Simba inadhaminiwa na GSM kimya kimya?

Simba inadhaminiwa na GSM kimya kimya?

Wazee wa Simba wamesema mmoja wa watendaji wa TFF mkewe anafanya kazi GSM, mambo ya ajabu kwelikweli.

Kama ingekuwa ushindi wa Yanga unapatikana kwa njia tofauti na kikosi imara GSM angetumia pesa nyingi kufanya sajili kubwa? Mmesahau Yanga walitoa kiasi gani kumsajili Aziz Ki achilia mbali mshahara mkubwa anaolipwa?

Mpira wa sasa umehamia kwenye uwekezaji, Simba wanapaswa kuondoka kwenye fikra za kizamani.

Una akili sana dada kama umeolewa na una watoto basi jamaa amepata mke haswa na watoto mama wanae
 
Azam anadhamini namungo wala hawaongei. Azam anaidhamini APR ya Rwanda na bado Azam haohao wametolewa CAFCC na APR wanaowadhamini
Mnajisumbua kuwajibu,hao ni mambumbumbu wanachotaka timu zingine zisizaminiwe Ili zikose pesa za kuimarisha vikosi vyao,wawe wanajipigia tu kila wapokutana nao.
 
Naanza kupata mashaka. Inawezekana Simba nayo inadhaminiwa na makampuni ya GSM kimya kimya. Kwanini kila wakicheza na Yanga wanafungwa? Hii ni mara ya nne mfululizo hawapati matokeo.

Nasema hivi kwa sababu imejengeka dhana kwamba timu zote zinazofanya biashara na GSM zinagawa points kwa Yanga ambayo ndio partner mkuu wa GSM. Achilia mbali Azam ambao wanadhamini timu zote 16 za Ligi Kuu.

Simba tuambizane ukweli, kama hoja ni points au kufungwa na Yanga kisa udhamini wa GSM, mbona na nyie mnafungwa kizembe sana!?

Msimu huu tutapimiana kipimo kile kile!

Wewe ni Masanza yule Msemaji Wa Singida..?


Kama ndo Wewe..basi Mambo Mengine utuachie Sisi Mashabiki..!

Sisi tuna Ulimwengu Wetu wa soka..!

Wewe Concentrate na Weledi ' Professionalism' !

Huu ni ushauri Sio Mkwala Usije Ukapotea ndugu..! Jitahidi hiyo timu yako angalau iwe kwenye Ramani ya soka Kwanza.
 
Back
Top Bottom