- Source #1
- View Source #1
- Tunachokijua
- Murtaza Mangungu alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba February 2021 baada ya kuwashinda mpinzani wake Juma Nkamia.
Madai
Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii Juni 3, 2025 imezuka taarifa ikiwa na nembo ya klabu ya Simba ikieleza kuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo Murtaza Mangungu amejiuzulu na hivyo bodi ya wakurugenzi inathibitisha kupokea barua yake
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia taarifa hiyo na kujirishisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
Ufuatiliaji zaidi umebaini kuwa taarifa hiyo ni ya kughushi na haijatolewa na klabu ya Simba. Taarifa hiyo pia ina mapungufu kadhaa na hivyo kuthibitisha kuwa ni ya kughushi mathalani aia ya mwandiko uliotumia (fonts) ni tofauti na mwandiko amabo umekuwa ukitumika katika taarifa nyingine zilizowahi kutolewa na Simba.
Aidha taarifa hiyo haipo katika kurasa rasmi za mitandao ya kijamii yaklabu ya Simba. JamiiCheck imemtafuta Meneja mawasiliano na habri wa klabu ya Simba Ahmedy Ali ambaye pia amethibitisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
"Hiyo ni barua feki, Klabu ya Simba haijatoa taarifa ya aina hiyo."