Simba ina waganga wengi wa kienyeji kuliko idadi ya wataalamu waliopo benchi la ufundi

Simba ina waganga wengi wa kienyeji kuliko idadi ya wataalamu waliopo benchi la ufundi

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
MTANDAO huu kwa muda mrefu sasa umekuwa ukifanya tafiti na kufuatilia mwenendo wa klabu ya Simba katika mechi za ligi kuu soka Tanzania bara msimu huu.

Mwishoni mwa juma lililopita, Simba ilifungwa magoli 2-0 na Mbeya City fc katika uwanja wa Sokoine, Mbeya na kuifanya klabu hiyo kongwe nchini kuendelea kukaa nafasi ya tatu kwa pointi 35 walizokusanya baada ya kushuka dimbani mara 22.

Machi 18 mwaka huu walifungwa magoli 2-0 na Mgambo JKT katika uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga, lakini wakashinda 2-1 ugenini dhidi ya Kagera Sugar uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga na ilikuwa aprili 6 mwaka huu (jumatatu ya pasaka).

Katika mechi hizo tatu, mtandao huu ulikuwa unachunguza mwenendo wa Simba na namna wanavyoiandaa timu kwa ajili ya mechi.

Katika mechi ya Tanga waliyochapwa na Mgambo, timu iligoma kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, wachezaji wakakaguliwa ndani ya basi nje ya geti karibu na vyumba vya kubadilishia nguo.

Simba walifanya hivyo wakihofia kurogwa na wenyeji wao, lakini mwisho wa siku wakafa mbili bila na walipoenda Shinyanga kucheza na Kagera walifanya hivyo hivyo, walikataa kuingia vyumbani na kukubali kutozwa faini na TFF.

Simba waliendeleza tabia yao ya kutoingia vyumbani kwa madai ya kuogopa kurogwa huku wakisingizia vyumba ni vibovu. Inawezekana kweli ni vibovu, lakini dhahiri walikuwa na mawazo mengine kichwani mwao kwani viongozi walionekana kuwapangia wachezaji maeneo ya kupita wakati wanaingia uwanjani.



Baada ya safari ndefu ya uchunguzi, hatimaye jibu limepatikana kule Mbeya ambako Simba amekufa tena mbele ya Wagonga nyundo wa Mbeya, Mbeya City fc.

Tulipiga kambi jijini Mbeya na kugundua kuwa Simba wameharibikiwa kwasababu wanawatumia Waganga wa kienyeji kwa muda mwingi wakiamini watawasaidia kupata matokeo ndani ya uwanja.

Dunia ya leo klabu kongwe ya Simba, mfano wa kuigwa inaendekeza imani za kishirikina kwa kiwango cha juu namna hii, inasikitisha sana.

Chakusikitisha zaidi ni kwamba, tunaamini viongozi waliopo madarakani ni vijana wa kidijitali yaani wa kisasa au kileo. Imefika wakati tunaamini wazee kama vile Hassan Dalali na wengineo hizi si zama zao, lakini hayo ni maneno tu, inawezekana wale wazee wakawa na mafanikio makubwa kuliko vijana ambao tunaamini wanaweza kuiendesha timu kileo au kisasa, vijana ambao ukiwaangalia ni watanashati, lakini matendo wanayoifanyia klabu ni mabaya mno.

Kwa aina ya viongozi wa sasa wa Simba, ni jambo la aibu kutumia muda mwingi kuwekeza katika uchawi , kutumia waganga au ndumba wakiamini watasaidia kupata matokeo kuliko kujikita katika maandalizi ya kitaalamu na kiuweledi.

Simba wamefungwa na Mbeya City kwasababu hawakutoa nafasi ya kiuweledi katika maandalizi yao, waliwekeza nguvu kwa mambo ya nje ya uwanja wakiamini yatawasaidia kupata matokeo.

Utaratibu ulivyo, unapoenda uwanja wa ugenini, siku moja kabla ya mechi, timu inatakiwa kufanya mazoezi kwenye uwanja ambao watachezea mchezo, kwahiyo Simba walitakiwa kwenda kufanya mazoezi Sokoine siku ya ijumaa, lakini kutokana na kuamini mambo ya kishirikina hawakwenda kufanya mazoezi siku hiyo, matokeo yake ilibidi wafanye mazoezi kwenye bustani (Garden) ya Hoteli waliyofikia, wanafanyia mazoezi ‘Garden' eti kwa sababu wanaogopa kurogwa na Mbeya City.

Hii ilikuwa kinyume, mwalimu na benchi la ufundi walitaka timu ikafanye mazoezi uwanjani, lakini baadhi ya viongozi walioandama na timu waliona timu ikienda kufanya mazoezi Sokoine wataenda kupoteza mchezo wa jumamosi.

