Simba Kimataifa Msimu Ujao: Is it road to another hell or new era of glory?

toobiter

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2017
Posts
1,309
Reaction score
2,577
Jana nchi ya Morocco ilipata watalii millioni 89. Hatujui uraia wao, hatujui tabia zao, hatujui wameoa au kuolewa, ila tunafahamu jambo moja tu kuhusu watalii hawa, wanapenda soka na jana mechi ya Simba na Wydad ilikuwa mbuga waliyoitembelea.

Usishangae, mech ya jana imetazamwa na watu million 89 duniani kote na hii sio kawaida kwa timu za Afrika mashariki.

SIMBA inajitafuta ndani ya soka la Afrika? Jibu ni hapana tayari imejipata japo haina kombe lolote kama kielelezo cha ukubwa wake ndani ya afrika.

Lakini pamoja na kutochukua kombe lolote kubwa ndani ya Mashindano ya Klabu Bingwa au shirikisho bado hakuna timu Afrika ambayo ikipangiwa Simba italala raha mstarehe, lazima kila mtu afanye homework yake vizuri la sivyo anaweza kutana na lolote linalopatikana ndani ya dakika 90.

Wapi ilipo Simba, inataka kwenda wapi na nani ataambatana nayo (wachezaji), hili linabakia kuwa swali muhimu mnoo kwa wana Msimbazi.

Kuna kauli moja maarufu huwa inatolewa misibani hasa wakati wa kuzika kwamba tulikupenda ila mungu amekupenda zaidi.Kauli hii inawahusu saana baadhi ya wachezaji wa simba.

Kama simba inajiona nusu fainali au fainali kabisa ya Klabu Bingwa Afrika basi kuna wachezaji wakuagana nao. Sio kwamba ni wabaya au hawafai ila kwenye basi la Simba la Nusu Fainali au Fainali Klabu Bingwa hawa hawana siti au nafasi hata ya kusimama tu ndani ya gari. Kifupi hawatakiwi.

Waitwe waambiwe ukweli na waagwe kwa heshima, kama wanaipenda klabu na kama mikataba yao inaelekea mwisho basi waachwe wakatafute malisho kwingine muda wao umeisha. We unaonaje is it a road to hell or road to glory?

Nani aachwe na nani abaki nadhani mechi ya jana imetupa majibu mazuri kabisa. Nini maoni yako juu ya Simba ijayo na safari yao?

Karibu.
 
Fanyeni transformation....Ili mfanye usajili mkubwa kama yanga

Watumien sana Yanga as role model wenu

Hakika mtafanikiwa
Kweli yanga anastahili kuwa role model wa yanga? Kweli?
 
Mabadiliko makubwa ya wachezaji ni muhimu na hili linaweza kufanyika kwa bachi za awamu tatu kwa misimu miwili ili kuifumua timu upya.

Bachi ya kwanza:
Bocco
Onyango
Sawadogo (mchezaji mzuri ila hatakuja kuwa fit)
Outtara (siasa zinamnyima namba)
Kakolanya (kaondoka mwenyewe)
Nyoni
Mkude
Saidoo
Kyombo

Bachi ya pili:
Zimbwe (wakati wa damu mpya). Sijamsoma vizuri ila nadhani Yahya Mbegu anaweza chukua nafasi yake.

Bachi ya tatu:
Chama (zama zake zinafikia ukingoni)
Manula (au abaki kuwa kipa #2)
Gadiel

Pia Kapombe ahamishiwe kiungo ndiyo ibaki nafasi yake ya kudumu na achukue nafasi ya Nyoni/Bocco kama senior player akirotate na kina Mzamiru/Kanoute. Mwenda aingizwe kwenye kikosi cha kwanza kama FB.

Atafutwe kipa mrefu ambaye baada ya mwaka mmoja kutoka sasa achukue nafasi ya Manula.

Baada ya miaka 2, Simba itakuwa mpya kabisa yenye damu changa lakini haitatetereka kwa mabadiliko haya.
 
Simba abaki
mzamiru
Kibu denisi
Kapombe
Zimbwe
Mwenda
Chama abaki ila awe anatokea sub
Inonga
Waliobaki wapumzike
 
At least naona hii inaweza kuwa reform nzuri

Tunahitaji "clasa hasa"ili tusonge mbele
 
Timely baada ya madirisha mawili au matatu tutaweza kuwa na kikosi kipya kabisa
 
Timely baada ya madirisha mawili au matatu tutaweza kuwa na kikosi kipya kabisa
Madirisha mawili makubwa na dirisha dogo moja. Dirisha la kwanza tu la wale wachezaji 7-9 wa kwanza, ukifanyika usajili sahihi hata kwa 70%, Simba itakuwa tofauti kabisa. Itabaki kumalizana na wakongwe waliobaki na kuagana nao kwa heshima.
 
Fanyeni transformation....Ili mfanye usajili mkubwa kama yanga

Watumien sana Yanga as role model wenu

Hakika mtafanikiwa
Yanga wametumia shortcut kukusanya kikosi cha AS Vita na ni faida ya misimu miwili. Kizazi hiki cha kina Mayele, Lomalisa na Bangala kinafikia ukingoni unaona jinsi wachezaji wameshachoka pamoja na rotation zinazofanyika. Baada ya msimu ujao Yanga itapata shida kwa sababu sidhani kama hawa kina Musonda, Mzize ni replacement za kiwango cha kina Mayele.
 
Madirisha mawili makubwa na dirisha dogo moja. Dirisha la kwanza tu la wale wachezaji 7-9 wa kwanza, ukifanyika usajili sahihi hata kwa 70%, Simba itakuwa tofauti kabisa. Itabaki kumalizana na wakongwe waliobaki na kuagana nao kwa heshima.
Yes na kocha apewe uhuru wa kuleta watu anaowataka
 
Tusiangalie udhaifu wa yanga bali tuangalie ubora wa simba mkuu
 
Tusiangalie udhaifu wa yanga bali tuangalie ubora wa simba mkuu
Nimeisemea kiujumla kumjibu huyo. Kuna wakati ilikuwa ukiiangalia Yanga inavyocheza unakubali jinsi wanavyocheza kitimu, ila sasa hivi hilo haulioni, wachezaji wameshachoka.

Ndiyo maana nasema hiyo shortcut ya kuchukua na kujaza wachezaji wenye uzoefu unapata matokeo haraka ila ya muda mfupi, baada ya hapo unaanza upya.
 
Mfano unaenda mgodini lengo likiwa ni kuchimba kupata dhahabu unfortunately unaishia njiani unatoka bila dhahabu hapo unakuwa umejipata?? Likewise Kwa Simba bado hawajajipata bali wanajipapatua, hizi sifa zisizo na maana ndo zinafanya mara Kwa mara waishie Quarter final..uwekezaji mkubwa zaidi unahitajika ili wajipate..kila la heri Simba kwenye kujitafuta ili kujipata na si kujipapatua.
 
Asante kwa maoni mkuu ila we made our job
 
John Bocco ameibeba sana Simba huko nyuma. Huu ni wakati wa kumwambia ahsante na kuagana naye. Naamini hata anapoingia zimebaki dakika mbili, tatu inakuwa ni shinikizo la viongozi sio uamuzi wa Robertino kocha
 
Onyango, Banda, Sawadogo, Ntibazonkiza,
 
Yahaya mbegu ameshasaini azam miaka 3
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…