Simba inaanguka taratibu na wauaji wake ni hawa hapa

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,333
Reaction score
5,845
Kuna utafiti mdogo nimefanya na kugundua kwa sasa waliokuwa wapenzi wa Simba wengi wameanza kutafakari iwapo walikuwa sahihi kuishabikia timu hii.

Hata hivyo kuna watu muhimu wanahusika moja kwa moja katika kuishusha Simba taratibu lakini kwa uhakika
Wa kwanza ni mwekezaji ambaye bila kupepesa macho wala kumumunya maneno,anahusika kwa kiwango kikubwa kuishusha na hakika atafanikiwa kufanya hivyo.

Inaonekana kama yeye ndiye chanzo cha migogoro kutokana na misimano na aina ya utendaji kazi wake.
Hapa sitaeleza mengi lakini kama anaweza kutoka hadharani na kusema anaidai Simba mabilioni ya pesa,huku watu wengine wakinyimwa fursa ya kuidhamini timu kwa kuwa yeye yupo,hilo linanifanya nimuone kama mbabaishaji kwani msingi wa kutoa pesa zake za udhamini,hauko wazi kimaandishi hivyo watu wengi kuona anatoa kwa mapenzi take tu.
Wa pili ni mwenyekiti wa sasa.

Huyu ni jeuri na hana msaada wowote kwa wanachama waliomchagua zaidi ya kutoa maneno ya kejeli kwa wanachama wanaohoji utendaji wake.
Wa tatu ni Aden Rage.

Huyu anaamini kwamba yeye ndiye mwenye akili pale Simba kwa kuwa aliwahi kuwa kiongozi na hivyo viongozi wote wako sawa tu hats kama timu haichukui vikombe achilia mbali kufungwa mechi zote na mpinzani wake wa jadi kitu ambacho Simba hawakufanya walipokuwa katika ubora wao.
Wa tatu ni Kaduguda.

Huyu mara kadhaa amekuwa akiungana na mashabiki kumlaumu Mangungo kuwa ameshindwa kuifunga Yanga,huku akidai yeye hawezi kufungwa na yanga mfululizo( hapa anawaza uchawi)
Kaduguda amepigilia msumari wa moto kwa kauli aliyotoa Rage kwamba ni kweli mashabiki wa Simba hawana akili kwa sababu hawajui misingi ya mpira wa miguu.

Yeye anajikuta ni mtu mwenye akili za pekee kuliko wanasimba wengine ambao hata hivyo wanatukanwa ni mbumbumbu kwa kuwa hawajui kazi za mangungo wanayemtaka ajiuzulu.

Wa mwisho ni mashabiki wenyewe ambao wengi wamechoka kuitwa mbumbumbu na hivyo wengi sana wanarudi nyuma na kutoishabikia tena Simba.

Hakuna mtoto atakayependa kuonwa hana akili kisa kuipenda Simba.
Kwa sasa Simba sio tena nguvu moja
 
Nakumbuka kipindi Yanga wanapitia magumu walikuja na msemo wao wa kujipa moyo "Tuliipenda wenyeweee acha ituue" asante sana @Kigelegele_Yanga ulitupa ujasiri wa kuipenda timu
I love you Yangaaa
 
Nakumbuka kipindi Yanga wanapitia magumu walikuja na msemo wao wa kujipa moyo "Tuliipenda wenyeweee acha ituue" asante sana @Kigelegele_Yanga ulitupa ujasiri wa kuipenda timu
Yanga huwa tunaanguka na team na kuinuka nayo,lile bakuli kila mechi pale Taifa tulikuwa tunatoa kwa moyo wote, wenzetu hawawezi kufanya vile
 
Kama ni report ya utafiti wako, basi ungeiweka hivi;

TAARIFA YA UTAFITI MDOGO KUHUSU KUANGUKA KWA TIMU YA SIMBA SC

Utangulizi
Utafiti huu mdogo umefanyika kwa lengo la kuchambua sababu kuu zinazopelekea kuporomoka kwa utendaji na mvuto wa Klabu ya Simba SC katika kipindi cha hiki. Matokeo ya awali yanaonesha mabadiliko ya mitazamo miongoni mwa mashabiki, pamoja na viashiria vya mgogoro wa kiuongozi na kiutendaji ndani ya klabu.

1. Mabadiliko ya Mitazamo ya Mashabiki

Kuna ongezeko la mashabiki waliokuwa waaminifu kwa muda mrefu kwa Simba SC kuanza kutafakari iwapo walikuwa sahihi kuendelea kuishabikia klabu hii. Hali hii inatokana na mwelekeo wa sasa wa klabu unaoonekana kutoendana na matarajio yao, jambo linaloathiri hamasa na mshikamano wa mashabiki.


2. Wadau Wakuu Wanaochangia Kuporomoka kwa Simba SC


2.1 Mwekezaji

Mwekezaji anatajwa kuwa mhusika mkuu katika kuporomoka kwa klabu. Kwa mujibu wa uchambuzi, aina ya misimamo na mtindo wa uongozi wa mwekezaji huyu umeleta mgogoro wa wazi. Aidha, kauli yake ya kudai klabu mabilioni ya pesa pasipo kuwepo kwa msingi wa kimaandishi wala makubaliano ya udhamini, imewafanya baadhi ya watu kumwona kama mbabaishaji. Pia, inadaiwa amewazuia wadhamini wengine kuiunga mkono klabu kwa sababu ya uwepo wake.

2.2 Mwenyekiti wa Sasa
Mwenyekiti anaelezwa kuwa na tabia ya kijeuri na kukosa msaada wa maana kwa wanachama waliomchagua. Anatajwa kutumia lugha ya kejeli dhidi ya wanachama wanaohoji utendaji wake, hali inayozidisha mpasuko wa ndani wa uongozi.

