Simba kama kweli mna Mpango wa kumuacha Thadeo Lwanga fikirieni upya

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Kuna tetesi zinavuma na zinavuma kweli kweli. Hata baadhi ya WanaJF àmbao ni mashabiki wa Simba wanazipa chapuo kwamba Kwa vile Mchezaji Thadeo Lwanga Kwa Sasa ni majeruhi basi Simba watumie nafasi yake kusajili mchezaji mwingine na hivyo kuachana naye Kwa kumvunjia mkataba.

Tukio hili halitakuwa na kiungwana na litawavunja moyo Sana Wachezaji wanaobaki kwamba nao siku wakijeruhiwa watatupiwa virago. Thadeo ni mchezaji mzuri na ameifanyia mengi Simba katika nafasi yake ya Mkata Umeme, Leo kumbwaga Kwa sababu ya ugonjwa haitakuwa tofauti na Mtu anayetoa talaka Kwa mkewe sababu ya kuugua Muda mrefu ili apate nafasi ya kuoa binti mwingine.

Mambo mengine tunatafuta laana.
 
Ndio kwanza nakusikia wewe na mm nashinda social media sana. Hofu zako tuu hizo
 
Amna kitu kama icho,wapinzani wa Simba kimataifa msimu uliopita walilalakiza kwa Mkapa kwaajili ya Lwanga.
 
Cha msingi kama wanaleta mbadala awe ni mkali mara 100 kuliko aliyetoka, sio wanatuletea u arsene wenger wakutaka kukuza vipaji katika nyakati tunazosaka mataji
 
Huwezi vumilia mchezaji majeruhi msimu mzima asiwepo hapo lazima utafute mbadala ikiwa unataka kugombea mataji kweli
 
Mh. GENTAMYCINE una maoni gani?
 
Ndio maana naipenda azam fc
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…