Mwisho wa siku wakafanya mazoezi uani, wakafanya mazoezi ‘Garden', na wakawa ‘wamefeli' rasmi.

Ikaja siku ya mechi, badala ya kupita kwenye mlango wa kawaida wakapitia mlango wa nyuma, wachezaji wakashuka na kuingilia mlango wa nyuma, wakashindwa kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, wakakaa pembeni kwenye kona kulia kwa jukwaa kuu la Sokoine, sehemu ambayo maaskari Polisi wanapenda kuweka magari yao.

Baadaye kidogo wakaenda karibu na sehemu ya vyumba vya kubadilishia nguo na kukaa nje upande wa kulia kwenye chumba chao , lakini wachezaji wakaamuriwa waondoke tena.

Muda huo wachezaji wa Mbeya City walikuwa wanapasha moto misuli ‘Warm-up) na walikuwa wameshafanya kwa muda mrefu, Simba wao walichelewa hata kupasha moto misuli kutokana na mambo yao ya kishirikina.

Wakati wanaingia kwenye ‘Warm-up' badala ya kuingilia kwenye benchi ambalo watakaa upande wa kushoto kwasababu kulia walikuwa wamekaa Mbeya City kinyume na taratibu zinazowataka wenyeji kukaa benchi la kushoto na wageni kulia, Simba wakarudi kwenye kona waliyoingilia mara ya kwanza

Simba walifuata taratibu kwamba wenyeji wanakaa benchi la kushoto, wageni kulia, lakini kulia ni sehemu ambayo Mbeya City wanakaa kila siku na Simba walikataa kukaa kushoto wakiamini pameshapigwa misumari. Walipotaka kukaa kulia Mbeya City wakagoma na ndipo ikatokea vurumai kati ya watu wa Mbeya City na Simba, ikabidi Simba wawe wapole na kukubali kukaa kushoto.

Wakati huo wachezaji walikuwa wamekaa chini nyuma ya lile benchi la ufundi na ilibidi wakafanye ‘warm-up', kwa itikadi hizo hizo za kishirikiana wakashindwa kuingia uwanjani kupitia eneo hilo, wakaambiwa watembee na kurudi goli la kusini wazunguke kwenye kibendera cha kona na waingie uwanjani na mstari ule wakafanye ‘warm-up'.

Ukiangalia kwa undani, wachezaji hawataki mambo hayo, wanakasirika, wanaingia uwanjani hawana raha, lakini kwasababu wamelazimishwa na wapambe wanaojifanya wanajua kila kitu, timu iingilie wapi, wakanyage wapi na kamwe hawataki kukiuka maigizo ya waganda wa kienyeji.



Siku ya mechi hakika wachezaji hawakuwa sawa kisaikolojia, waliingia kupasha misuli na kuanza mechi, wakati wanacheza Mbeya City waliwazidi Simba, walikuwa wamechangamka, walionesha kabisa wanahitaji matokeo, lakini Simba walikuwa wanacheza tu kama vile mtu anayetaka kutekeleza jukumu lake na kuondoka.

Jonas Mkude, Abdi Hassan Banda, Said Ndemla wakawa wanazunguka tu, wanageuka nyuma na mipira, hawaoneshi nia ya kwenda mbele, Elius Maguli, Ibrahim Hajibu wakaonekana vimeo kwasababu walikuwa hawapati huduma kutoka kwa viungo.

Mbeya City walicheza vizuri sana ukiachana na mambo ya kupiga misumari kwa wale wanaoamini hivyo, lakini kwasisi ambao hatuamini hivyo, tukiamini kuwa maandalizi ya mechi ni mazoezi, Mbeya City walicheza zaidi ya Simba, walitengeneza nafasi nyingi na kilichosababisha Simba washindwe kucheza ni imani za kishirikina.

Kuna baadhi ya wachezaji ambao sitaki kuwataja hawafurahishwi na vitendo vya kuendekeza vitendo vya kishirikina, walienda Tanga kuchuana na Mgambo, kuna mtu mmoja wa kamati ya utendaji (jina tunalo) anapenda sana mambo ya kishirikina, alienda na waganga karibia nane (8) Mkwakwani, wakapigwa 2-0 na Mgambo.

Pointi yetu ni kuwakanya Simba na timu nyingine za ligi kuu kuachana na mambo ya kuamini waganga . Hata tabia ya Mbeya City kulinda uwanja, kuchimbua uwanja na kufukia vitu ni ya kishamba, matokeo hayapatikani kwa njia ya Waganda. Mbona kuna mataifa yanasifika kwa uchawi lakini wanaboronga katika soka?

Hata hapa Tanzania maeneo yanayosifika kwa uchawi mfano Sumbawanga mbona hawana hata timu ya ligi kuu?

