Simba imgeukie Masoud Djuma

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Simba msimu huu ina kikosi kizuri (sio kipana) kuliko ilivyowahi kutokea misimu mingi sana iliyopita. Lakini Simba ya msimu huu ni mbovu sana kuliko Simba ya misimu mingi iliyopita. Hii inakatisha tamaa wale waliowekeza pesa zao Simba na wanachama na mashabiki wa Simba wanaoisifia Sana timu Yao kutokana na uwekezaji na aina ya wachezaji waliosajiliwa.

Simba ya mbelgiji imefungwa kwa aibu na timu ambazo ni under dog sawa na pombe ya ngomani kila mtu anajichotea tyuu na kunywa. Miaka ilipota kabla Simba kufungwa 5-0.

Masoud Djuma ukimpatia kikosi kizuri kama hiki cha Simba angefanya makubwa haki ya nani. Simba itajilaumu kuchelewa kumtimua Aussens.
 
Timu ya hovyo hii kila siku Manara anapiga tarumbeta la kusifia wachezaji wa Simba kuwa wana uwezo wa kuamua matokeo.

Wachezaji gani kwa mfano? Bora useme KMC wana kikosi kipana ila siyo genge la wavaa njumu la Simba.
 
Zinafungwa Barcelona, Madrid, Man City, Psg tena na timu ndogo tu. Mkuu Manara uwe unampuuza vinginevyo utaamini kweli Simba ni zaidi ya hizo timu nilizotaja.
Yule msemaji domo limezidi sana. Anaichora Simba kwneye level za kimataifa wakati hata mashindano ya kitaifa tunakosa uhakika wa kupata ushindi.
 
Leo watu mmewashwa kweli kufungwa kwa Simba. Inaonyesha dhahiri kuwa ndio kidume chenu maana mti wenye matunda ndio hupigwa mawe.

Ulishaona mgunga (yanga) ukipigwa mawe? Nani anakula miba?
 
Masudi Djuma ungejua sababu aliyoondolewa Simba, usingekaa kuandika haya.

Mfaransa yule aliyeipa ubingwa kaondoka kisa figisu zake za kuutaka ukocha mkuu kilazima. Hadi huyu mbelgiji hawakuwa wakiiva akasema hamtaki awe msaidizi wake, ndiyo maana Simba kipindi ligi inaanza ilisuasua kisa mgogoro huo.

Alishaanza kuwamezesha wachezaji sumu ilimradi kocha aonekane siyo atimuliwe, sasa timu ikamwondoa ili yasije madhara zaidi akaigawa timu kisa ukocha mkuu.

Mechi alizokabidhiwa kama kocha mkuu, alifungwa zote tena ni muhimu mno timu ikiwa hatua ya fainali michuano mbalimbali.

Kiufupi Masudi hajafikia hadhi ya kuwa kocha mkuu, yule ni mfitini mzuri ila si kocha mzuri
 
Timu ya hovyo hii kila siku Manara anapiga tarumbeta la kusifia wachezaji wa Simba kuwa wana uwezo wa kuamua matokeo.

Wachezaji gani kwa mfano? Bora useme KMC wana kikosi kipana ila siyo genge la wavaa njumu la Simba.
Mtu wa Kwanza wa kufukuza Simba ni Haji Manara. Huyu anasababisha wachezaji kucheza Kwa hofu kubwa kutokana na Manara kuwakweza Sana Kwa mashabiki, viongozi wa nchi na jamiikwa jumla. Hivyo wachezaji wanaingia uwanjani na hofu kubwa ya kuhofiia Yanga hata kama wanacheza na timu nyingine isiyo Yanga. lakini wanahofia pia kumuangusha Manara, Mo, viongozi wa 'tff' hasa rais wa tff na viongozi wengine ambao wanashirikishwa Sana na Manara kwenye mambo ya Simba.

Djuma alikuwa anammudu Manara kwakuwa alikuwa kama msemaji mwingine wa club na wachezaji kuliko mbelgiji. Djuma ni kijana kama kama wachezaji, Zahera, ole sosjure, Emery, Zidane, Henry, Ben Mwalala. Wazee kama mholanzi wa Azam na mbelgiji wa Simba hawatafua dafu nakwambia.
 
Leo watu mmewashwa kweli kufungwa kwa Simba. Inaonyesha dhahiri kuwa ndio kidume chenu maana mti wenye matunda ndio hupigwa mawe.

