Rage alishawahi kuwabatiza jina ambalo sio busara kulitaja hapa
1. Team ilipigwa 5 November 2023
Ila wana simba masikini washashahau
2.kwenye mkutano waliletewa manzoki na kupewa ubwabwa na chupa 1 ya pepsi big.
Wakampa kura za ndio Mangungu
3. Mo anadai team ameinunua na ni team yake binafsi.
Masikini watani hawana habari wapo wanapata faraja fake ya goli la azizi ki kukataliwa
4. Walichangishwa hela wajenge uwanja
Wakaambiwa pesa imejenga ukuta na chumba cha mlinzi,
Masikini watani wakajisahau hata hawakumbuki
5. Alikuja goal keeper Mbrazil kwa usajili wa B 1.3.
Aliishia kuumia mazoezini hakucheza hata mechi moja
Mbumbumbu wamesahau na hili
6. Mafanikio ya last season ni kibegi, na kufungua group la WhatsApp, ndo walivoambia kwenye mkutano mkuu.
Maskini mbumbumbu waliishia kushangikia kwa furaha
7.usajili uliovunja record ni ule wa Jobe na Fredi, wanacheza kama wajawazito, masikini wanasimba wenyewe hawajali
8.Jezi hazina quality kama sare za magereza. Unakuta watani hata hawatambu hilo
9. Walifanya pre season Qatar na wachezaji 7 tu.
Huku wengine wakiwa na mgomo na hakuna mbumbumbu yeyote alitambua hilo
10. Robo final ndo team pekee imepigwa nje ndani lakini maskini watani hawajali wapo busy kujifariji na bao la Azizi ki lililodhulumiwa
Chonde chonde tuwaache usingizi ili tuchukue ubingwa back to back kwa miaka 10
Nitamheshimu sana Rage kwa kuwaita watani wetu hawa jina mbumbumbu. Hakika aliona mbali ni nabii