toobiter
JF-Expert Member
- Dec 22, 2017
- 1,309
- 2,577
Jana nchi ya Morocco ilipata watalii millioni 89. Hatujui uraia wao, hatujui tabia zao, hatujui wameoa au kuolewa, ila tunafahamu jambo moja tu kuhusu watalii hawa, wanapenda soka na jana mechi ya Simba na Wydad ilikuwa mbuga waliyoitembelea.
Usishangae, mech ya jana imetazamwa na watu million 89 duniani kote na hii sio kawaida kwa timu za Afrika mashariki.
SIMBA inajitafuta ndani ya soka la Afrika? Jibu ni hapana tayari imejipata japo haina kombe lolote kama kielelezo cha ukubwa wake ndani ya afrika.
Lakini pamoja na kutochukua kombe lolote kubwa ndani ya Mashindano ya Klabu Bingwa au shirikisho bado hakuna timu Afrika ambayo ikipangiwa Simba italala raha mstarehe, lazima kila mtu afanye homework yake vizuri la sivyo anaweza kutana na lolote linalopatikana ndani ya dakika 90.
Wapi ilipo Simba, inataka kwenda wapi na nani ataambatana nayo (wachezaji), hili linabakia kuwa swali muhimu mnoo kwa wana Msimbazi.
Kuna kauli moja maarufu huwa inatolewa misibani hasa wakati wa kuzika kwamba tulikupenda ila mungu amekupenda zaidi.Kauli hii inawahusu saana baadhi ya wachezaji wa simba.
Kama simba inajiona nusu fainali au fainali kabisa ya Klabu Bingwa Afrika basi kuna wachezaji wakuagana nao. Sio kwamba ni wabaya au hawafai ila kwenye basi la Simba la Nusu Fainali au Fainali Klabu Bingwa hawa hawana siti au nafasi hata ya kusimama tu ndani ya gari. Kifupi hawatakiwi.
Waitwe waambiwe ukweli na waagwe kwa heshima, kama wanaipenda klabu na kama mikataba yao inaelekea mwisho basi waachwe wakatafute malisho kwingine muda wao umeisha. We unaonaje is it a road to hell or road to glory?
Nani aachwe na nani abaki nadhani mechi ya jana imetupa majibu mazuri kabisa. Nini maoni yako juu ya Simba ijayo na safari yao?
Karibu.