Simba imeridhika na kuhadaika na historia, Yanga ikiwa na kiu ya mafanikio na kutengeneza historia

Simba imeridhika na kuhadaika na historia, Yanga ikiwa na kiu ya mafanikio na kutengeneza historia

Pesanyingi

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2023
Posts
1,157
Reaction score
1,983
Kwanza hongereni timu ya wananchi.

Hakika mmeonyesha kile ambacho mashabiki zenu walikuwa wakitegemea na kazi bora ya viongozi chini ya Hersi.

Tofauti yenu na Simba kwasasa ni kubwa hilo halina ubishi, mmekuwa ni timu ya kiushindani, kujituma, kujitoa, kucheza kitimu pamoja na nidhamu ya wachezaji.

Kwa miaka ya karibuni mmeshaweka alama yenu kwenye mashindano ya Africa kuanzia kombe la shirikisho hadi club bigwa mmeiheshimisha soka letu.

Mnauwezo wa kupambana na timu yoyote Afrika kwa ubora mlio nao sasa.

Sisi makolo bado tunaamini ni timu kubwa kwa nadharia ila kivitendo kwa Sasa hamna kitu, wachezaji wazito kama hakuna kocha wa viungo, wavivu, wachoyo rejea babu yetu Saido n.k.

Hongereni naona mkifika mbali kwa hali mliyokuwa nayo ya mafanikio.
 
Jamani kila nikitaka kulala mnapandisha threads mpya halafu nzuri nzuri.

Hii iwe ya mwisho sasa, tutajadili kesho Insha’Allah.
Na, Asante Mkuu.
unalalaje mapema weekend hii,bado na ushindi mnono mmeupata ndio kabisa akuna kulala.
amka dadangu nikupe siri moja kubwa sana kuhusu ushindi wa Yanga leo hii.
 
Yanga ya sasa hata ikifugwa wala shabiki halalamiki kwani unaona wanavyojituma tofauti na Simba ikipata goli moja wanaanza show za kitoto.Na sijuwi Yanga wanatowaga wapi makocha wao,alafu Simba tunakwama.
 
Hili tuliliongea kitambo, na tuliliona kitambo, viongozi wasimba ndio wachawi namba 1.
Na kwenye uwanja wa mazowezi inavyoonekana Simba wanamuda mwingi wa kucheka cheka na kujirikodi video wakikata mauno badala ya kuwa serious.
 
Majini Sports Club wanaupiga mwingi
Hongereni watani,maisha ni kupambana tu
Lengo la Klabu yoyote ni kufika juu hivi unadhani
maji maji na Lipuli wanapenda wawe pale? hapana ni hesabu tu zimekataa!
🤔🤔
 
Ni mtazamo tu
Chelsea alibeba UEFA mbele ya Bayern si kwa kuwa Bayern na Barcelona zilikuwa zimeridhika no , ni mpira uliamua iwe hivyo kwa wakati husika tu ,hata hawa Yanga hawatoperform kila siku namna hii na mtakuja kuongea mengi baadae
 
Mimi ni Simba lakini bado naendelea kukumbuka kauli ambayo ilishayolewa na mdau mmoja kuwa kama ipo timu itakayoleta kombe la champions Tanzania basi ya kwanza itakuwa Yanga. Itapita miaka na miaka lakini I believe Yanga ndio itakuwa ya kwanza kama wakiendelea na mipango Yao ya sasa. Simba tujitazame hata ligi kuu Yanga anaweza kuchukua kombe zaidi ya mara Tano. Usije na jaziba kinijibu ila tumia akili utanielewa
 
Ni mtazamo tu
Chelsea alibeba UEFA mbele ya Bayern si kwa kuwa Bayern na Barcelona zilikuwa zimeridhika no , ni mpira uliamua iwe hivyo kwa wakati husika tu ,hata hawa Yanga hawatoperform kila siku namna hii na mtakuja kuongea mengi baadae
Leo ndio mmejua haya? Siku zote hua mnaiponda Yanga akili zinakuaga wapi?
 
Back
Top Bottom