Mlachake
JF-Expert Member
- Oct 13, 2009
- 4,437
- 4,618
Kilichotuangusha Yanga ni Red Card. Laiti kama ile card isingekuwepo palikuwepo uwezekano mkubwa wa Yanga kuibuka washindi
Hebu fikiria kwa dakika 40+ Yanga imecheza wakiwa pungufu ya mtu mmoja lakini Simba kwa muda wote huo wameshindwa kabisa kuziona nyavu pamoja kuwa na wachezaji wao ambao wenyewe wanawaamini kupitiliza katika kutupia, Chama, Miquessone na Mugalu.
Sasa utajiuliza je Wananchi wangekua wametimia matokeo yangesema nini?
Yanga tusife moyo uwanjani tulikua bora,goli tulilofungwa yawezekana kabisa jua lililokua likipiga upande ule lilichangia sana kwa kipa na mabeki kutouona mpira vizuri ikumbukwe hata kipindi cha kwanza kona walizokua wakipiga Yanga upande ule jua liliwasumbua sana hasa Aishi Manula na Mabeki
Ýanga tusife moyo hakika tulikua bora zaidi yao uwanjani, hakika hawa siku zao zinahesabika wacha tushushe vifaa vya uhakika wakiweno Heritier Makambo, Fistoo Mayele na Shabaan Djumaa.
Mkuu Mpira haupo hivyo. Unakumbuka kuna mechi simba alipata kadi nyekundu kipindi cha kwanza huku yanga anaongoza goli moja lakini Simba ikaishia kushinda mbili kwa moja pamoja na kuwa pungufu.
Team iliyopungufu huwa inacheza kwa tahadhari na kushtukiza na Jana kama Yacouba angetlia na ile chance nisngee shanga yanga kushinda ile game.
Team ikiwa pungufu inazuia sana na kutafuta nafasi za kushtukiza ambazo ni hatari sana.