Simba inadhaminiwa na GSM kimya kimya?

Simba inadhaminiwa na GSM kimya kimya?

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
1,016
Reaction score
2,195
Naanza kupata mashaka. Inawezekana Simba nayo inadhaminiwa na makampuni ya GSM kimya kimya. Kwanini kila wakicheza na Yanga wanafungwa? Hii ni mara ya nne mfululizo hawapati matokeo.

Nasema hivi kwa sababu imejengeka dhana kwamba timu zote zinazofanya biashara na GSM zinagawa points kwa Yanga ambayo ndio partner mkuu wa GSM. Achilia mbali Azam ambao wanadhamini timu zote 16 za Ligi Kuu.

Simba tuambizane ukweli, kama hoja ni points au kufungwa na Yanga kisa udhamini wa GSM, mbona na nyie mnafungwa kizembe sana!?

Msimu huu tutapimiana kipimo kile kile!
 
Comrade una hoja ya msingi. Ila sikushauri uingie sana kwenye hizi siasa za simba na Yanga. Maana zinaweza kukutoa kwenye mstari. Mimi nakushauri uwekeze zaidi nguvu zako kwenye kujenga brand ya timu yako ya Singida Black Stars.

Hizi siasa za simba na Yanga ungetuachia wenyewe. Ni ombi tu lakini, huku nikitambua wazi ya kwamba una haki na uhuru wa kutoa maoni yako humu jukwaani.
 
Hakuna jipya
 
Attachments

  • Image_1729576239525.jpg
    Image_1729576239525.jpg
    147.1 KB · Views: 5
Wazee wa Simba wamesema mmoja wa watendaji wa TFF mkewe anafanya kazi GSM, mambo ya ajabu kwelikweli.

Kama ingekuwa ushindi wa Yanga unapatikana kwa njia tofauti na kikosi imara GSM angetumia pesa nyingi kufanya sajili kubwa? Mmesahau Yanga walitoa kiasi gani kumsajili Aziz Ki achilia mbali mshahara mkubwa anaolipwa?

Mpira wa sasa umehamia kwenye uwekezaji, Simba wanapaswa kuondoka kwenye fikra za kizamani.
 
Comrade una hoja ya msingi. Ila sikushauri uingie sana kwenye hizi siasa za simba na Yanga. Maana zinaweza kukutoa kwenye mstari. Mimi nakushauri uwekeze zaidi nguvu zako kwenye kujenga brand ya timu yako ya Singida Black Stars.

Hizi siasa za simba na Yanga ungetuachia wenyewe. Ni ombi tu lakini, huku nikitambua wazi ya kwamba una haki na uhuru wa kutoa maoni yako humu jukwaani.
Ana hoja ya msingi, timu yake imekuwa ikisakamwa sana kila ikutanapo na Yanga.
 
Wazee wa Simba wamesema mmoja wa watendaji wa TFF mkewe anafanya kazi GSM, mambo ya ajabu kwelikweli.

Kama ingekuwa ushindi wa Yanga unapatikana kwa njia tofauti na kikosi imara GSM angetumia pesa nyingi kufanya sajili kubwa? Mmesahau Yanga walitoa kiasi gani kumsajili Aziz Ki achilia mbali mshahara mkubwa anaopokea?

Mpira wa sasa umehamia kwenye uwekezaji, Simba wanapaswa kuondoka kwenye fikra za kizamani.
Kwamba mke wa Karia kufanya kazi GSM ni dhambi?
Hivi Kwa mfano mke wa Ali kamwe hawezi kuajiriwa metl ya mo akapiga kazi?
Mpira sio uadui
 
Kimsingi makolo hawana hoja ya maana. Kinachoendelea kwa sasa ni kutapatapa tu kutafuta huruma na ahueni kutokana na vipigo mfululu vinavyowaandama. GSM sio wa kwanza kudhamini wapo walioanza na hatakua wa mwisho kudhamini timu nyingi kwenye ligi moja.

Jengeni timu, ongezeni uwezo kwa viongozi wenu wa mpira. Haya mambo muyaache bado mnaishi kizamani kwa kuendelea kuamini uchawi na mambo kama hayo ya bahasha
 
Comrade una hoja ya msingi. Ila sikushauri uingie sana kwenye hizi siasa za simba na Yanga. Maana zinaweza kukutoa kwenye mstari. Mimi nakushauri uwekeze zaidi nguvu zako kwenye kujenga brand ya timu yako ya Singida Black Stars.

Hizi siasa za simba na Yanga ungetuachia wenyewe. Ni ombi tu lakini, huku nikitambua wazi ya kwamba una haki na uhuru wa kutoa maoni yako humu jukwaani.

Nimekuelewa kamaradi lakini soma vizuri mstari wangu wa mwisho umebeba ujumbe mzito!
 
Wazee wa Simba wamesema mmoja wa watendaji wa TFF mkewe anafanya kazi GSM, mambo ya ajabu kwelikweli.

Kama ingekuwa ushindi wa Yanga unapatikana kwa njia tofauti na kikosi imara GSM angetumia pesa nyingi kufanya sajili kubwa? Mmesahau Yanga walitoa kiasi gani kumsajili Aziz Ki achilia mbali mshahara mkubwa anaolipwa?

Mpira wa sasa umehamia kwenye uwekezaji, Simba wanapaswa kuondoka kwenye fikra za kizamani.
Acha waendelee kutafuta mchaw...badala ya kuboresha kikosi[emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom