Simba kufungwa 5, Misri: Lawama kwa bechi la ufundi la Simba

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Posts
34,181
Reaction score
41,563
Unacheza AWAY GAME na timu ambayo ni nzuri yaani inakuzidi kila idara, unaamua kucheza 4-3-3 Yaani unaanza na washambuliaji watatu.

Huu ni uamuzi wa ajabu kabisa, isitoshe unajua fika kwamba back 4 yako si nzuri imetoka kupigwa 5 juzi juzi na bado unaamua kuanza na striker 3 yaani Okwi, Kagere na Rashid.

Hivi kocha hajifunzi ulaya mfano EPL ile mechi Chelsea aliyopigwa 4 au ile City aliyopigwa 2 wiki iliyopita?

Alitakiwa acheze na striker 1 lets say Okwi then midfielders 5 yaani Mkude na Kotei kati; Mzamilu Chama na Dilunga.

Rashid na Kagere hawakutakiwa kuanza game ya jana. Pia Beki ya kulia angeanza yule yule Gian; sasa mliona chocholo kule kulia watu wanangongeana one two utafikiri wanafanya mazoezi.

Mfumo ungekuwa kukaa nyuma kusubiri counter attacks; si aibu kupaki basi bwana, eti na wewe unafungua kama wao wewe.

Sasa kipi bora kupaki Bus ama kupigwa Hamsa???

Bechi la Ufundi wajitafakari.

acha niangalie mpira wa Man U hapa; utaona Leistercity watakavyocheza counter, Vady atakuwa mbele anasubiri chance ikitokea ni mbio.

Usijifanye fundi wakati ufundi unazidiwa, kubali kuwa underdog.
 
Na sisi Yanga tunajipanga tuwapige 6-0 mechi ya marudiano ligi kuu tarehe 16 ya mwezi huu wa pili teh teh teh!!
 
Eti mikia Congo alifanyiwa kitchen part misri send off tarehe 16/2/2019 anaolewa kabisaaa watu wana maneno yanga nimewavulia kofia😂😂😂
 
FUSO,

Hjui mpira hata kidgo...
Jana Simba wamecheza 4-5-1 halafu unasema 4-3-3. Ndugu ni kwel wachzaji wa simba walikua ndo wale wale ambao wanachezaga 4-3-3 lkn kwa jana ilibadilika. ukiangalia vzur utaona jan okwi hakua steka alikua winga na chama akua wing kama sik zote alikua inside ten anacheza nyuma ya kagere..
unakurupuka uko unasema walicheza 4-3-3..
shabiki bana[emoji12][emoji12][emoji12]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu FUSO,

Umesema kweli kabisa, ningekuwa mimi kulia pengine angecheza Mlipili au acheze namba 5 na 4 Juuk Murshid, Wawa na Gian nisingewachezesha.

Kwangu mimi Wawa is nowhere near beki kisiki Mlipili aliyeipatia Simba ubingwa wa ligi baada ya kuumia Mbonde

Sent using Jamii Forums mobile app
 
lazima uchezeshe natural midfielders wewe; uliona wapi Kagere akakaba? uliona wapi Rashid akakaba kusaidiana na wing back? kama hujui uliza. Pointi yangu kwa game kama ile ni kuchezesha natural midfielders 5 pale kati. Mfumo uwe kujilinda na kushambulia kwa kushitukiza.
 
Kama ndivyo basi mtoa mada yupo sahihi. Utawageuzaje washambuliaji kuwa viungo?

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Mkuu pengo la Kapombe na Nyoni lipo wazi lakini si muda wa kulia lia TRUST me kama Simba ingeanza na natural midfielders 5 basi mabao ingekuwa 0 - 0 au hata kama kipigo isingekiwa zaidi ya 2.
 
