Simba kukipiga na Gor Mahia Tarehe 15 NOV 2026 nchini Kenya katika kumbukizi ya Kifo cha Raila Odinga

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Mashabiki wa soka Afrika Mashariki wanaweza kushuhudia pambano kubwa la kimataifa kati ya vigogo wa soka kutoka Tanzania na Kenya, baada ya Simba SC kuripotiwa kupangwa kukutana na Gor Mahia FC katika michuano maalumu ya Raila Odinga Super Cup.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa, mchezo huo unapendekezwa kuchezwa Novemba 15, 2026, katika Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi, Kenya.

Michuano hiyo imeandaliwa kwa ajili ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Amolo Odinga, aliyefariki dunia Oktoba 15, 2025.

Iwapo mchezo huo utathibitishwa, utawakutanisha miamba miwili ya soka kutoka Afrika Mashariki. Simba SC, maarufu kama Wekundu wa Msimbazi, itakuwa ikikabiliana na Gor Mahia, inayotambulika pia kwa jina la K'Ogalo, moja ya klabu zenye mafanikio makubwa nchini Kenya.

Mbali na ushindani wa ndani ya uwanja, pambano hilo linatarajiwa kuwa fursa ya kuimarisha mahusiano ya kimichezo kati ya Tanzania na Kenya pamoja na kuendeleza mshikamano kupitia mchezo wa soka.

Hata hivyo, hadi sasa taarifa za kukutana kwa timu hizo zinapaswa kuchukuliwa kama taarifa zilizoripotiwa, kwani ushiriki wa Simba SC na Gor Mahia bado unahitaji uthibitisho rasmi kutoka kwa waandaaji au klabu husika.

Endapo litathibitishwa, pambano hilo linaweza kuwa miongoni mwa matukio makubwa ya soka yatakayovutia mashabiki wa Afrika Mashariki mwezi Novemba mwaka huu.
 
Binafsi ningetamana club za Afrika Mashariki zifanye vizuri huko CAF, tukawa na utawala wa kisoka
 
Simba ikikubali kitacheza kikosi B
 
Mechi hiyo kama kweli itachezwa itakua ni kipimo kizuri kwa Lunyasi kuelekea mchezo wao wa CCL dhidi ya Orlando Pirates tatehe 27 November

Hawa Gor walishawahi kutwaa kombe la Shirikisho Barani Afrika mwaka 1987. Wakati huo lilikua linaitwa Kombe la Washindi Barani Afrika(Cup Winners Cup), Ilikua ni michuano migumu sana maana kila nchi ilitoa muakiishi mmoja kwenye CCL na mmoja kwenye Kombe la Washindi

Walicheza na Esparence. Mechi ya kwanza Jijini Tunis ilikua 1-1 na marudiano pale Nairobi Gor wakafanikiwa kushikilia bomba wakatoka sare ya bila kufungana hivyo goli la ugenini likawapa ubingwa
 
Yeah
 
Back
Top Bottom