Simba inaenda kutolewa kombe la waliofeli Jumapili

Simba bado inajitafuta, bahati mbaya sana wako kwenye mashindano na hali bado kocha anatengeneza timu.

Wanampa mzigo mkubwa sana kocHa, sijui kama wanajifunza kuwa wanatakiwa kuleta kocha mapema na wachezaji mapema ili akae nao pre season aweze kutengeneza kitu. Lakini hii unamleta kocha siku kadhaa kabla ya ligi na mashindano makubwa sio nzuri.

Simba wasijiachie sana kwa kuwa tu wako nyumbani, wakafunguka zaidi watapigwa na kushangazwa. Waendelee kucheza kwa tahadhari.

Mwisho, uongozi wa Simba unazingua, mambo yasipoenda vizuri uwanjani wanamtoa kafara kocha wakati wao mambo wanayepeleka hovyo.

CEO Barbra alikuwa smart sana, simba ilikuwa inaendesha mambo yake kitaalamu. Tangu ameondoka usajili ni wa hovyo, kocha scouting hovyo, vurugumechi.
 
Mabingwa wanacheza Zanzibar zungumzieni hao achaneni na Simba.
 
Wacha watolewe tu Losers Cup.
 
 
Kuna Chura mwenzako aliahidi kutoa tiGO kama Simba ingeshinda au kutoa droo tu kule Tripoli. Ila cha ajabu haonekani tena hapa JF.

Uto muwe mnajitahidi kutimiza ahadi zenu.
 
weka walau alama za uandishi
 
Exactly🤝yaan huyu bwege kachambua akili yake ya kimaskini
Yaan umechambua akili yako ya kimaskini siyo mpira💀hata kama msemeje ukweli ni kwamba darasa la saba aliyefaulu hawez mringishia form four aliyefeli🤝😂😂chukua hyooo...baada ya mechi tunasubir uchambuz wako mwingne🚮😂
 
Umesoma ukaelewa nilichoandika Dada? Mpira unafatilia? Au unadhani mimi sio Mshabiki wa Simba.

Sasa ambacho unakipinga ni kipi?
Kwamba Simba haijitafuti sasa hivi?
Kocha hajachelewa kuja?
Simba wasicheze kwa tahadhari?

Yani unachokikataa ni nini, sijakuelewa
 
Huwez elewa mpka uwe na D mbili😂😂😂🫂
 
Alafu unajiita mchambuzi! Labda unachambua maharage na mbaazi...
Simba itapambana kadri itakavyo kuwa.Kama itatolewa basi si Jambo geni...
Mungu ibariki Tanzania...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…