Ulishaona mgunga (yanga) ukipigwa mawe? Nani anakula miba?
Haji inaiponza Simba, Aussens hana uwezo wa kufundisha wachezaji wazembe kama mkude, kichuya, nk. Yeye labda apatiwe wachezaji professional wasiohitaji kufundishwa namna ya kutuliza mpira na kutoa pasi kama hawa wakwetu wanapohitaji kufanyiwa majaribio kwanza kabla ya kusajiliwa.
Wachezaji wengi pale Simba wapo kwaajili ya maslahi lakini hawaipendi timu kabisa. Wachezaji kama niyonzima, Okwi, ndemla, mo Ibrahim, chama, Wawa, Bocco ni hela Tu sio mapenzi.
 
aaaah, kama wachezaji waliweza kuelewana hadi kumsikiliza na kufuata anachosema Djuma basi Djuma ndiye kocha anayefaa. Hata Moirhino na Aserne Wenger walikuwa makocha wazuri lakini wachezaji walikuwa hawaelewani kuliko sasa Ole na Emery na timu zinafanya vizuri.

Yanga inafanya vizuri kwakuwa wachezaji na mwalimu ni kitu kimoja
 
Utakuwa uongo, Masoud amekuwa msaidizi tangu aingie Simba
Yeye kudai kuwa kocha mkuu si kosa kwanza alitakiwa awe kocha mkuu na Aussien awe msaidizi kwa viwango vyao vya ufundishaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vyovyote iwavyo lakini ukweli kiwango kinachooneshwa na timu yetu hakiridhishi kama kuna tatizo lolote ambalo lipo ndani ya uwezo wao viongozi walishughulikie mapema kabla mambo hayajaharibika zaidi,mashabiki tunaumizwa kwa mwenendo wa timu yetu
Ondoa kocha huyo anafundisha 'pedestrian' football ambalo lilizitoa Brazil, Spain kwenye ubingwa wa kombe la dunia. Kwenye ligi ya bongo ukicheza mpira slow vile utapata sare nyingi sana na ikitokea umefungwa hutarudisha goli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, huu utafiti umeufanyia wapi na kwa namna ipi? Yaani makelele ya Manara yawatie hofu wachezaji wa timu yake? Wakati mwingine ni bora kukaa kimya
 
Yule msemaji domo limezidi sana. Anaichora Simba kwneye level za kimataifa wakati hata mashindano ya kitaifa tunakosa uhakika wa kupata ushindi.
Hivi mnaweza kuonyesha uhusiano uliopo kati ya kelele za Manara na matokeo ya Simba? Yule anahamasisha watu wajaze uwanja, na pengine amefanikiwa sana. Kazi ya kocha na wachezaji haziathiriwi moja kwa moja na kelele zake. Hivi ndio kusema bila Haji Manara kuongea, Simba ingezifunga timu ngumu kama mabingwa wa DRC AS Vita? Kama TP Mazembe habebi ubingwa mbele ya Vita, ajabu ipi Simba kufungwa? Simba kuifunga Nkana na kuiondoa mashindanoni, unaona ni kitu cha kawaida tu?
 
Utakuwa uongo, Masoud amekuwa msaidizi tangu aingie Simba
Yeye kudai kuwa kocha mkuu si kosa kwanza alitakiwa awe kocha mkuu na Aussien awe msaidizi kwa viwango vyao vya ufundishaji

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa uliza uambiwe, makocha kuanzia Omog hadi huyu wa sasa hakuna alowahi elewana na huyo jamaa hadi akawa anawagawa na wachezaji.

Aussien tu ndiyo kabaki ila wengie waliamua kuondoka kisa yeye. Simba ilipitia kipindi kigumu kisa huyo, kila mechi aliyopewa aongoze kaboronga.
 
Hebu ongea unachokifahamu vingine acha, tu, mpaka kuondolewa ilibidi
 
Anaongea ujinga, kelele zisizo na maana ni ujinga.
 
Kweli hii
 

Attachments

  • IMG-20190126-WA0008.jpg
    49.8 KB · Views: 23
Tuweke records sawa, Masoud hakumkuta Omog Simba. Hapo ndipo wenye uongo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa post utakuwa mwana Jangwani unataka kuleta migogoro kwa timu,niambie masudi wako alichukua kombe lipi baada ya kupewa timu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…