Sio kweli, nakukumbusha kuwa Berkane, Zamalek, USMA, ni miongoni mwa timu ambazo zilianzia second round msimu huu unaoisha.
Kinachosababisha timu zingine zianzie second round ni kutokana na idadi ya timu zinazoshiriki kwenye mashindano iwe klabu bingwa ama shirikisho.
Kikawaida zinatakiwa timu 64 kwenye klabu bingwa na pia timu 64 kwenye shirikisho ili wakicheza hatua ya raundi ya kwanza zibakie timu 32. Na baada ya hapo inacheza raundi ya pili zinabakia timu 16 zitakazokuwa zimefuzu hatua ya makundi.
Hivyo ikitokea timu zinazokubali kushiriki ni pungufu ya 64, hupelekea timu zingine zisianzie hatua ya awali ili kuweza ku balance timu 32 zitakocheza hatua ya pili.
Mfano tuchukulie timu zilizokubali kushiriki mashindano zipo 52 pekee, hapo kuna gap ya timu 12 kufikisha timu 64. Hivyo timu 12 zitakuwa zimefuzu moja kwa moja kucheza hatua ya pili na hizo timu 12 zitapatikana kutokana na point zao kwenye rank ya CAF.
Kwahiyo itakuwa 52-12= 40
Timu 40 zitacheza hatua ya awali na katika hizo timu 40, timu 20 zitatolewa na timu 20 zitafuzu kucheza hatua ya pili. Sasa unachukua timu 20 unajumlisha na timu 12 zilizofuzu moja kwa moja unapata timu 32 zinapaswa kucheza hatua ya pili ili kupatikana timu 16 za hatua ya makundi