Simba imechezea shilingi Chooni Msimu huu hamna cha kufa kiume pale

Simba imechezea shilingi Chooni Msimu huu hamna cha kufa kiume pale

themagnificient

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2016
Posts
1,033
Reaction score
3,720
Nimekuwa nikiishabikia simba kwa Vitendo mechi zote za CAF na zile baadhi ya ligi nimekuwa nikienda Taifa kuisuport timu yangu ila niseme tu ukweli kati ya Robo fainali zote Simba ilizoingia kwenye Michuano ya CAF basi hii ndio ilikuwa Neema kwa simba kutinga Nusu fainali Yaani Simba tulipata bahati ya Mtende pale Taifa na Tukashindwa kuitumia

Kama simba ingekuwa Makini Mechi ilikuwa inaisha hapa hapa Taifa yaani ile mechi ya kwanza kama Safu ya ushambuliaji ya Simba wangekuwa makini na tungekuwa na watu wenye uwezo basi Waidad alikuwa anakula Goli 3 hadi 4 Pale Taifa yaani kule kwao tungekuwa tunatafuta Sare tu au kushinda au kufungwa Goli moja na kweli Wydad ya sasa kama mlivyoiona majamaa hawana kitu na mkitaka kuamini muangalieni Mamelodi atakavyoenda kuuwa mtu nusufainali ndio Mtajua wydad ya sasa hamna kitu pale

Ushauri wangu Club iache Ubahili,Maswala ya kuokota Wazee wanaomaliza mikataba washafikisha mika 38 hadi 40 timu ibadilike , Mpira wa Sasa ni pesa huwezi pata vijana Damu Changa wanaolijua soka kwa kuendekeza Ubahili, Mtu kama Mzee Saido ndio kocha anamtegemea kwenye mechi kubwa kama ile kwa Dakika 90, Mtu kama Mzee Onyango angalia mechi zilizopita alivyochomesha magoli ya wazi.

Msimu ujao kama timu itaendekeza tamaduni za kuendekeza wazee na kuleta ubahili kwenye Usajili nawahakikishia tutashia kwenye mtoano
 
Wajifunze kushinda mechi za ugenini kwa sababu ukishinda tu kwa mkapa halafu fainali ichezewe sehemu nyingine hilo kombe utashindaje?

Mistake ya kwanza ni kuwa na mentality ya kwa mkapa hatoki mtu bila kuwaza kuwa hakuna finali yoyote imewahi pangwa kuchezewa hapo kwa mkapa.

BADILIKENI
 
Back
Top Bottom