SI KWELI Simba imefungwa goli 6 na timu ya daraja la pili Misri kwenye Pre season ya 2024/25

SI KWELI Simba imefungwa goli 6 na timu ya daraja la pili Misri kwenye Pre season ya 2024/25

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
IMG_20240716_122258.jpg


Klabu ya Simba ambayo ipo nchini Misri katika maandalizi ya msimu mpya 2024/25, leo Julai 14, 2024 imecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Tersana FC inayoshiriki ligi daraja la pili Misri na kuambulia kichapo cha goli 6-2.

Mchezo huo ambao ulikuwa na lengo la kujaribu kikosi chao, Wanalunyasi walijikuta wakipokea kichapo hicho cha goli 6-2 baada ya kiungo wao Debora kupata kadi nyekundu dakika ya 36 huku matokeo yakiwa 2-1.

Magoli mawili ya Simba katika mchezo huo yalifungwa na mshambuliaji raia wa Zambia Fred Koblain dakika ya 32 na Kiungo wao mpya Yusufu Kagoma dakika ya 61.

Magoli 6 ya Tersana yalifungwa dakika za 12, 26, 41, 54,67 na 76.

Mara baada ya mchezo huo makocha wa Simba waligoma kuongelea matokeo hayo kwani ni sehemu ya mazoezi ya kikosi hicho. Kocha wa timu ya Tersana alisema kikosi Cha Simba bado hawana maelewano na baadhi ni wachezaji wa viwango vya kawaida.

 
Tunachokijua
Julai 14, 2024 ilianza kusambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii ikidai timu ya Simba iliyopo Ismailia Misri kwa maandalizi ya msimu mpya wa ligi ya 2024/25 imecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Tersana FC inayoshiriki ligi daraja la pili Misri na kuambulia kichapo cha goli 6-2.

Aidha, taarifa hii inadai magoli ya Simba yalifungwa na mshambuliaji wao Freddy Kouablan na Yusuph Kagoma, pia makocha wa Simba waligoma kuzungumza chochote baada ya mechi hii.

Rejea hapa, hapa, hapa na hapa ili kuona baadhi ya akaunti zilizochapisha madai haya.

Ukweli wa madai upoje?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini madai haya hayana ukweli. Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally ameiambia JamiiCheck kuwa "Siyo taarifa ya kweli ni uzushi, jana (Julai 15, 2024) ndio timu imefanya mazoezi ya kucheza mechi ya wenyewe kwa wenyewe, baadhi ya Wachezaji walivaa jezi nyekundu wengine nyeupe.”

Kupitia ufuatiliaji wake wa kutumia nyenzo wazi za utafutaji wa kimtandao, JamiiCheck imebaini kuwa taarifa za uwepo wa mchezo husika hazijachapishwa kwenye kurasa rasmi za Simba SC na Tersana FC hivyo kuongeza mashaka ya usahihi wake.

Aidha, Julai 10, 2024, Akaunti nyingine ya Mtandao wa YouTube ilichapisha taarifa inayodai Simba ilicheza mchezo wa kwanza kwa kirafiki dhidi ya Al Ittihad na kuipa kichapo kikali cha magoli 6-1 ambapo wachezaji wake wapya Joshua Mutale na Steven Mukwara wakifunga magoli matatu kila mmoja.

Hii inaonesha kuwa zipo taarifa nyingi siziso za kweli zinazozushwa kwenye kipindi cha usajili na maandalizi ya msimu mpya wa ligi zikihusisha timu kubwa kote duniani.
Back
Top Bottom