mkuu.
Nauliza tu kwamba.
Ivi timu zote za ligi ya Tanzania, ni timu ya Simba pekee ndo ina matumizi mabaya ya pesa yaliyofanywa na viongozi wake ?

Ivi Simba pekee ndo ina hati chafu katika ukaguzi wa fedha zake ?
Naomba majibu wadau.
Ni kwanini Simba pekee ndo ifuatiliwe.
Ni kweli timu za
Yanga, mbao, ndanda, JKT zote, Majimaji, Prisoni, Kagera, Stendi, Mwadui, Mbeya City, Azamu, A.Lyoni, Mtibwa, nk
Zina hati safi isipokuwa Simba Sports pekee.
Naomba japo wazo la huu uhakiki.
Kuna nini hasa ?
 
Ungekuwa mfuatiliaji wa soka wala usingekuwa na haja ya kuandika upuuzi huu
 
Sijapata kusikia wala kuona, mtu aliyeibiwa kuandaa mawakili wa kumtetea mwizi aliyekuibia....

Sijaelewa sababu za kuwakinga watu walioihujumu team,...

Au itakua mchongo wamehusika wengi?

Hii team inaonekana bila kaburu na Hanspope, hakuna mwenye akili angalau ya kuweza kuwaongoza hawa watu....


Klabu kwa sasa imeandaa jopo la mawakili litakalowatetea viongozi wetu na tunaamini Mahakama itatenda haki pande zote zinazohusika na shauri hilo. Tunawaomba

Watanzania, wapenzi na mashabiki wetu wawe watulivu wakisubiri taarifa rasmi ya kikao cha Kamati ya Utendaji,”imesema taarifa hiyo.

Baada ya kukosekana kwa Aveva na Kaburu, wanaobaki ni Wajumbe wa Kamati ya Utendaji tu, wa kuchaguliwa na kuteuliwa. Wajumbe wa kuchaguliwa ni Collins Frisch, Said Tuliy, Ally Suru, Iddi Kajuna na Jasmine Costa wakati wa kuteuliwa ni Zacharia Hans Poppe, Salim Abdallah ‘Try Again’, Mohammed Nassor, Kassim Dewji, Musley Ruweih.
Aveva na Makamu wake, Kaburu jana walipelekwa mahabusu hadi Julai 13, mwaka huu baada ya kunyimwa dhamana kufuatia kusomewa mashitaka matano Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, Dar es Salaam.

Wawili hao walifikishwa mahakamani mapema asubuhi na kusomewa mashitaka hayo matano mchana, ambayo ni pamoja na kughushi nyaraka zinazodai kuwa klabu ya Simba inawalipa madeni Rais Aveva na Makamu wake, Kaburu kiasi cha dola za Kimarekani 300,000.

Makosa mengine ni Aveva kutoa nyaraka za uongo kwenye benki ya CRDB tawi la Azikiwe mjini Dar es Salaam Machi 10, 2016, la tatu ni kutakatisha fedha kinyume cha sharia, ambapo inadaiwa Rais huyo na Kaburu walikula njama za kufanya uhalifu huo.

Shitaka la nne ni Kaburu kutakatisha fedha dola 300,000 na kuziweka kwenye benki ya Barclays tawi la Mikocheni mjini Dar es Salaam, na la tano ni kutakatisha likimhusu tena, Makamu wa Rais, Kaburu aliyemsadia Aveva kutakatisha fedha katika Barclays baada ya kughushi nyaraka.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo na wakili wa Serikali, Christopher Msigwa, washitakiwa hao walikana mashitaka yote na kupelekwa rumande hadi Julai 13, mwaka huu huku wakinyimwa dhamana.

Wawili hao walipandishwa kizimbani jana baada ya juzi kukamatwa na Maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa uchunguzi juu ya tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutokana na mchezaji Emmanuel Okwi.
Inadaiwa kuna ‘ufisadi’katika mauzo ya mchezaji Emmanuel Okwi kwenda klabu ya Esperance ya Tunisia dili ambalo liliripotiwa kugharimu dola za Kimarekani 300,000, zaidi ya Sh. Milioni 600 za Tanzania.

Lakini Aveva hakuwapo madarakani wakati Simba inamuuza Okwi mwaka 2013, bali Kaburu alikuwa Makamu wa Rais, chini ya Rais wa wakati huo, Alhaj Ismail Aden Rage.
Hata hivyo, Esperance ilichelewa kulipa fedha hizo na hadi Machi mwaka jana, wakati huo tayari Aveva ni Rais wa klabu na Kaburu ni Makamu wake, baada ya Rage kutogombea tena.

Okwi alinunuliwa na Etoile Januari mwaka 2013, miaka mitatu tu baada ya kujiunga na Simba mwaka 2010, lakini baada ya miezi mitatu akatofautiana na klabu ya Tunisia kufuatia na kufungua kesi FIFA akiomba aruhusiwe kucheza klabu nyingine kulinda kipaji chake wakati mgogoro wake na Etoile unaendelea.

Etoile ilisitisha huduma kwa Okwi, baada ya kukerwa na desturi ya mchezaji huyo kuchelewa kurejea kujiunga na timu kila alipokuwa anaporuhusiwa kwenda kujiunga na timu yake ya taifa Uganda.

Akasaini tena SC Villa katikati ya mwaka 2013 kabla ya Desemba mwaka huo, kuhamia Yanga SC- wakati wote huo kesi yake na Etoile ikiendelea FIFA na Simba walikuwa hawajalipwa fedha zao.
Simba nayo ilifungua kesi FIFA ikisistiza kulipwa fedha zake baada ya kumuuza mchezaji huyo Etoile Januari 2013.

Okwi na Simba wakaungana tena mwaka 2014 baada ya mchezaji huyo kutofautiana na Yanga pia, akidai ilishindwa kummalizia fedha zake za usajili, hivyo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumruhusu kuondoka, naye akarejea Msimbazi.

Kabla haijapata fedha za kumuuza Okwi Etoile, Simba ikamuuza tena Okwi klabu ya Sonderjyske ya Denmark kwa dau la dola za Kimarekani 110,000 zaidi ya Sh. Milioni 230 za Tanzania.

Hata hivyo, Denmark nako aliposaini mkataba wa miaka mitano, aliondoka baada ya miaka miwili tu na kurejea SC Villa mapema mwaka huu, kabla ya juzi kusaini mkataba wa miaka miwili kujiunga tena na Simba kwa mara ya tatu...
Mashitaka yote hayo yanahusu pesa za okwi alipouzwa uarabuni na ufafanuzi ulishatoka zamani sana, sisi watu wa soka tunaelewa kwanini ikawa vile na mpaka leo kinachotokea.
 
7778a553fed17e67089c9b9e3cba6b97.jpg
Tatizo kubwa la watu walioko madarakani kwenye hizi klabu zetu ni watu wa kupachikwa. Hata kutambua kwamba kesi ya mtu binasi haihusiani na masuala ya klabu inakuwa vigumu. Hapa wanataka kutuaminisha kwamba hawa mabwana wameonewa kumbe ni wahalifu.

Hili jambo la fedha za Okwi Rage aliwatahadharisha sana viongozi wa Simba wawe waangalifu. Niwaombe wapenzi wa Simba wawe watulivu na waziache mamlaka za kisheria zifanye kazi yake kwa uadilifu bila mashinikizo. Wasitake kuihusisha klabu ya Simba na uhalifu
 
Simba waunganishwe kwenye kesi wote wezi
Eliimu elimu kitu kizuri wangekaa kimya
 
Back
Top Bottom