Inawezekana waganda wanatumika kwasababu ya mila na desturi za kizamani, lakini hayatakiwi kufanyika kwa kasi ya ajabu kama wanavyofanya Simba na timu nyingine.

Kama yanafanyika kwasababu za kitamaduni basi yafanyike kwa siri pasipokuwahusisha wachezaji, haiwezekani eti wamekuja waganga usiku Hotelini, wachezaji wanaamushwa usiku kusikiliza maelekezo ya Waganga.

Unawachosha wachezaji, hawapumuziki vizuri, matokeo yake wanapoteza malengo, inatakiwa mchezaji alale mapema, akae kitandani awaze mechi ya kesho, ajiandae na mechi kisaikolojia, lakini unapomuamsha usiku unamnyima muda wa kupumzika, pia unamnyima nafasi ya kuuwaza mchezo wa kesho na matokeo yake analala na msongo wa mawazo na hasira juu kutokana na kusumbuliwa usiku.

Matokeo yake wanaingia kwenye mechi bila kuwa sawa kisaikolojia na wanafungwa si kwasababu ya kukosa uwezo bali ni miundombinu ya viongozi kushindwa kuwaandaa wachezaji kiuweledi.

Waganga hawasaidii katika soka, maandalizi ya kitaalamu, kiuweledi ndiyo yanatoa nafasi ya kupata matokeo. Simba na timu nyingine zote badilikeni!

Nawatakiwa jumatatu njema, tukutane tena jumatano ya wiki hii!

Chanzo: ShaffihDauda Blog

 
mkuu kuna kitu hukijui ni kwamba simba au yanga hawezi kumfunga mbeya city kwa nguvu ya uchawi na sababu kubwa ni kwamba hakuna mwanainchi au mganga ataetoa ushirikiano wa uhakika kwamba mcc wafungwe hivo simba na yanga zinapigwa changa la macho.

Mechi ya mwaka jana kati ya mcc na ssc kuna watu kwa kushirikiana na watu wa ssc toka dsm inasemekana walienda kwa mganga kuroga mcc habari zikawafikia wazee wa kimila unajua waliambiwa nn.

Walichoambiwa ni kwamba endapo mcc wangepoteza mchezo wangehama mjini cha nguvu bila mjadara bahati nzuri kwao na mbaya kwetu mcc tukadroo lile gemu. Sasa kwa mazingira hayo wanaweza wakafanya mchezo mwingine wa kuisababishia matokeo mengine ssc.

Japo sina imani na chanzo chako cha habari kwa sababu shafii dauda ni muongo sana tena sana na mwisho simba na yanga wacheze mpira sasa ivi siyo zamani
 
tatizo akili ndogo ya viongozi wa simba
 
Mimi huwa naona viongozi wa vilabu vyetu vya Simba na Yanga kama wendawazimu baridi.

Hivi inaingia akilini hatujapata mafanikio ya maana kwenye soka toka Uhuru pamoja na kutumia waganga lakini bado tunaendekeza upuuzi.
 
Mimi huwa naona viongozi wa vilabu vyetu vya Simba na Yanga kama wendawazimu baridi.

Hivi inaingia akilini hatujapata mafanikio ya maana kwenye soka toka Uhuru pamoja na kutumia waganga lakini bado tunaendekeza upuuzi.

Ungetoa lawama kwa viongozi wa Simba sports club na wala si wa Yanga Fc....!

Yanga Fc ndio Klabu pekee Tanzania yenye idadi mataji ya kufa mtu....!
 
Simba inajulikana kwa shughuli hizo. Hapo Shafii kafanya habari iwe rasmi tu lakini wanajulikana jinsi wajanja wanavyo wapiga hela. Hivi timamu ukwepe mazoezi uwanjani kwa upuuzi huo?

Na kocha akikataa huo upuuzi wao anatimuliwa!
 
shafii mnafki sana ***** zake,ye mambo ya ajabu yote anayanasbisha na simba,yanga hawagusi ***** zake cauz viongoz wao watata kina akilimali,jery af pia anamwogopa sana manji mpumbav yule,kila siku kuikandia simba sa muache na si tutanza utata atukaushie mana kazidi kutupanda..
 
shabhibhii nafwa;

mambumbumbu bwana sasa hapo imeingiaje tena ? maana mbeya city hajawahi kumfunga yanga tangu apande ligi kuu sikuzote huwa anapokea vipigo haijalishi kama yupo ugenini au sebuleni kwake..na katika hiyo makala ya shaffih sijaona akiizungumzia yanga
 
Last edited by a moderator:
Kumbe ndo yako kwa jirani hayo,
kah sikuyajua ahsante Shaffih Dauda kwa kutujuza ili waweze kujirekebisha.
 
Back
Top Bottom