Simba itacheza Michuano ya Shirikisho barani Afrika baada ya kuzidiwa idadi ya mabao ya kufunga na Azam FC

Simba itacheza Michuano ya Shirikisho barani Afrika baada ya kuzidiwa idadi ya mabao ya kufunga na Azam FC

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Sasa ni rasmi msimu ujao Klabu ya Simba itacheza Michuano ya Shirikisho barani Afrika baada ya kuzidiwa idadi ya mabao ya kufunga na Azam FC licha ya wote kuwa na pointi 69 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara iliyotamatika leo.

Licha ya Simba kushinda mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania lakini haikusaidia kuwavusha kwenda Ligi ya Mabingwa baada ya Azam FC kushinda mabao 2-0 dhidi ya Geita Gold FC uwanja wa Nyankumbu.

Bao la kwanza la Simba katika mchezo huo limefungwa dakika ya 87 kwa mkwaju wa penalti na Saido Ntibazonkiza huku bao la pili kikifungwa na Willy Essomba Onana dakk ya 90, aliyeingia kuchukuwa nafasi ya Mzamiru Yassin.

Timu zote zilionyesha mpira mzuri na dakika 45 kipindi cha kwanza zilikamilika bila kufungana.

Dakika ya 30 na 31 kipa wa Simba Ayoub Lakred aliokoa mipira ya hatari iliyopigwa na David Bryson mpira wa faulo baada ya Shomari Kapombe kucheza madhambi kwa Ismael Kada. Kwa upamde wa Simba dakika 6 Luis Miquisson amekosa nafasi ya wazi alipiga shuti nje ya 18 na mpira kupaa juu ya lango.

1716910836466.jpg
 
Kwaio sasa shirikisho ni losers Cup amna sio ??😂😂
 
Namtafuta Ahmed Ally; aje hapa tuhangaike naye.
 
Tumevuna tulichopanda, bora ilivyokuwa hivyo maana janjajanja na propaganda zilizidi.
Kabisa, wale matapeli kina Try Again wasingeona makosa yao, wacha twende huko shirikisho labda watayaona makosa yao. Tumebaki kujivunia mashabiki wa Insta na X.
 
Klabu ya simba INA uongozi mbovu na wachezaji wenye kiwango duni, sishangai kuona wanamaliza nafasi ya tatu. Hata huyu kocha Mgunda hana uwezo wa kubadilisha timu kwenye tactical na technical organization wakati Mpira unaendelea
 
Back
Top Bottom