Mkuu pengo la Kapombe na Nyoni lipo wazi lakini si muda wa kulia lia TRUST me kama Simba ingeanza na natural midfielders 5 basi mabao ingekuwa 0 - 0 au hata kama kipigo isingekiwa zaidi ya 2.
Pamoja na natural midfielders nadhani walihitajika Orthodox defenders ndio maana nasema Mlipili alitakiwa acheze pamoja na Juuk Murshid, kulia angeweza kucheza Bukaba, natural defenders.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ndio mana wanasema mashabiki wanajua mpira kuliko makocha na wachezaji, kocha ambae kasoma fifa anakibali cha kufundisha sehem yyt dunian leo unatak kumfundisha et angeweka tipical midfilders...
oky emu twende mbele turudi nyuma, mech na as vita si aliweka ao viungo asili wote kweny eneo la kiungo nini walikifanya? matokeo yalikuaje..?
mpira syo siasa mzee
Sent from my EVA-L09 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, ongea kwa facts, mchezo na AS Vita alitumia 4-4-2 na siyo 4 -5 -1; Hata hivyo hii mifumo hubadilika badilika nachoongea mimi ni lazima ujilinde ukiwa ugenini hasa kama unajua timu yako haina ubora wa kiufundi kama timu pinzani. Siku hiyo alimwanzisha Okwi na Kagere. Hapa alitakiwa abakie striker mmoa kisha kiungo mwingi mkabaji awe ndani.

Nachosema mimi ni kwamba unajua unacheza ugenini, wachezaji wako hawana ubora kama ule wa timu pinzani kwa nini usijaribu plan B ?? Nani atakucheka? Huwezi kucheza mpira ugenini kwa style ile ile unayocheza taifa na Stand United kaka, utaumia.

Tukisema hivi mnasema eti siasa, siasa ipo wapi hapa?? Kupaki basi si dhambi hata wakikucheka sawa ila walau umetoka na ka pointi kamoja ama kupunguza idadi ya mabao ya kufungwa.

Huwezi kufungwa goli 10 mechi mbilli za away huu udhaifu wa kiunfundi.
 
Hao makocha wa FIFA huwa wanafukuzwa ulaya kwa kelele za mashabiki na wapenzi, usidharau watu waliopo kwenye stands wanajua mpira pia.

Ukiwa na degree ya kilimo sio necessarilly kuwa unajua kulima, kulima ni more practical kuliko theories za darasani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata ingetumika formation ya kupak basi kama morinyo, inabidi tukubali ya kuwa quality ya wacgezaji wa al haly na simba ni tofauti kabisa. Kuanzia individual hadi squad, Hivyo visingizio vinavyoletwa hapa ni kama mnataka kutuaminisha kuwa zilikutana timu za kiwango kimoja bali tumefungwa kutokana na mbinu za kiufundi. Yaani wale wachezaji wa al haly hata kuchukua mpira mguuni kwao tulikuwa hatuwezi, tunasubili pasi ipotee au goal kick. Siwezi kumlaumu kocha kwa quality ya wachezaji wa simba nilivyowaona, sisi tulisajili wachezaji wa kiwango cha ligi yetu, simba ni bora kwenye ligi yetu, ila bado sio bora kwenye klab bingwa, hata morinyo na pep ukiwapa timu cha kwanza wanatafuta quality players, hizo mbinu sijui 4 4 2 sijui 5 3 2 hazichezi mpira. Tukubali tulizidiwa.
 
Unapocheza ugenini ni tofauti ukicheza nyumbani, weka maneno yako vizuri siku wakija hawa waarabu Taifa au hao AS Vita uone Mpira utakavyobadilika.

Simba hihi imeshinda game mbili nyumbani, sasa iweje ugenini timu ipigwe 5 mtungi game mbili? ufundi kaka ufundi. maana kama ni Wawa mbona kacheza game zote hadi walipofikia kwenye makundi?

Ushindi si kuwa na wachezaji bora tu bali ni Mbinu. angalia Man kwa sasa inavyochakaza watu wakati timu liliuwa bovu hatari.

Hapa Benchi liwaombe radhi washabiki ili waanze viporo vya ligi moja pamoja.
 
Sawa upo sahihi lakini viwango vya wachezaji wetu na wao vina lingana ?akiri ya uwanjani na wachezaji wetu IPO sawa nao?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa upo sahihi lakini viwango vya wachezaji wetu na wao vina lingana ?akiri ya uwanjani na wachezaji wetu IPO sawa nao?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli, suala la kuwaweka sawa wachezaji ki saikolojia, motisha nk ni suala la bechi la ufundi pia, Bechi la ufundi siyo mbinu za uwanjani tu hapana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…