Simba Itatolewa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho. Itakutana na Vigogo Wydad, Asec Mimosas na As Vita

Bora umetoa elimu ya bure kwa ndunduka
Bahati mbaya wewe na mwenzio wote mmeonesha mnafanana akili, na umekariri kuwa mtu akitoa maoni fulani ni Simba. Labda wewe ni mgeni na mimi, mimi ni mshabiki wa mpira hivyo mpira kwa ujumla naufahamu kwa kiasi chake kwanzia, taratibu, kanuni, sheria, mbinu na ufundi pia japo siwezi kujua kila kitu ila sinaga tabia ya kuongelea mpira kwa angle ya kiushabiki. Sasa huyo mwenzio hapo juu nimempa somo kubwa tu kuhusu mashindano ya CAF hivyo kwavile nawe umeonesha kutokujua basi pitia. Kisha njoo na hoja kuhusu kile nilichokiandika. Nipo tayari kukosolewa karibu
 
High ranked teams zinaanzia round ya pili siyo hicho ulichoeleza wewe.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Sawa embu twende taratibu utanielewa tu, nijibu maswali yafuatayo:
1) CAF ina jumla ya wanachama wangapi?
2) Je ni high ranked teams ngapi zinazotakiwa zianzie round ya pili?
Huwa zinakuwa 8 -10 kwa champions league na CAFCC zinakuwa 4-10. kutegemea na idadi ya highly ranked club

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
CAFCL msimu huu ulioisha,
Simba
Sundowns
Al Ahly
Esperance
Wydad
Petro Luanda
CR Belouzdad
Pyramids
ASFAR
TP Mazembe

Walianzia second round na zingine zilianzia first round.

Kwenye CAFCC hizi timu Tisa zilianzia second round
Zamalek
USM Alger
Modern future Fc
Rivers United
Diable Noire's
Segrada Esperanca
RS Berkane
Saint Eloi Lupopo
Super Sport United.



Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu unapoteza muda wako, humu kuna raia hakuna wanalojua kuhusu soka. Ni ushabiki tu wa kijinga.
 
Kwanini simba apangwe na wydad wakati kwenye rank za caf wote wapo juu
 
Sasa mkuu umeona ulivyojionesha kuwa ni muongo?
Ulisema inatakiwa timu 8 ndio zicheze hatua ya pili kwenye CAFCL halafu kwenye list yako kuna timu 10.

Umesema timu 4 kwenye CAFCC halafu kwenye list yako kuna timu 9 hauoni uliongea uongo?

Hapo kwenye CAFCC kuna timu tatu umeziacha, jumla timu zilizoanzia second round kwa msimu huu ulioisha katika CAFCC ni timu 12.

Kwanini timu 12?
Kwasababu jumla ya wanachama walioshiriki michuano ya CAFCC ni 41.
Katika wanachama 41, kuna wanachama 12 zinatakiwa kuingiza timu 2 hivyo unachukua 41 - 12 = 29
Wanachama 29 zinatoa timu moja moja na wanachama 12 zinatoa timu mbili mbili hivyo jumla ya timu ni 29 + 24 = 53

Jumla ya timu zilizopaswa kushiriki michuano ya kombea shirikisho kutola kwa wanachama 41 ni timu 53.

D.R. Congo, hakuweza kuingiza timu mbili japo inatakiwa kuingiza timu mbili kutokana na timu ya Maniema na Motema Pembe kushindwa kupata CAF license. Hivyo badala ya timu kuwa 53 zikawa timu 52.

Timu 52 haziwezi kucheza zenyewe kwa zenyewe zikabakia timu 32 hivyo ili upate timu 32 ni lazima timu ziwe 64 hivyo kuna pungufu ya timu 12.
Hivyo ili kupata timu 32 ni lazima timu 12 zikaanzie hatua ya pili na timu 40 pekee ndio zitacheza hatua ya awali ili kupata timu 20 zitakazoungana na zile timu 12 kufanya timu 32 za kucheza hatua ya pili
 

Ni timu 12 kwenye CAFCC zilianzia second round
1) Zamalek
2) USMA
3) Modern future
4)Rivers
5) Diable
6) Rayon sports
7) club Africain
8) KCCA
9) Berkane
10) Super sport united
11) St. Lupopo
12) Sagrada Esperanca
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…