2.3 Aden Rage
Aden Rage anatajwa kuwa na mtazamo wa ubinafsi wa kiakili, akiamini kuwa yeye pekee ndiye mwenye uelewa ndani ya klabu kwa sababu ya kuwa kiongozi wa zamani. Ameonekana kutokuwa na wasiwasi hata pale timu inaposhindwa kutwaa makombe au kupoteza mechi dhidi ya wapinzani wa jadi, tofauti na utamaduni wa mafanikio ya awali ya Simba SC.

2.4 Kaduguda
Kaduguda ametajwa kuwa miongoni mwa wanaochochea lawama zisizo na msingi dhidi ya Mangungu, hasa baada ya kushindwa mara kadhaa dhidi ya Yanga SC. Kauli yake ya kuunga mkono madai ya Rage kwamba mashabiki wa Simba hawana akili, imezua taharuki. Anaonekana kujiona mwenye uwezo wa kipekee zaidi ya mashabiki wengine wa Simba, hali inayowavunja moyo wanachama na mashabiki wa kawaida.

2.5 Mashabiki Wenyewe
Mashabiki nao wametajwa kuwa miongoni mwa wachangiaji wa hali hii, hasa kutokana na ukosefu wa msimamo wa pamoja na kuchoka wa kudhalilishwa kwa kuitwa "mbumbumbu." Wengi wameanza kurudi nyuma na kuacha kuishabikia timu, wakiwa na hofu ya kushushwa hadhi ya kiakili kutokana na mapenzi yao kwa Simba. Kwa sasa, Simba SC haionekani tena kuwa β€œnguvu moja.”

Mwisho
Utafiti huu mdogo umebainisha kuwa matatizo ya Simba SC hayaishii katika uwanjani pekee, bali yamejikita kwenye ngazi za juu za uongozi, wawekezaji, viongozi wa zamani, na hata mashabiki wake. Ili kurejesha heshima na mafanikio ya klabu, kunahitajika mabadiliko ya kina katika fikra, uongozi, na ushirikishwaji wa wanachama.
 
Ongera Sana Mkuu Uliyosema yote ni Sahihi/ (1) Huyu Ponjoro MO DEWJI ni mbabaishaji Sana tu, Mimi Nilikuwa Namtetea kipindi Cha Nyuma, Lakini nikiri Wazi Yeye ndio Chanzo, (2) Huyu MMATUMBI Murtaza Mangungu sijapata kuona Toka SIMBA izaliwe Mwaka 1936 Kuwa na kiongozi Mjinga -Jeuri KILAZA, Imefika Hatua Wanachama/ Wapenzi na Mashabiki Tumeshindwa kuchukua Hatua Kwa huyu Mpumbavu MURTAZA MANGUNGU/(3) Aden Rage, huyu Msomali Anajiona Pale SIMBA kama Yeye ndio Mchezaji wa Zamani Sana Aliyechezea Simba Kwa kiwango kikubwa- Imefika Hatua Anajiona Yeye ndio Kila kitu - Wakati Kuna Wachezaji Waliupiga Mwingi Pale SIMBA/ Ambao Wako hai na Wako kimiya/ Abdallah kibadeni, Mohamed Bakari Tolu, Nico Njohole, Daudi Salum, SHABANI Baraza- Awa ndio Wachezaji Nembo ya Simba Sio yule Mpumbavu Msomali Rage, (4) Kuhusu Simba wa Yuda Mhina kaduguda/ Yuko Sahihi kusema Mashabiki Wapenzi na Wanachama Mbumbumbu, ikiwa Mbaka Leo Takataka Mangungu Tunashindwa kumtoa KAZI yetu kulalamika kwenye Mitandao, Basi ni Bumbumbu kweli kaduguda Yuko Sahihi, Na Simba Day hawo Niliowataja Wote watakwenda uwanjani na wake Zao Wangese hawa Viongozi Mamluki
 
Mjinga ni mjinga tu.

Yaan wewe hayo yote uliyoyataja Ndio Mhumili wa Simba,sasa niambie Simba imeanguka Au Lah!
 
Mvuto umeukosa wewe Uto FC. Simba Ina nguvu, mshikamano na Raha kuliko kipindi kingine chochote. Kufungwa na Uto Fc ni jambo la ovyo na linauma but si sababu ya sisi kuanzia kugombana. Nisichopinga ni kwamba Mo anafaidika na Simba kwa kiasi Fulani but Simba bila Mo itakuwa ka pamba tu.
 
Kijana wa Rage. Wewe ndio kubwa la mambumbumbu. 😁😁😁😁😁
 
Adui wa mwingine ni wachambuzi bahasha bin ticket wao kutwa kuiponda yanga hata kwa mazuri wakihisi wana ivuluga kumbe ndio wanawaonyesha panapo vuja na wanakarabati
 
Hivi Sheria za Tanzania zinaruhusu wachezaji wangapi kutoka. Nje kwa timu Moja?
 
Toa kwanza tofauti kati ya mdhamini vs mfadhil vs muwekezaji kisha tuje kwenye research
 
SIMBA IMECHEZA FAINALI JUZI,NI JUZI TU.HALAFU KIMATAIFA SIMBA NI KUHWA KULIKO YANGA.
 
Toa kwanza tofauti kati ya mdhamini vs mfadhil vs muwekezaji kisha tuje kwenye research
Mdhamini-anaweka pesa bila kutaka faida kutoka kwako bali ana njia zake ambazo atafaidika kupitia wewe.

Mfadhili-anaweka pesa anakusaidia bila kujali kurudishiwa au kufaidika chochote kutoka kwako.
Muwekezaji-anaweka pesa ili afaidike kutoka na ile hela aliyoweka kupitia kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…