Simba iwaongeze wabrazil watatu wa Singida na Manzoki, Okwa, Akpan, Dejan, Quattara piga chini

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Wale Wabrazil watatu wa Singida ni moto sana, nawaomba viongozi wa Simba waongee na Singida ili wale Wabrazil wakipige Msimbazi.

Aisee Simba ikiwapata wale wanaume itakuwa balaa, Makundi na akina Mzamiru siyo kweli, tutatia aibu mbele ya safari.

Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app
 
Quattara abaki ana improve mazoezini.

Hao wengine wa kuondoka dirisha dogo.
 
Unadhani kuwasajili hao ni kama kwenda kununua mtumba kariakoo?
 
KWA hio robo fainali zote tulizofika Mzamiru hukuona KAZI yake ? KWA TAARIFA yako Mzamiru yuko vizuri kuliko hao wa Brazil wako
 
Hao Wabrazil koko watafanya nini? Nilikuwa sijawahi kumuangalia vizuri yule Dario nikaona Watanzania kumbe tunashoboka na vichenga chenga, yule kule pembeni anakocheza kuna watu bora zaidi yake.
 
Mzamiru sasa hv amebadilika sana kiuchezaji naweza kumfananisha na bwana mdogo Kante pale chelsea. Mechi ya jana nadhani ndiye mchezaji aliyekimbia sana uwanjani kwa upande wa simba na amekiwasha dakika zote tisini bila ya kukata moto.
 
Tukiwapata hao wabrazili nadhani ndoo ya afrika itatua tanzania bila ya wasiwasi wowote
 
Hivi kwanini hamuwezi pendekeza usajili ufanyike bila kubeza waliopo..!

Kwahivyo haiwezekani kufika makundi na Mzamiru hiyo robo fainali zilizopita zilifikwa na Mbappe?
Muulize sasa yeye anaweza nini? Mashabiki wengi wa kitanzania ni mbumbumbu mkuu.
 
Wanacheza nafasi zip na Simba wana mapungufu maeneo yap? ndio mana kwenye timu zetu tunaharibu usajili maana hatuangalii mahitaji tunaangalia umachachari wa mchezaji
 
Mleta mada nenda kaongee na wabrazil na SBS, ukiweza sisi tutatoa pesa
 
Mwigulu hawezi kuwaachia hao
 
Acha upumbavu,Mzamiru usimchukulie poa na dharau za kishamba.
 
Mwigulu hawezi kuwaachia hao
Hivi ni kweli wanalipwa na Mwigulu?
Ana biashara gani ya kuweza ku manage kulipa wachezaji kama wale iwapo timu kubwa licha ya udhamini ya mabilioni bado wanalalamika gharama za uendeshaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…