Simba itaingia fainali ikiwa huko Afrika kusini

Ushindi mwembamba Gani?
Kwani wao walimtoa Zamalek kwa magoli mangapi?
Mbona unarukaruka kama bisi kikaangoni?! hoja hapa ni kauli zenu mlipofungwa misri mlisema "subirini watakuja nyumbani dar, leo tena mnasema mambo yamebadilika kwenye mpira hakuna cha nyumbani, πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ twende na hiyo hoja kwanza
 
Tangu msimu unaanza Simba imeonyesha Changamoto kubwa sana kwenye No 10.

Nimepiga kelele na Viongozi Dirisha dogo wasajili quality Walau tatu.
Mpanzu, Kimvuzuidi, Traole. Cha ajabu na kusikitisha wakasajili Mchezaji Mmoja tu mpanzu.
Mkuu mbona viongozi walishasema kupata mchezaji mzuri kwenye dirisha dogo huwa ni ngumu, huyo mpanzu mwenyewe tumembahatisha kwa vile tu alifeli ulaya akawa hana timu ila naye ilibaki kidogo tumkose, hakuna timu inayokubali kumuachia mchezaji wao wa maana dirisha dogo wanaoachwa ni hao hao magalasa tusubiri dirisha kubwa tu
 
Asante Mungu,ulinionesha juu ya mchezo wa marudiano kati ya Simba na Stellenbosch kia Simba atafuzu.
 
Hongera sanaa kaka
Leo natembelea uzi za waliotabiri na wakapatia mbarikiwe sanaaa
Nawapendaaa mnoo
Amina Dada yangu.
Simba imeingia fainali Kwa jasho na damu
Simba Kila mechi kwake ilikua ni kama Fainali,tofauti na Yanga walipoingia,
Timu walizokutana nazo zilikua choka mbaya.
Simba bado tunajenga timu,hii wala sio masihara.
 
Ulinena kweli...
 
Amina Dada yangu.
Simba imeingia fainali Kwa jasho na damu
Simba Kila mechi kwake ilikua ni kama Fainali,tofauti na Yanga walipoingia,
Timu walizokutana nazo zilikua choka mbaya.
Simba bado tunajenga timu,hii wala sio masihara.
Sure my kaka..
 
Nimeongea na Mo akuajiri uwe mkubwa wa kamati ya ufundi aka vigagula ya simba.
 
Mimi nitakuwa Tofauti kidogo.

Natamani simba wafanye Sajili za wachezaji Bora Afrika, sio hawa waliopo leo.

QUALITY YA WACHEZAJI 50% HAWAFAHI KUCHEZA SIMBA.
SIMBA INAZIDIWA QUALITY NA SINGIDA.
QUALITY.
QUALITY.
QUALITY.
Niliwaambia simba inazisiwa quality na Singida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…