SI KWELI Simba imetoa taarifa kwa umma kuomba radhi mashabiki wake kushindwa kuvumilia utani wa Yanga SC

SI KWELI Simba imetoa taarifa kwa umma kuomba radhi mashabiki wake kushindwa kuvumilia utani wa Yanga SC

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
SIMBASCSEPT162025.jpg
 
Tunachokijua
Septemba 16, 2025 ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2025/2026 inatarajiwa kufunguliwa kupitia mchezo wa ngao ya jamii utakaowakutanisha watani wa jadi Yanga SC na Simba SC zote kutoka Dar es salaam. Kila mechi inayowakutanisha wababe hao wa soka kutoka Tanzania imekua ikiambatana na utani, mizaha kwa pande zote mbili jambo ambalo limekuwa likichochea hamasa na kuwavutia wengi pindi timu hizo zinapokutana.

Sasa ipo taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii, ikidaiwa kuwa ni taarifa kwa umma iliyotolewa na timu ya Simba kuelekea mechezo wa Septemba 16, kuomba radhi mashabiki wake kushindwa kuvumilia utani wa Yanga SC.

"Klabu ya Simba SC inapenda kutoa taarifa kwa Umma kuwa inaomba radhi kwa moshabiki wake wote kwa kushindwa kuvumilia utani umbaõ Klabu ya Yanga imekuwa ikifinaya kuelekea michezo yetu.

Kupitia barua hii, Simba SC inaomba Klabu ya Yanga kusitisha utani huu kwani hauna afya kwa maendeleo ya soka letu."

Je, ni kweli taarifa hiyo imetolewa na Simba SC?


JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli. Kupitia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) imebainika kuwa haijatolewa na Simba SC, kwani kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii hazijachapisha taarifa hiyo.

Aidha yapo baadhi ya mapungufu katika barua hiyo yanayoashiria kuwa imeghushiwa na wapotoshaji. Mpangilio mzima haufanani naule unaotumika katika taarifa rasmi za Simba SC, Matumizi ya nembo isiyo ya Smba SC, makosa ya kisarufi, kukosewa kwa baadhi ya maneno, kutokuwekwa bayana kwa tarehe iliyotolewa na kadhalika.

Rejea hapa taarifa rasmi ya Simba SC.​
Taarifa hii haijachapishwa na ukurasa wowote wa simba sports club iwe kwenye ukurasa wa facebook, Instagram ,na twitter zamani X hivyo imetengenezwa kwa ajili ya kusambaza taarifa potofu dhidi ya klabu ya simba sports club.

Uthibitishaji unaonesha kuwa taarifa hiyo sio sahihi kwa kuzingatia kuwa taarifa mda inachapishwa haikuwa na nembo rasmi ya taasisi ya simba na haikuwa na tarehe ambayo taarifa hiyo imechapishwa na haikuwa na jina la kiongozi ambaye ameidhinisha taarifa hiyo kufikia umma

Pia taarifa jiyo inakosa makossa mengi ya kimaandishi kwa mfano katika aya ya kwanza ya taarifa hiyi iankukuu kuwa ’’klabu ya simba inapenda kutoa taarifa kwa umma kuwa inaomba radhi kwa moshabiki wote kwa kushindwa kuvumilia utani ambao klabu ya yanga imekuwa ikifinaya kuelekea michezo yetu ’’

Kwenye nukuu hiyo kuna makosa kama ikifinaya na moshiba jambo ambalo inathibitisha kuwa taarifa hiyo haijachapishwa na simba sports club
Licha ya hivyo aina ya fonts (ambayo imetumika kwenye taarifa kwenda kwa umma ni tofauti na fonts ambazo huwa zinatumiwa na klabu ya simba kwenye uwasilishaji wa taarifa kwa umma )

Pia kwa kutumia ufuatiliaji inaonesha kuwa nembo ya simba haipo sehemu maalumu ambayo huwa inawekwa hivyo kuthibitisha uhalali wa taaarifa potofu kwa wananchi
 
Back
Top Bottom